Kuandama kwa Mwezi na Kufunga ama kufungua ramadhani, sheria na hukumu za kuangalia mwezi

Kuandama kwa Mwezi na Kufunga ama kufungua ramadhani, sheria na hukumu za kuangalia mwezi

Kuonekana kwa mwezi wa RamadhaniSwaumu ya Ramadhani inaanza kwa kuona mwezi baada ya siku ya 29 Shaaban au 30 Shaaban kama tunavyofahamshwa katika hadithi zifu atazo:
'Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Msifunge mpaka muuone mwezi umeandama na msiache kufunga mpaka muone mwezi (wa Shawwal) umeandama. Kama kuna mawingu (hukuuona) hesabu kamili (siku 30). Katika simulizi nyingine amesema: Mwezi una masiku 29, kwa hiyo usifunge mpaka uone mwezi umeandama kama kuna mawingu subiri na kamilisha idadi ya siku 30.'
(Bukhari na Muslim)Kutokana na Hadithi hii ni wazi kuwa watu hawaruhusiwi kufunga kwa kufuata kalenda. Inabidi juhudi za kuuangalia mwezi ziwepo kwa umma wa Waislamu tangu mwanandamo wa Shaaban.'Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuw a Mtume w a Allah ameagiza: Hesabu mwandamo wa Shaaban kwa ajili ya Ramadhani'. (Tirmidh).Kwanini kufuata mwandamo wa mwezi?Tunafunga kwa kuona mwezi kwa sababu ndivyo alivyotuamrisha Mtume wa Allah (s.w) kama tulivyojifunza kutokana na hadithi zilizonukuliwa hapo juu. Kumtii Mtume (s.a.w) ndio Uislamu. Rejea Qur-an katika aya zifuatazo:


'Sema: 'Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkikengeuka (Allah atakuadhibuni) kwani Allah hawapendi makafiri.' (3:32)


' Na anachokuleteeni Mtume, kipokeeni, na anachowakataza
kiacheni' (59:7).


'Anayemtii Mtume, kwa yakini amemtii Mw enyezi Mungu' (4:80)


Pia amri hii ina hekima yake. Mwaka unaohesabiwa kwa mwandamo wa mwezi una siku 354 kwani kwa wastani mwezi mmoja una siku 29?. Mwaka unaohesabiwa kwa kufuata jua, muda ambao dunia huchukua kulizunguka jua una siku 365, saa 5, dakika 48 na nukta 46. Kwa hiyo ukilinganisha mwaka wa hesabu ya mwezi na mwaka wa hesabu ya jua, utaona kuwa mwaka wa mwezi ni mfupi kwa siku10 hivi. Hivyo mwezi wa Ramadhani hurudi nyuma siku kumi katika kila mwaka ukilinganisha na mwaka wa jua. Hivyo basi, mtu yeyote atakayejaaliwa kufunga muda wa miaka 36 hatakuwa na siku au msimu katika mwaka ambao hakuufunga. Yaani atawahi kufunga siku zote za jua, za mvua, za upepo, za shwari, za kusi, za kaskazi na kadhalika. Kama ingelikuwa inafuatwa kalenda ya mwaka wa jua, wengine daima wangalifunga nyakati za joto tu, wengine nyakati za baridi tu, wengine nyakati za njaa tu, wengine nyakati za mavuno na kadhalika ilimuradi pasingalikuwa na mabadiliko.


Ni lazima kila mfungaji aone mwezi?Mwezi wa Ramadhani akiona mtu mmoja muadilifu inatosha na wengine waliobaki itawabidi wafunge. Hivi ndivyo alivyoamrisha Mtume (s.a.w) kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:'Ibn Abbas (r.a) ameeleza kuwa Mwarabu wa Jangwani alikuja kwa Mtume (s.a.w) akasema: Hakika nimeuona mwezi wa Ramadhani umeandama. Mtume (s.a.w) akamuuliza: Unashuhudia kuw a hapana Mola ila Allah? 'Ndio' alijibu. Akamuuliza tena: Unashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume w a Allah? Akajibu 'Ndio '. Akasema (Mtume): Ee Bilal! Watangazie w atu kuw a haw ana budi kufunga kesho'. (Abu Daud, Tirm idh, Nisa i, Ibn Majah).'Ibn Omar (r.a) ameeleza: Watu waliuona mwezi. Kisha nikamfahamisha Mtume (s.a.w): Hakika nimeuona. Kwa hiyo alifunga na aliwaamrisha watu wafunge'. (Abu Daud, Darimi).


                   
Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 448


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

maana na asili ya dini, kazi zake na nadharia potofu za makafiri kuhusu dini
2. Soma Zaidi...

NDANI YA JUMBA LA ALADINI
Soma Zaidi...

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI
Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUUMBWA KWA NABII ADAMU (A.S)NA HADHI YAKE NA HADHI YA WANAADAMU DUNIANI
Adam(a. Soma Zaidi...

NAMNA AMBAZO DUA HUJIBIWA
NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA. Soma Zaidi...

Zaka katika mapambo, mali ya biashara na mali iliyofukuliwa ardhini
Soma Zaidi...

mtazamo wa uislamu juu ya dini
Soma Zaidi...

ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...

Uovu wa kumzulia Muumini Uzinifu na Maovu mengine na Hukumu dhidi ya Wazuaji
Kumzulia mtu mtwahirifu kuwa amefanya tendo la zinaa pasina kuleta ushahidi stahiki ni tendo ovu mno mbele ya Allah (s. Soma Zaidi...

DUA 51 - 60
51. Soma Zaidi...

Nadharia ya uchumi kiislamu
1. Soma Zaidi...

Twahara na namna ya kujitwaharisha, nguzo zake na sunna zake
Soma Zaidi...