Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kutoka kwa mimba na dalili zake
KUTOKA KWA UJAUZITO, DALILI ZAKE NA SABABU ZAKE.Kutoka kwa ujauzito mara nyimgi hutokea katika hiki kipindi cha kwanza yaani ndani ya wiki 12 za mwanzo. Inakadiriwa kuwa robo ya mimba zinazotoka basi hutoka katika kipindi hiki. Mwanamke anaweza akatokwa na mimba kwa kujuwa ana bila ya kujuwa. Inaweza kutokea pia mwanamke akabeba ujauzito na ukatoka bila kuwa na habari yeyote kama alikuwa na miba na imetoka. Ni kuwa mimba inaweza kutoka bila ya kuwa na dalili za wazi kama kutoka na damu.
Dalili za kutoka kwa mimba:A.Maumivu ya mgongoB.KuharishaC.KichefuchefuD.Maumivu ya maeneo ya nyonga na kiuno kama unahisi unataka kuingia kwenye siku zakoE.Maumivu makali ya tumboF.Kutokwa na majimaji kwenye uke.G.Kutokwa na vitu kama vijioande vya nyama vijidogo kwenye ukeH.Uchovu mkali sana usio na sababuI.Kupotea kwa dalili nyingine za ujauzitoJ.Kutokwa na damu mabonge manonge ama damu nyingi
Kumbuka hizi ni dalili tu, unaweza kuwa nazo na ujauzito ukawa salama kabisa. Ukiona unahisi dalili hizo muone daktari atathibitisha vyema kwa vipimo ikiwemo utrasound ama kuangalia kiwango cha homoni ya ujjauzito kwneye damu yako.
Ni zipi sababu za kutoka kwa mimba?Mara nyingi kutoka kwa ujauzito kunaweza kusababishwa na chromosomal abnormalities. Hili ni tatizo la kigenetics. Hapa seli za mtoto zinashindwa kugawanyika vyema na kukuza mtoto. Sababu nyingine za kutoka ujauzito ni:-A.Matatizo katika homoni kuwa nyingi sana ama kidogo sanaB.Kama mama mjamzito ana kisukari na hafuati masharti vyemaC.Mazingira yanaweza kuchangia kama kuna mionzi hatari kama ya madini ya uraniumD.Maambukizi na mashambulizi ya vijidudu kama bakteria kwenye via vya uzazi.E.Shida katika mlango wa uzazi (cevix)F.Kutumia madawa kiholela ama kutumia madawa kusudi kwa lengo la kutoa ujauzitoG.Ugonjwa wa endometriosis (kuvimba kwa kuta za mji wa mimba “uterus”)H.Magonjwa ya ngono kama gonoria
Sababu nyingine za kutoka kwa mimbaA.Utapia mloB.Kuwa na kitambiC.Matumizi ya vilevi na sigaraD.Maradhi ya tezi ya thyroidE.Shinikizo la damu la juu sana
NITAZUIAJE MIMBA KUTOKA?Mimba nyingi zinazotoka husababishwa na genetics ama mambo ya kiafya ambayo si rahisi kuzuilika. Hivyo kwa mimba hizi ni ngumu sana kuzuia kutoka kwake. Hata hivypo kitu ambacho unaweza kukifanya ni kuhakikisha kuwa unabakia katika afya salama kabla na baada ya kubeba ujauzito. Fafya mabo yafuatayo yatasaidia katika kuboresha afya yako na kuzuia kiutoka kwa ujauzito:-
A.Kula mlo kamili wenye virutubisho (balanced diet)B.Fanya mazoezi mara kwa mara. Si lazima eti mazoezi ya kukutoa mijasho, unaweza kufanya mazoezi ya viungo pia hata ukiwa kitandani.C.Wacha ama punguza kutumia pombe, sigara ama dawa za kulevya.D.Punguza unywaji wa chai kama unakunywa kwa wingi kupitiliza. Hapa ninazungumzia chai ya majani ya chai ambayo ina caffein.E.Fanya uchunguzi wa afya yako mara kwa mara.F.Wacha kutumia dawa kiholelaG.Jiepushe na mambo ambayo yataweza kuwa ni hatari kwa ujauzito kama kupigana ama miereka.H.Fuata maelekezo vyema kutoka kwa wahudumu wa afya.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Kutokwa Majimaji sehemu za siri kwa mwanamke sio jambo la kushangaza na kuhisivunaumwa. Majimajivhaya ndio huboresha afya ya uzazi kwa kusafisha na kulinda via vya uzazi. Lakini majimajivhaya yakiwa mengi, ama yanawasha ama yanaharufu haa ndipo kwenye tat
Soma Zaidi... Posti hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa ovari kunakosababishwa na maambukizo ya bakteria na kawaida huweza kusababishwa na magonjwa sugu katika Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya testosterone, hii homoni kwa kiwango kikubwa ukutwa kwa wanaume ndiyo homoni ambayo umfanya mwanaume aonekane jinsi alivyokuwa na sifa zake zote.
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukupa dalili ambazo zinaonyesha kuwa mimba ni ya mapacha. Dalili hizi zitahitajika kuthibitishwa na kipimo cha daktari ili kujuwa kuwa ni kweli.
Soma Zaidi...Ujauzito husababisha mabadiliko mengi mwilini, ikiwepo ongezeko la Majimaji ukeni ifikapo tarehe za kukaribia kujifunguwa. Majimaji haya ni muhimu kwa afya ya mtoto aliye tumboni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa wale wenye tabia ya kutoa mimba mara Kwa mara .
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kutibu tatizo la ugumba kwa Mwanaume, ni njia ambazo utumiwa na wataalam mbalimbali Ili kuweza kutibu tatizo la ugumba kwa wanaume.
Soma Zaidi...Vyakula hivi hapasi kuvila mwanamke mwenye ujauzito kwa kiasi kikubwa, hasa yule mwenye mimba chaga
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi, tunajua kabisa wakati wa hedhi damu inapaswa kuwa nyepesi na ya kawaida ila kuna wakati mwingine inakuwa na mabonge zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi.
Soma Zaidi...