Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia Ugonjwa wa kaswende, tunajua wazi kuwa Ugonjwa huu unasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kufanya ngono zembe na njia nyingine kwa hiyo tunaweza kuzuia kusambaa na kuenea kwa ugonjwa huu kwa n
1.Njia ya kwanza kabisa ni kutibu Ugonjwa huu mara tu unapoonekana.
Matibabu ni njia mojawapo ya pekee kuliko zote na wakati wa matibabu ni lazima kuachana na kujamiiana na pia wapenzi wote wawili wanapaswa kutibiwa au kama ni wanafamilia wanapaswa kutibiwa wote kwa sababu unapotibu mmoja unakuwa unafanya kazi bure, hivyo matibabu kwa wapenzi ni kitu cha lazima.
2. Dawa ambazo zinapaswa kutumika ni dawa inayoitwa benzathrine penicillin ambayo utolewa kwa dozi moja,au mtu kama ana mzio au aleji na benzathrine penicillin anaweza kutumia doxycycline gramu mia moja ambayo utumika mara mbili kwa siku dawa hii uenda mpaka siku kumi na tano.
3. Pia na dawa ya Erythromycin inaweza kutumika hasa kwa Mama wajawazito , nayo hii utumika kama kuna mtu mwenye mzio au aleji na dawa ya benzathrine penicillin na doxycycline,kwa hiyo hii ni nzuri hasa kwa wajawazito.
4. Kama Ugonjwa huu wa kaswende una mwaka zaidi ya mmoja daima tumia benzathrine penicillin G 2.4 MU kupitia kwenye nyama au kwa kitaalamu huitwa intramuscular kwa wiki tatu.
5. Baada ya kufahamu Ugonjwa huu wa kaswende ni vizuri kabisa kutumia matibabu kama tulivyoona ila matibabu haya yanapaswa kutumika kwa kuongozwa na wataalamu wa afya, usitumike matibabu haya kiholela kwa sababu unaweza kupata matatizo mbalimbali, kwa mfano kama una aleji na dawa fulani ukitumia na uko mazingira ya nyumbani ni shida na unaweza kuleta matatizo mbalimbali kwa hiyo ni vizuri kutumia wataalamu wa afya.
6. Vilevile tunapaswa kutoa elimu kwa umma au jamii nzima kama kuna kuongeza kwa Ugonjwa huu kwa sababu kwa wajawazito unaleta shida kubwa ambayo ni pamoja na kujifungua mtoto mfu au mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo la macho, kwa hiyo matibabu ni lazima na yapo na Ugonjwa huu unatibika. Na tupunguze kuendekeza ugonjwa huu daima juwa na mpenzi mmoja na wa maisha hali huu utapunguza kuendelea kuwepo kwa janga hili.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa Ugonjwa huu wa ukimwi ukishasmbaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuleta madhara makubwa kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na mambo hatari yanayosababisha ugonjwa wa moyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwahudumia wenye Maambukizi kwenye mifupa, ni njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuwasaidia wenye Maambukizi kwenye mifupa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ukimwi za kwenye ulimi na mdomo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za maambukizi kwenye ovari, ni maambukizi ambayo hutokea kwenye ovari na kusababisha matatizo makubwa kama mgonjwa haujatibiwa mapema.
Soma Zaidi...Malaria inaweza kumpata mtu yeyote bila ya kujali mri.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za jeraha kali kwenye ubongo, ni majeraha ambayo utokea kwenye ubongo pale ambapo mtu anapata ajali au amepigwa na kitu chochote kigumu kichwni, zifuatazo ni dalili za jeraha kali kwenye ubongo
Soma Zaidi...Tezi dume ambayo haijashuka si ya kawaida kwa ujumla, lakini ni ya kawaida kwa wavulana waliozaliwa kabla ya wakati.na muda mwingine zikipanda tumboni huwa hazishuki kabisa kwenye korodani.
Soma Zaidi...