Mambo gani ni Haramu kwa mwenye janaba?

Mambo gani ni Haramu kwa mwenye janaba?

Hadathi ya kati na kati (Janaba).

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Mambo gani ni Haramu kwa mwenye janaba?

Hadathi ya kati na kati (Janaba).



Mtu hupatwa na hadathi ya kati na kati kwa kupatwa na Janaba. Janaba ni hali inayompata mtu baada ya kufanya kitendo cha jimai (kitendo cha ndoa) au kutokwa na manii kwa kuota au kwa namna nyingineyo. Mtu mwenye janaba yuko katika hali chafu kulingana na sharia ya Allah (s.w) na ameharamishiwa kufanya ibada hizi:



(i)Kuswali (rejea Qur-an 4:43, 5:6)
(ii)Kutufu.
(iii)Kukaa Msikitini.



β€œAysha (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Msielekeze milango ya nyumba hizi msikitini kwa sababu si halali msikiti kwa mwanamke mwenye hedhi au kwa mtu mwenye janaba ”. (Abu Daud)


(iv) Ku is oma Qur-an hata kwa moyo.
Ibn Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: β€œWenye hedhi na wenye janaba hawatasoma chochote kutoka kwenye Qur-an ” (Tirmidh)



Si vibaya kwa mtu mwenye janaba kula, kuongea au kugusana na watu. Pia kutokana na mafundisho ya Mtume (s.a.w) si lazima mtu kukoga mara tu baada ya kufanya kitendo cha jimai na mkewe, hasa ikiwa usiku bali anatakiwa aoshe sehemu za siri na atawadhe alale, kisha akiamka ndipo akoge kwa kujitwaharisha kwa ajili ya swala ya Alfajiri. Mafundisho haya tunayapata katika hadithi ifuatayo:



Aysha (r.a) ameeleza kuwa: Mtume (s.a.w) alipotaka kula au kulala akiwa na janaba, alikuwa kwanza akitawadha kama anavyotawadha kwa ajili ya swala. (Bukhari na Muslim).




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1862

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

MARADHI MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA MBU ( matende, ngirimaji, homa ya manjano, n.k
MARADHI MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA MBU ( matende, ngirimaji, homa ya manjano, n.k

Tofauti na maradhi yaliyotajwa hapo juu pia tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwepo kwa maradhi mengine hatari yanayosambazwa na mbu, kama vile ngirimaji pamoja na matende.

Soma Zaidi...
Haki za viumbe na mazingira
Haki za viumbe na mazingira

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Sifa nyingine za kuchaguwa mchumba ambazo watu wengi hawazijui
Sifa nyingine za kuchaguwa mchumba ambazo watu wengi hawazijui

Hizi ni sifa za ziada za mchumba katika uislamu. Sifa hizi wengi hawazijui ama hawazingatii.

Soma Zaidi...
Swala ya jamaa na taratibu zake
Swala ya jamaa na taratibu zake

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya jamaa na taratibu zake.

Soma Zaidi...
Nini maana ya twahara katika uislamu
Nini maana ya twahara katika uislamu

Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya twahara katika uislamu. Pia utakwenda kujifunza hukumu za twahara, aina za twahara na mambo mengineyo

Soma Zaidi...