Huwenda ukawa ni moja kati ya watu wanaotaka kujuwa juu ya dalili za ukimwi. Kama wewe ni katika watu hawa tambuwa kuwa kuna dalili za VVU (hiv) na dalili za ukimwi. Makala hii itakwenda kukuletea dalili kuu za mwanzo za VVU na HIV kuanzia wiki tatu za mw
JE UNAZIJUWA DALILI ZA UKIMWI?
Yaliyomo
Ukiwa na maoni, mapendekezo ama maswali wasiliana nasi kupitia komenti hapo chini ana namba ya simu.
VVU ni ufupisho wa maneno Virusi Vya Ukimwi. Hivi ni virusi vinavyo sababisha upungufu wa kinga mwilini. Ni katika aina ya virusi inayofahamika kitaalamu kama retrovisus. Virusi hivi vinaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwingine kwenda kwa mwingini kupitia muingiliano wa majimaji ya mwilini (body fluid). ni vurisi ambavyo kushambulia aina ya seli inayofahamika kama CD4.
Nini maana ya UKIMWI?
UKIMWI ni ufupisho wa maneno Upungufu Wa Kinga Mwilini. Upungufu huu hutokea baada ya mwili kushambuliwa na virusi aina ya VVU. Tunasema mtu ana upungufu wa kinga mwilini endapo seli zake za CD4 zitakuwa chini ya 200 kwenye kipimo. Kutoka kupata VVU hadi kuonyesha kupata upungufu wa kinga inaweza kuanzia miaka 5 hadi 5 baada ya maambukizo.
Historia fupi ya UKIMWI na asili yake.
Historia ya ukimwi imeanza zamani sana hata kabla ya neno IKIMWI kuanza kutumoka. Kabla hatujaona kwa ufupi hi historia hii ni vyema tukaanza kujuwa nini chanzo cha ukimwi? Kuna utata wa kutokukubaliana kauli juu ya chanzo cha UKIMWI. Wapo wanaodai kuwa ukimwiumetengenezwa kwenye maabara kisha kusambazwa, kuna wanaosea kuwa ni Mwenyezi Mungu ametowa adhabu ila wanasayansi wanaamini kuwa chanzo cha ukimwi ni Masokwe.
Kwa ufupi zipo nadharia zaidi ya 10 zinazojaribu kueleza nini chanzo cha UKIMWI. Kisayansi inathibitika kuwa ukimwi chanzo chake huwenda ikawa ni masokwe. Hoja hii pia inatiliwa nguvu na historia katika maeneo mbalimbali kama Kongo na maeneo mengine ya Afrika ya Magharibi.
Kwa ufupi ni kuwa tafiti zinaoyesha kuwa virusi vya VVU vilitika kwenye masokwewakati wa uwindaji, huwenda kuitia majeraha ama namna nyingine kulitokea mwingiliano wa majimaji ya mwili na ya sokwe. Virusi vikaanza kubadilika kutoka hatuwa moja hadi nyingine hadi kufikia leo. Kauli hii inatiliwa nguvu baada ya kupatikana kwa taarifa za kihistoria ambazo huwenda miaka ya 1950 watu wa maeneo ya UGANDA NA Kongo1920 walipata upungufu wa kinga Mwilini na walikuwa wanakufa kwa maradhi ambayo yana uhusiano na UKIMWI.
Kwa mara ya kwanza dunia ailianza kupata taharuki juu ya uwepo vivirusi hivi miaka ya 1980 ha hapo virusi hivi vikajulikana kwa jina la HTLV-III/LAV na nchini Uganda ugonjwauliosababishwa na virusi hivi ulikuwa ukifahamika kwa jina la slim. Mpaka kufikia mwaka 1986 international Committee on Taxonomy of Viruses wakaviita virusi hivi kama HIV na ugonjwa unaosababihwa na virusi hivi uitwe AIDs na hapo jina UKIMWI ndipo lilipoanzia.
