KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.
KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO
Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito. Kitaalamu hali hii hutambulika kama odema. Wakati mwingine si miguu tu ndio huvimba bali mikono, nyayo na uso huweza kuvimba. Ijapouwa huku kukuvimba kwa ghafla kwa uso na mikono ni dalili ya maradhi mengine kama preeclampsia.
Hali hii ya kuvimba kwa miguu huweza kuwapata wanawake katika kipindi chote cha ujauzito, iwe wajauzito ulio mchanga, ama kipindi cha katikati cha ujauzito ama kipindi cha mwisho cha ujauzito. Katika hali ya kawaida kuvimba kwa miguu kwa wajawazito sio jambo la kusumbua kiafya yaani kusema kuwa ni tatizo kubwa. Hapana hii ni kawaida kwa wajawazito.
Kuvimba huku kunaweza kuwa ni tatiko kama kutaweza kuambatana na baadhi ya matatizo mengine ya kiafya kama maumivu makali ya kicha, kizunguzungu, kutokwa na damu, kushinwa kuona kwa usahihi ama kushinwa kupumua ama kupumua kwa taabu, hali hizi kuweza kuashiria hatari. Ni vyema mjamzito awahi kituo cha afya kama ana hali hizi.
Sababu za kutokea kwa vimbe hizi ni mabadiliko ya mwilini yanayopatikana wakati wa ujauzito. Kuongezeka kwa damu mwilini na kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kuchangia zaidi hali hii. Halikadhalika ongezeko la homoni maalumu zinazotolewa wakati wa ujauzito. Haya yote kwa pamoja huchangia kutokea hali hizi za kuvimba.
Tofauti na sababu hizi pia zipo nyingine kama mabadiliko ya hali ya hewa. Hapa tunazungumzia joto, ambalo pia ni sababu ya kuvimba. Sababu nyingine ni kutokunywa maji ya kutosha, matatizo ya homoni yaani homone imbalance. Kukaachini kwa muda mrefu ukaaji wa kukalia miguu. Ama kusimama kwa muda mefu.
Kupunguza ama kuepuka hali hii ni vyema kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kukaa kivulini, kulalia upande kwa kushoto unapolala. Hakikisha unakula mlo kamili, hakikisha kuwa unakunywa maji ya kutoka kwa siku. Na hata ukizidisha ni faida kwako. Epuka kusimama kwa muda mrefu ama kukaa kwa kukalia mguu. Epuka kukaa kwa muda mrefu kwa staili moja. Kuna matatizo mengu ya kiafya yanayoambatana na ujauzito, ni vyema mjamzito akiwa makini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi uzazi wa mpango kwa njia ya kumwaga shahawa nje, hii ni njia mojawapo kati ya njia za uzazi wa mpango ambapo mwanaume humwaga nje mbegu ili asimpatie Mama mimba.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu mbalimbali za mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mkubwa, mara nyingi tatizo hili uwakumba akina mama mbalimbali ambapo mtoto uzaliwa akiwa na uzito mkubwa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za mama kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, hili ni tatizo ambalo uwapata akina Mama wengi wanapomaliza kujifungua kwa hiyo tutaweza kuziona sababu zinazosababishwa na tatizo hili.
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukufundisha baadhi ya dalili za uchungu kwa mama mjamzito.
Soma Zaidi...Kutoka na majimaji ka uchache kwa mwanamke sio jambo lakishangaa sana. Damu hii inawezapiabkikbatana damu na maumivu makali.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea hatua za ukuaji mimba na dalili zake
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi athari za kuweka vitu ukeni, tunajua kwa wakati huu kadri ya kukua kwa sayansi na teknolojia watu wanaendelea kugundua mbinu mbalimbali ili waweze kuwafurahisha wapenzi wao wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili za saratani kwa watoto, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto na ikiwa mlezi au mzazi akiziona tu anaweza kutambua mara moja kwamba hii ni saratani au la na kama bado ana wasiwasi anaweza kupata msaada zaidi kutoka kwa wataa
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu damu, uteute na maji yanayotoka ukeni kipindi cha ujauzito
Soma Zaidi...