Yanayotengua Udhu
Mtu aliyetawadha hutokwa na udhu wake kwa kupatwa au kutokewa na mojawapo kati ya haya yafuatayo:
1.Kutokwa na kitu chochote kwenye sehemu za siri. Ni pamoja na kwenda haja ndogo au kubwa. Kutokwa na upepo, maji maji yatokayo katika utupu wa mbele kutokana na matamanio au sababu nyinginezo.
2.Kutokwa na fahamu kwa kulala usingizi kwa kuegemea mahali bila ya kumakinisha makalio yake ardhini. Tunajifunza katika hadithi ifu atayo:
Amesimulia Basrah (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) kasema:Kutawadha kuna kuwa lazima kwa mwenye kulala usingizi kitandani, kwa sababu anapolala kitandani maungo yake hulegea ”.(Tirmidh, Abuu Daud).
3.Kushika sehemu za siri kwa viganja vya mikono kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:
Amesimulia Basrah (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) kasema: “Mmoja wenu atakapogusa tupu yake, na aende kutaw adha tena ”.(Malik, Ahm ad, Abuu Daud, Tirmidh, Nasai, Ibn Majah)
Haya matatu ndio yanayotengua udhu bila ya khitilafu yoyote kati ya Waislamu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu,aina za swala (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم "لَا يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ [ يشهد أن ل?...
Soma Zaidi...- Ni taasisi za kifedha zinazohusika na kuhifadhi akiba na mali za watu zenye thamani kubwa kama dhahabu, n.
Soma Zaidi...Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma.
Soma Zaidi...