Hadi kufikia miaka ya 1988 WHO walitangaza siku ya ukimwi duniani. Mapaka kufikia mwaka 1989 maambukizi kidunia yakafikia 400000 kwa makadirio ya moja wa mataifa. Hadi kufikia mwaka 1990 mwezi wa 10 dawa ya kwanza ya kupunguza makali ya virusi tunazozijuwa hivi leo kama ARV ilitangazwa nayo ilikuwa ni zidovidine (AZT).
Ni zipi dalili za mwanzo za HIV?
Hili ni swali la msingi sana na ni zuri pia. Kwa ufupi dalili za mwanzo za HIV huweza kujitokeza kuanzia wiki 2 toka kupata maambikizi, hadi kufikia wiki ya sita toka kupata maambukizi. Kuna wengine wanapita wiki hizi hata bila ya kuona dalili yeyote ile. Lakini pia dalili hizi huweza kuingiliana na maradhi mengine, hivyo haimaanishi kila mwenye dalili hizi atakuwa ni muathirika. Dalili hizo ni kama:-
Dalili hizi huweza kuchukuwa muda mchache sana ndani ya wiki za mwanzo wiki ya 2 mpaka ya 6. huwenda pia zikachelewa ama zikawahi. Dalili hizi si zenye kudumu, yaani zitapotea baada ya muda na hazihitaji matibabu yeyote. Katika kipindi ili kiwango cha virusi kwenye damu ni kikubwa sana na huzaliana kwa haraka sana.
Baada ya dalili hizi kutokea bado virusi vya ukimwi haviweze kuonekana kwenye kipimo cha HIV. Itachukuwa kuanzia wiki 3 mapaka miezi mitatu kwa virusi kuweza kuonekana kwenye kipimo na mtu kuambiwa ni muathirika. Katika kipindi hiki mtu anaweza kumuambukiza mtu mwingine kwa uahisi.
Baada ya miezi mitatu ya mwanza dalili zote za HIV hazitaweza tena kuonekana na hapa mtua ataishi kawaida bila ya kuhisi chochote. Virusi vitaanza kupunguwa kwenye damu na kuhamia maeneo mengine ya mwili na kujifucha huko ili kujijengea makazi ya milele. Wakati huu vitaendelea kuchambulia seli za CD4 kidogo kidogo.
Seli za Cd4 ni nini?
Hizi ni seli ambazo kazi yake ni kupambana na vijidudu vya maradhi kama virusi, bakteria, fanfasi na protozoa. Seli hizi zinatafuta vijidudu hivi popote vilipo kwente mwili. Piti vikikutana nae vinatoa kemikali ambazi zitauwa kijidudu hiko. Kwa ufupi wa maneno seli za CD4 NI ASKARI MWILINI. Sasa virisi vya VVU vyenyewe vinatafuta sei hizi za CD4 popote zilipo na kuanza kuzishambulia na kuziuwa. Hii ni sawa na kusema VVU hushambulia askari wa mwili. Na ikitokea askari kapigwa basi mwili hauna ulizi dhidi ya maradhi.
Hatuwa za kufikia UKIMWI
Kikawaida seli za CD4 zipokuanzia 500 mpaka 1600 kwa mtu mwenye afya. Sasa kama tulivyoona kuwa VVU hushambulia seli hizi na kuzimaliza. Hivyo endapo zitafikia chnini ya 200 mtu huyu huambiwa ana upungufu wa kinga mwilini au UKIMWI. Na hadi kufikia hapa huwenda mtu huyu aliambukizwa VVU yapata miaka mitano hadi kumi iliyopita. Kufikia hapa ndipo mtu ataanza kuona dalili za UKIMWI.
Je ni zipi dalili za UKIMWI?
Je ni njia zipi HIV huambukizwa
Kumekuwa na mawazo mengi na potifu kuhusu njia ambazo virusi vya VVU huambukizwa. Hapa tutaona baadhi tu ya njia ambazo VVU huambukizwa. Kisha tutaona njia ambazo watu hudhania huambukizwa ila ukweli ni kuwa haziambukizi njia ambazo VVU huambukizwa ni kama:-
Nia hizi haziwezi kuambukiza VVU
Je ipo dawa ya VVU na UKIMWI?
