Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii
Hii ni hali inayowapata wanawake kwa kiasi kikubwa wakati wanaposhiriki tendo la ndoa. Maumivu haya pia yanaweza kumpata mwanaume ila kwa uchache sana. Hali hii kitaalamu inafahamika kama dyspareunia.
Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa uume unapoingia kwa mara ya kwanza, ama wakati wote wa kuingia na kutoka ama baada ya kumaliza tendo la ndoa. Maumivu ya wakati wa tendo la ndoa yanaweza kutokea kwenye uke, ama uume ama kwenye tumbo kwa kwa wanawake. Makala hii itakwenda kukuorodheshea sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa
1.Uke kuwa mkavu kutokana na maandalizi mabovu kabla ya kuingiza uume. Pia inaweza kuwa ni kutokana na kukosa hamu ya kushiriki tendo.
2.Kuwepo kwa majeraha kwenye uume ama uke. Majeraha haya yanaweza kuwa ni kukeketwa ana ya namna nyingine.
3.Kuwepo kwa uvimbe ama ukawa na matatizo ya ngozi katika sehemu za siri. Haya yote yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kuingia kwa uume.
4.Maumbile ya uke. Wakati mwingine jinsi uke ulivyo inaweza kuwa ni tatizo. Kuwa uke mwingine unatabia ya kubana misui yake. Hali hii inaweza kupelekea maumivu wakai wa kupenya kwa uume.
5.Matatizo ya kimaumbile, kwa mfano kuwa na ukilema kwenye uke, ama kuwa na nyama ama ngozi ambayo inaweza kuzuia kupenya kwa uume.
6.Kuwepo kwa maradhi katka mfumo wa uzazi wa kike. Matatizo haya ya kiafya yanaweza kuwa kwenye ovari, ama kukawa na uvimbe ndani ya kizazi ama kukawa na shida katika mirija ya uretas.
7.Kufanyiwa baadhi ya matibabu katika maeneo ya siri. Kwa mfano baadhi ya matibabu ya saratani katika sehemu za siri, matibabu haya yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa
8.Matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawaso. Wakati mwingine uoga, kuwa na msongo wa mawazo ama kukumbuka maumivu uliyoyappata siku zanyuma, hali hizi zinaweza kupelekea maumivu wakati mwingine.
9.Staili iliyotumika wakati wa kufanya sex. Wakati mwingine mikao ya kufanya tendo la ndoa inaweza kuwa ni sababu ya maumivu. Ni vyema kutumia mikao iliyo rahisi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye tumbo la uzazi la Mama pindi anapobeba mimba, ni mabadiliko yanayotokea kwa mwanamke anapobeba mimba kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi changamoto za kwenye ndoa kwa wale waliotoa mimba mara Kwa mara,hizi ni changamoto za wakati wa kufanya tendo na mme wake au mtu mwingine kwa ajili ya kupata mtoto.
Soma Zaidi...Kipimo cha Mlimba huweza kuonyesha mimba changa mapema sana. Pia ni rahisi kutumia na kinapatikana kwa bei nafuu. Je ungeoendavkujuwa ni muda gani kinatoa majibu sahihi?
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Mimba inapotoka ina dalili, na zipo sababu kadhaa za kutoka kwa mimba. Je utazuiaje mimba kutoka. Soma makala hii
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa akina dada.
Soma Zaidi...KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zilijitokeza zinaweza kusababisha ugumba hasa kwa wanawake, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa makini kwa Dalili hizi hasa kwa wadada, kama kuna uwezekano wa matibabu tibu mapema ili kuepuka tatizo la kuwa mgumba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za mimba ya miezi kuanzia minne mpaka sita kutoka , Kuna kipindi mimba kuanzia miezi mimne mpaka sita utoka kwa sababu mbalimbali.
Soma Zaidi...