Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye tumbo la uzazi la Mama pindi anapobeba mimba, ni mabadiliko yanayotokea kwa mwanamke anapobeba mimba kama ifuatavyo.
Mabadiliko kwenye Tumbo la Mama anapobeba mimba.
1.Mama anapobeba tu mimba tumbo la uzazi linakomaa na kuwa na mazingira ya kumpatia mtoto chakula na mazingira kwa ajili ya kukua kwa mtoto, hii utokea pale ambapo mimba ukomaliza kutungwa tu tumbo la uzazi uandaliwa kwa ajili ya kutunza mimba iliyotungwa na namna ya kulisha mimba iliyotungwa kwa miezi Tisa mpaka pale mtoto anapozaliwa.
2.Baada ya Mimba iliyotungwa kutoka kwenye milija ambapo mimba utungiwa kwa kitaalamu huitwa follapian tube mimba ushuka mpaka kwenye tumbo la uzazi hapo placenta utengenezwa na kumalizika kwa mda wa wiki Kumi, na kazi za hiyo placenta ni kusafilisha hewa Safi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kusafirisha chakula kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, hewa chafu kutoka kwa mtoto kwenda kwa Mama na pia kuzuia sumu kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.
3.Sehemu ya ndani ya tumbo la uzazi ambayo kwa kitaalamu huitwa myometrium kwa kusaidia a na homoni ambayo huitwa ostrogen usaidia kukomaa kwa misuli ambayo IPO ndani ya tumbo, hiyo misuli ukua na kukomaa kwa ajili ya kutunza mtoto.
4. Kiwango Cha uzito wa tumbo la uzazi uongezeka kutoka kwenye hali ya kawaida ambayo ni 60gm kama mwanamke Hana mimba mpaka 1000gm ikiwa mwanamke ana mimba, kwa hiyo hiki ni kiwango kikubwa kutoka 60gm mpaka 1000gm kwa hiyo sehemu ya tumbo la uzazi inabidi kuandaliwa vizuri Ili kuweza kumtunza vyema mtoto.
5. Size ya mlango wa kizazi nayo ubadilika kutoka kwenye hali ya kawaida ambayo ni 7.5 mara 5 mara 2.5 mpaka 30 mara 22.5 mara 20 in cm. Tunaona size kabla mama hajabeba mimba ni tofauti kabisa na baada ya kubeba mimba kwa hiyo Mama anapaswa kuangaliwa kwa namna ya pekee kwa sababu ya Mzigo Mzito aliubeba.
6. Na pia kwenye mlango wa uzazi mishipa ya damu unaongezeka Ili iweze kusambaza damu vizuri kwa Mama na mtoto na pia kuweza kufanya kazi ya placenta vizuri Ili damu kwa mtoto na Mama iweze kutosha kwa kiwango kinachohitajika kwa hiyo Mama akiwa na Mimba mishipa ya damu uongezeka kwa namba na idadi Ili kusambaa kwa damu ya kutosha kwa Mama na Mtoto.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi njia za kutibu kuharisha kwa watoto wakiwa nyumbani, kwa sababu mara nyingine mtoto anaweza kuharisha si kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi ila ni uchafu tu kwa hiyo njia muhimu zinazofaa kutibu mtoto ni pamoja na yafuatayo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia kwa mtoto pindi anapozaliwa,tunajua wazi kuwa mtoto anapoanza kutokeza kichwa tu ndio mwanzo wa kuanza kumtunza mtoto na kuhakikisha anafanyiwa huduma zote za muhimu na zinazohitajika.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maelekezo muhimu kwa mama au mlezi wa mtoto mgonjwa. Ni maelekezo muhimu hasa wakati wa kutoa dawa kwa mtoto.
Soma Zaidi...Kuzaa kabla ya wakati ni kuzaliwa ambayo hufanyika zaidi ya wiki tatu kabla ya kuzaliwa kwa mtoto au kuzaliwa mapema ni moja ambayo hutokea kabla ya mwanzo wa wiki ya 37 ya ujauzito. Kawaida, ujauzito hudumu kama wiki 40.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mathara yanayosababisha Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo chini ya umri wa miaka mitano ili kuweza kuweka afya yake kwenye njia safi.
Soma Zaidi...Ni vyakula gani anapasa kula mjamzito, na utaratibu mzima wa lishe kwa wajawazito
Soma Zaidi...Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii
Soma Zaidi...