Kwa ufupi dawa ya kutibu na kumaliza VVU hakuna, ila matumaini yapo kuwa itapatikana. Mapka sasa kuna mgonjwa mmoja ambaye ainaaminika amepona kabisa UKIMWI. Ilamatibabu ambayo alipatiwa hayaweza kutumika kwa watu wengine kutokana na hatari yake. M hii inaleta matumaini kuwa tafiti zinahitajika zaidi na kuna matumaini pia ya kupatikana dawa kwa siku za mbeleni.
Kwa sasa tunayo matibabu ambayo atapatiwa muathirika ili kuzuia virusi visiendelee kuharibu kinga za mwili. Matibabu haya yanajulikana kama ART (antirteoviral therapy) ambapo mgonjwa atapatiwa dawa za ARV. Endapo mtu atatumia vyema itamsaidia kuzuia uharibifu wa kinga zake na pia itambunguza hatari ya kuambukiza wengine.
Je vipi kuhusu kinga ya UKIMWI?
Yes kinga ya ukimwi ipo nayo ni kondomu. Kama itatumika vyema inaweza kukinga kwa asilimia kubwa na kumuweka mtu salama. Ila tambuwa kuwa unaweza kutumia kondomu na ukaathirika kwani njia za maambukizi ni njingi. Kazi kuu ya kondomu ni kulinda maambukizi yanayopatikana kwa njia ya ngono. Zingatia haya:
Tukutane makala nyingie tutaona zaidi kwa nini unaweza kufanya ngono na muathirika na usiathirike.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Mapigo ya moyo ni hisia za kuwa na moyo wa haraka, Kupepesuka au kudunda. Mapigo ya moyo yanaweza kuchochewa na mafadhaiko, mazoezi, dawa au, mara chache, hali ya kiafya. Ingawa mapigo ya moyo yanaweza kuwa ya kutisha, kwa kawaida hayana madhara. Katik
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za kuonyesha kuwa Kuna maambukizi kwenye kitovu hasa hasa chini ya kitovu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za maumivu ambayo yanasikika kwenye magoti, huu ni ugonjwa ambao umewapata walio wengi na bado ni kilio kwa walio wengi kwa vijana na kwa wazee, Kuna wataalamu mbalimbali ambao wameweza kugundua sababu za maumivu kwenye mago
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za fangasi uken, hizi ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la fangasi uken.
Soma Zaidi...Kiufipi posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na sababu zinazopelekea tumbo kujaa gesi
Soma Zaidi...Bila shaka umeshawahi kujiuliza kuwa je mate yanaambukiza HIV ama laa. Na kama hayaambukizi ni kwa sababu gani. Sio mate tu pia kuhusu jasho kama pia linaweza kuambukiza ukimwi ama HIV. Wapo pia wanajiuliza kuhusu mkojo kama unaweza kuambukizwa HIV. Kar
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na was Uharibifu wa seli nyekundu za damu ambapo hujulikana Kama Ugonjwa wa Hemolytic uremic (HUS) ni hali inayotokana na uharibifu usio wa kawaida wa seli nyekundu za damu mapema. Mara tu mchakato huu unapoanza, seli nye
Soma Zaidi...Jipu la jino ni mfuko wa usaha unaosababishwa na maambukizi ya bakteria. Jipu linaweza kutokea katika maeneo tofauti ya jino kwa sababu tofauti.
Soma Zaidi...Dalili za HIV zina utofauti na dalili za UKIMWI. Kwani HIV huwezakuonyesha dalili wiki ya pili hadi ya sita baada ya kuathirika kisha zinapotea, lakini dalili za UKIMWI huwezakutokea baada ya miaka 5 hadi 10.
Soma Zaidi...Psti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi ya tezi za mate ambao hujulikana Kama MABUSHA (mumps) ni maambukizi ya virusi ambayo kimsingi huathiri tezi mojawapo ya jozi tatu za tezi za mate zinazotoa mate, zilizo chini na mbele ya masikio
Soma Zaidi...