11.
11. Kusoma Tahiyyatu
Kusoma tahiyyatu ni nguzo ya swala. “Tahiyyatu” ina maana ya “Maamkizi”, ukiwa umekaa kikao cha tahiyyatu unaleta maamkizi kama ifuatavyo: “Attahiyyaatu lillaah, wasw-swalawaatu, watwa-yyibaatu, assalaamu ‘alaika ayyuhannabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuhu, assalaamu ‘alay-naa wa-’alaa ‘ibaadillaahi swswaalihiina. Ash-hadu an-llaailaaha illallaahu wa-ash-hadu anna Muhammadan ‘abduhuu warasuuluhu”. “Maamkizi yote ni ya Allah, na swala zote na yote mazuri, Amani iwe juu yako, ewe Mtume na Rehma na Baraka za Allah. Na amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah. Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mja na, ni Mtume wake”. (Muslim).
12. Kumswalia Mtume (s.a.w).
Kumswalia Mtume (s.a.w) ni nguzo ya swala inayofuatia baada ya kusoma Tahiyyatu. Kumswalia Mtume si faradhi katika swala tu bali pia ni faradhi kumswalia kila anapotajwa kwa jina lake. Msisitizo wa amri ya kumswalia Mtume unaonekana katika aya ifuatayo:
“Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume; na Malaika wake (wanamuombea dua). Basi; enyi Mlioamini msalieni (Mtume, muombeeni Rehema) na amani”. (33:56)
Pia hadithi zifuatazo zinasisitiza umuhimu wa kumswalia Mtume (s.a.w) kila atajwapo na kila mtu apatapo wasaa. Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Bakhili ni yule anayesikia nikitajwa, lakini haniswalii. (hanitakii rehma). (Tirmidh).
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Anayenitakia Rehma (anayeniswalia) mara moja, Allah humrehemu mara kumi”. (Muslim).
“Ibn Mas’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakayekuwa kipenzi changu katika watu, katika siku ya Kiama atakuwa ni yule aliye mbele kuliko wote katika kunitakia Rehma (kuniswalia). (Tirmidh).
Namna ya kumswalia Mtume (s.a.w) imeelezwa katika Hadithi nyingi lakini iliyomashuhuri katika hizo ni ile iliyosimuliwa na Abdur- Rahman bin Ubaidillah(r.a) na kupokelewa na Maimamu wote wa Hadithi kuwa Mtume (s,.a.w) ametufundisha tumswalie (tumtakie Rehma) kama ifuatavyo;
“Allahumma swalli ‘alaa muhammad wa’alaa aliy Muhammad kamaa swallaita ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik ‘alaa muhammad wa’alaa ali muhammad kamaa barakta ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahima innaka hamiidum-majid”
Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha maana ya kusimamisha swala kama inavyotumika kisheria.
Soma Zaidi...Swala iliyosimamishwa vilivyo ndiyo nyenzo kuu ya kumtakasa Muislamu na kumpa sifa zinazomuwezesha kustahiki kufanya kazi takatifu ya kusimamisha Uislamu katika jamii.
Soma Zaidi...Haya ni maandalizi anayofanyiwa mtu aliye katika kilevi cha kifo yaani sakaratul maut
Soma Zaidi...