Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Faida (matunda) ya kusimamisha swala katika jamii.
Swala za faradhi zikisimamishwa vilivyo faida zifuatazo hupatikana katika jamii;
Usafi na unadhifu wa mwili.
Kwani muislamu hawezi kuswali mpaka ahakikishe kuwa msafi (twahara) kikamilifu katika nguo na mwili pia na sehemu ya kuswalia.
Rejea Quran (7:31).
Utakaso wa Nafsi.
Kwa kutekeleza sharti na nguzo za swala pamoja na mnyenyekevu katika swala, hupelekea mja kuwa mtiifu ipasavyo kwa Mola wake muda wote.
Swala za jamaa huimarisha udugu, umoja na usawa.
Kuswali katika jamaa huleta udugu, umoja na usawa wa kweli na kuepusha mfarakano, chuki na ubaguzi miongoni mwa waislamu.
Rejea Quran (49:10,13).
Swala za jamaa huwafunza waislamu uongozi bora.
Swala huongozwa na imamu (kiongozi) wa waumini husika anayetokana na wao kutokana na sifa maalumu za kuwa kiongozi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi asili ya madini ya Shaba, ni sehemu ambapo madini ya Shaba yanaweza kupatikana ni katika mimea na wanyama
Soma Zaidi...utajifunza njia za kuzuia kiungulia, dalili za kiungulia na dawa ya kutibu kiungulia.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mahindi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula bamia
Soma Zaidi...