Mimba inapotoka ina dalili, na zipo sababu kadhaa za kutoka kwa mimba. Je utazuiaje mimba kutoka. Soma makala hii
Kutoka kwa ujauzito mara nyimgi hutokea katika hiki kipindi cha kwanza yaani ndani ya wiki 12 za mwanzo. Inakadiriwa kuwa robo ya mimba hutoka. Mwanamke anaweza akatokwa na mimba kwa kujuwa ana bila ya kujuwa. Inaweza kutokea pia mwanamke akabeba ujauzito na ukatoka bila kuwa na habari yeyote kama alikuwa na miba na imetoka. Ni kuwa mimba inaweza kutoka bila ya kuwa na dalili za wazi kama kutoka na damu.
Dalili za kutoka kwa mimba:
A.Maumivu ya mgongo
B.Kuharisha
C.Kichefuchefu
D.Maumivu ya maeneo ya nyonga na kiuno kama unahisi unataka kuingia kwenye siku zako
E.Maumivu makali ya tumbo
F.Kutokwa na majimaji kwenye uke.
G.Kutokwa na vitu kama vijioande vya nyama vijidogo kwenye uke
H.Uchovu mkali sana usio na sababu
I.Kupotea kwa dalili nyingine za ujauzito
J.Kutokwa na damu mabonge manonge ama damu nyingi
Kumbuka hizi ni dalili tu, unaweza kuwa nazo na ujauzito ukawa salama kabisa. Ukiona unahisi dalili hizo muone daktari atathibitisha vyema kwa vipimo ikiwemo utrasound ama kuangalia kiwango cha homoni ya ujjauzito kwneye damu yako.
Ni zipi sababu za kutoka kwa mimba?
Mara nyingi kutoka kwa ujauzito kunaweza kusababishwa na chromosomal abnormalities. Hili ni tatizo la kigenetics. Hapa seli za mtoto zinashindwa kugawanyika vyema na kukuza mtoto. Sababu nyingine za kutoka ujauzito ni:-
A.Matatizo katika homoni kuwa nyingi sana ama kidogo sana
B.Kama mama mjamzito ana kisukari na hafuati masharti vyema
C.Mazingira yanaweza kuchangia kama kuna mionzi hatari kama ya madini ya uranium
D.Maambukizi na mashambulizi ya vijidudu kama bakteria kwenye via vya uzazi.
E.Shida katika mlango wa uzazi (cevix)
F.Kutumia madawa kiholela ama kutumia madawa kusudi kwa lengo la kutoa ujauzito
G.Ugonjwa wa endometriosis (kuvimba kwa kuta za mji wa mimba “uterus”)
H.Magonjwa ya ngono kama gonoria
Sababu nyingine za kutoka kwa mimba
A.Utapia mlo
B.Kuwa na kitambi
C.Matumizi ya vilevi na sigara
D.Maradhi ya tezi ya thyroid
E.Shinikizo la damu la juu sana
NITAZUIAJE MIMBA KUTOKA?
Mimba nyingi zinazotoka husababishwa na genetics ama mambo ya kiafya ambayo si rahisi kuzuilika. Hivyo kwa mimba hizi ni ngumu sana kuzuia kutoka kwake. Hata hivypo kitu ambacho unaweza kukifanya ni kuhakikisha kuwa unabakia katika afya salama kabla na baada ya kubeba ujauzito. Fafya mabo yafuatayo yatasaidia katika kuboresha afya yako na kuzuia kiutoka kwa ujauzito:-
A.Kula mlo kamili wenye virutubisho (balanced diet)
B.Fanya mazoezi mara kwa mara. Si lazima eti mazoezi ya kukutoa mijasho, unaweza kufanya mazoezi ya viungo pia hata ukiwa kitandani.
C.Wacha ama punguza kutumia pombe, sigara ama dawa za kulevya.
D.Punguza unywaji wa chai kama unakunywa kwa wingi kupitiliza. Hapa ninazungumzia chai ya majani ya chai ambayo ina caffein.
E.Fanya uchunguzi wa afya yako mara kwa mara.
F.Wacha kutumia dawa kiholela
G.Jiepushe na mambo ambayo yataweza kuwa ni hatari kwa ujauzito kama kupigana ama miereka.
H.Fuata maelekezo vyema kutoka kwa wahudumu wa afya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango, sio kwa imani potofu ambazo Watu utumia kuelezea uzazi wa mpango.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa uzazi wa mpango kwa watoto, sio akina Mama peke yao wanaofaidika na uzazi wa mpango vile vile na watoto wanafaidika na uzazi wa mpango kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Kutoka na majimaji ka uchache kwa mwanamke sio jambo lakishangaa sana. Damu hii inawezapiabkikbatana damu na maumivu makali.
Soma Zaidi...Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi na uvimbe katika mirija ya uzazi. Mara nyingi hutumiwa sawa na ugonjwa wa uvimbe kwenye fupa nyonga (PID), ingawa PID haina ufafanuzi sahihi na inaweza kurejelea magonjwa kadhaa ya njia ya juu ya uzazi
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni. Ni maji ambayo kwa kitaalamu huitwa (Amniotic fluid)
Soma Zaidi...Unaweza kupitiliza siku zako za hedhi kwa sababu nyingi. Post hii itakueleza ni kwa nini umechelewa kupata siku zako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kumpeleka mtoto kliniki, kliniki nisehemu ambayo mtoto hupelekwa Ili kujua maendeleo ya mtoto akiwa chini ya umri wa miaka mitano
Soma Zaidi...Nini humaanisha kama chuchu zinauma na hupati period mwanaidi mrefu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku ya 7 Hadi ya 14
Soma Zaidi...