Vitamini D ni vitamini inayosaidia miili yetu iweze kuvyonza madini ya calcium, magnesium na phosphate. Vitamini D hutengenezwa chini ya ngozi kwa kutumia mwanga wa jua. Vitamini D ipo katika makundi makuu mawili nayo ni vitamini D2 na vitamini D3. Vitamini vipo katiaka makundi mengi kuna vitamini A, B, C, D, E na K . katika makala hii tutakwenda kuona zaidi kuhusu vitamini D, namna ambavyo vitamini D hutengenezwa mwilini, Je ni zipi kazi za vitamini D, na upungufu wake unasababisha athari gani mwilini?.
YALIYOMO:
1.Maana ya vitamini D
2.Makundi ya vitamini D
3.Kazi za vitamini D
4.Chanzo cha votamini D
5.Upungufu wa vitamini D
Maana ya Vitamini D
Vitamini D ni matika fat soluble vitamin ambayo imetokana compound za cholesterol. Vitamini D vimegunduliwa mwaka 1922 na Mwanasayansi anayefahamika kwa jina Elmer McCollum. Historia ya uchunguzi huu wa vitamini D ulianzia toka mwaka 1914 wakati Elmer McCollum na Marguerite Davis walipogundua vitamini A
Vitamini hivi vimeitwa D kwa sababu ndio vitamini vya nne kugundulika toka A, B, C na sasa ni vitamini D. ugunduzi wa vitamini D ulianzia kwenye mbwa mgonjwa ambaye alikuwa ana matege. Baadaye ikajulikana kuwa mbwa aliweza kupona matege kwa sababu ya chembechembe amazo baadaye ndiyo zikaitwa vitamini D.
Makundi ya vitamini D
Kama ilivyokuwa vitamini K na vitamini B zina makundi mengi. Basi hata hivyo vitamini D vimegawanyika katika makundi kadhaa, makuu katika kundi hilo ni vitamini D2 na bitamini D3. makundi haya mawili kwa pamoja ndiyo hufahamka kama vitamini D.
Vitamini D1 na vitamini D2 kwa pamoja pia huitwa calciferol. Vitamini D2 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwa ka 1931 na vitamini D3 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwaka 1935.
Kazi za vitamini D
Katika miili yetu vitamini D ina kazi kuu ya kufanya metabolism ya madini ya calcium. Kwa lugha nyepesi ni kuhakikisha kuwa unyonzwaji wa madini ya chumvi ambayo ni calcium, magnesium na phosphate unafanyika vyema ndani ya utumbo mdogo.
Faida za vitamini D:
1.Husaidia kufyonza mwili kufuonza madini ya calcium
2.Husaidia kuboresha afya ya mifupa
3.Husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani
4.Husaidia kuboresha mfumo wa faya
5.Kupunguza uzito na kitambi
Chanzo cha vitamini D
Chanzo kikuu cha vitamini D ni mwanga wa jua ambao husaidia katika utengenezwaji wa vitamini D chini ya ngozi. Kama mtu hataweza kupata mwangaza wa jua vyema kuna uwezekano wa kupata upungufu wa vitamini D.
Pia tunaweza kupata vitamini D kutoka katika vyakula na mboga, kama vile:-
1.Uyoga
2.Yai lililopikwa
3.Maini
4.Samaki
Upungufu wa vitamini D
Upungufu wa vitamini D unaweza kusababisha athari kubwa kwenye afya. Miongoni mwa athari hizo ni:-
1.Matege
2.Udhaifu wa mifupa
3.Mifupa kuvunjika kwa urahisi
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Hivi ni vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo. mwenye vidonda vya tumbo hatakiwi kula vyakula hivi
Soma Zaidi...Hii ni orodha ya matunda yenye vitamini C kwa wingi sana ikiwemo machungwa, mapera na mapapai
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza faida na matumizi ya asali mwilini.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu upungufu wa protini na dalili zake
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za karoti na umuhimu wake kiafya
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi za madini ya chuma mwilini,Ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini na pia utokana na vyakula mbalimbali ambavyo upatikana kwenye wanyama na mimea. Zifuatazo ni kazi za madini ya chuma.
Soma Zaidi...