Home Afya Shule ICT Burudani Dini Maktaba Maswali Madrasa Apps Blog Legacy Login

LENGO LA HIJJAH NA MATENDO YA IBADA YA HIJJAH NA MAFUNZO YATOKANAYO


image


Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)


 

Lengo la Hijjah.

Kuwa askari Mcha-Mungu aliyekuwa tayari kutumia mali na nafsi yake katika kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kutawala maisha ya jamii.

Rejea Quran (48:18) na (3:96-97).

 

 

Matendo ya ibada ya Hijjah na Mafunzo yatokanayo.

Kabla na wakati wa kutekeleza ibada ya Hijjah, kuna mafunzo na hatua za kuzingatia kama ifuatavyo;

 

Maandalizi na Safari ya Hijjah.

Ni lazima muislamu kabla ya kwenda Hijjah afanye maandalizi ikiwa ni pamoja na kuzidisha ucha-Mungu, kuandaa gharama, mahitaji, n.k.

Rejea Quran (2:197)

 

Ihram.

Ni hali ya kuwa katika vazi rasmi na miiko kwa mwanaume mwenye Kuhiji au kufanya Umrah.

Funzo (49:13):

-  Vazi la Ihram linatufunza usawa baina ya wanaadamu wote.

 

Talbiya.

Ni kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kusema yafuatayo, “Labbayka Allahumma Labbayka. Labbayka laashariika laka labbayka. Innal-hamda Wanniimata laka wal-mulka, laashariika laka

 

Mafunzo (22:27) na (48:18):

Talbiya inatufunza kumuitikia Mwenyezi Mungu (s.w) kufuata maamrisho na kuacha makatazo yake.

-     Talbiya inatufunza umoja na usawa baina ya waislamu wote.

 

Tawaf.

Ni kitendo cha kuizunguka Kaaba mara saba kuanzia jiwe jeusi kwa mwelekeo wa kinyume na saa kwa kulibusu au kuligusa au kuashiria.

 

Mafunzo:

Kuchukua ahadi ya utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Kumtaja na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wingi.

Inatufunza umoja, udugu na usawa baina ya wanaadamu wote.

 

Sai.

Ni kitendo cha kutembea mara saba baina vilima viwili, Saffaa na Marwaa, kwa kuanzia Saffaa na kumalizia Marwaa.

 

Mafunzo:

Inatufunza utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

Inatufunza ushujaa na uhodari katika kupigania Uislamu.

Inatufunza kuwa tayari kuhangaika kwa ajili ya kupigania Uislam

 

Kupiga Kambi Mina, Mwezi 8 Dhul-Hijah.

Ni kitongoji kilichopo baina ya Mji wa Makkah na bonde la Arafah. Mahujaji hulala hapo na kuondoka kesho yake kuelekea Arafa asubuhi.

 

Mafunzo:

Huwafunza mahujaji kuwa askari waliotayari kuacha kila chaokwa ajili ya kupigania Uislamu.

Huwafunza mahujaji kuwa askari wanatiifu kwa Muumba wao.

 

Kusimama Arafah, Mwezi 9 Dhul-Hija.

Arafa ni bonde lililo baina ya vilima vitatu. Mahujaji husimama humo tangu Swala ya Adhuhuri hadi Magharibi na kuomba dua mbali mbali. 

 

Mafunzo:

Huwakumbusha mahujaji mkutano mkuu wa siku ya Kiama.

Hutufunza kuwa hakuna aliyebora ila amchae Mungu zaidi.

Kisimamo cha Arafa kinatufunza usawa baina ya wanaadamu.

 

Kupiga Kambi Mzidalfah.

Mzidalfa ni kitongoji kilicho baina ya Mina na Arafa. Mahujaji huswali Magharib na Isha hapo na kuelekea Mina mara tu baada ya swala Alfajir.

 

Mafunzo:

Huwafunza mahujaj kuwa askari waliojiandaa kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w).

Kuomba dua hutufunza kuwa ushindi ni kwa nusura ya Mungu tu.

 

Kutupa Mawe Mina katika Minara Mitatu, Mwezi 10, Dhul-Hija.

Ni kitendo kinachofanyika kuanzia Mwezi 10-13, Dhul-Hija kwa kutupa vijiwe saba kila Mnara.

 

Mafunzo:

-   Zoezi hili huwafunza mahujaj ujasiri wa kupambana na maadui zao.

-   Huwafunza mahujaj pia mbinu na silaha katika kupigana na maadui.

 

Kuchinja mnyama Mwezi 10, Dhul-Hija.

Katika siku hii Hajj atanyo nywele, kuchinja mnyama, kutupa mawe kwenye Minara mitatu na kutufu Tawaful-Ifaadha (tawafu ya nguzo).

 

Mafunzo:

-   Zoezi hili linawafunza mahujaj utiifu kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

-   Tunajifunza kuwa tayari kuua au kuuawa kwa ajili ya Mungu.

-   Inatufunza kuwa na subira na kujitoa muhanga katika kunusuru dini

Rejea Quran (22:37) na (37:111).

 

Siku za Tashriiq Mwezi 11-13, Dhul-Hija.

Ni kilele cha ibada ya Hija, ambapo mahujaj hupumzika kambini na kutathmini vitendo vyote walivyovifanya.

 

Mafunzo:

-   Huwafunza mahujaj kumkumbuka Mungu baada ya kazi ngumu.

-   Huwafunza askari kuwa na mazingatio na yale waliojifunza kwayo.

 

Tawaf ya Kuaga (Tawaful-Widaa).

Ni Tawafu ya kuaga baada ya ibada ya Hija kukamilika na kujiandaa kurejea nyumbani kwa mahujaji.

 

 

Mafunzo:

Huwafunza mahujaj kuwa viongozi (makhalifa) katika ardhi.

Kuwa askari waliochukua mafunzo tayari kwa kuyatekeleza.

Kuchukua ahadi ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu (s.w).



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 ICT       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    5 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS

Imeandikwa na Tags Dini , DARSA , ALL , Tarehe 2022/01/18/Tuesday - 07:22:01 pm     Share On facebook or WhatsApp Topic school Zaidi Dini AFYA ICT Burudani Tags Uzazi maswali Afya mengineyo dini HIV Sira vyakula Matunda HTML php Alif Lela 1 Alif Lela 2 FANGASI Dawa SQL Tips Quran Sunnah fiqh DARSA Magonjwa Tajwid tawhid simulizi Dua Academy Wahenga chemshabongo WAJUWA Michezo ICT Imesomwa mara 1869



Post Nyingine


image Sanda ya mtoto
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kutoa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Zoezi la 5
Maswali mbalimbali kuhusu fiqih Soma Zaidi...

image Suratul-takaathur (102) imeteremshwa makkah Ina aya nane
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Msimamo wa uislamu juu ya utumwa
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mambo yanayodhaniwa kuwa yanaharibu funga lakini hayaharibu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kwanini lengo la zakat na sadaqat halifikiwi katika jamii yetu
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Tofauti kati ya fiqh na sheria
Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria. Soma Zaidi...

image Hijja na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...