Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?

Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?

Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Mgogoro wa kuandama kwa mwezi, Je mwezi wa Kimataifa ama kila Mji na mwezi wake?

Mwezi ukionekana sehemu moja, Waislamu wote ulimwenguni watalazimika kufunga?



Waislamu wote wanakubaliana kutokana na hadithi tulizozinukuu hapo juu, kuwa mtu mmoja au watu wachache wakishuhudia kuandama mwezi wa Ramadhani, Waislamu watalazimika kufunga. Pia waislamu wote wanakubaliana kuwa watu wa wili au zaidi wakishuhudia kuandama kwa mwezi wa Shawwal, Waislamu watalazimika kufuturu na kuswali Id dil-Fitr.



Hitilafu kati ya Waislamu juu ya swala la watu wachache kushuhudia kuandama mwezi wa Ramadhani au wa Shawwal ipo kwenye umbali, kwamba ni watu wa wapi wafunge watakaposikia habari za kuandama mwezi kutoka wapi? Juu ya suala hili Waislamu wamegawanyika katika makundi mawili yafu atayo:



Kundi la kwanza ni la wale wanaosema kuwa mwezi ukionekana katika mji mmoja au sehemu moja, basi Waislamu wengine popote walipo ulimwenguni watalazimika kufunga au kufungua. Haya pia ni maoni ya Imamu Hambali, Malik na Abu Hanifa. Hawa wamejiegemeza katika hadithi tulizozinukuu hapo juu.



Kundi la pili ni la wale wanaojiegemeza katika Hadithi ifuatayo: Kurayb (r.a) ameeleza kuwa Umm Fadhl, binti wa Harith alimtuma (mtoto wake) Fadhl Syria (Sham) kwa Muawiya. Fadhl aliwasili Syria na akatekeleza yale aliyotumwa na mama yake. Alipokuwa pale Syria mwezi wa Ramadhani ulianza. (Amesema Fadhl): Niliuona mwezi wa Ramadhani ulipoandama siku ya Ijumaa. Kisha nilirudi Madina mwishoni mwa mwezi. β€œAbdullah bin Abbas (r.a) aliniuliza juu ya kuandama kwa mwezi wa Ramadhani na akasema: Mliuona lini? Nikajibu: Tuliuona usiku wa Ijumaa. Akaniuliza; Uliona wewe mwenyewe? Nikajibu; Ndio na watu pia waliuona na walifunga na Muawiya pia alifunga, ndipo akasema; lakini sisi tuliuona usiku wa Jumamosi. Kwa hiyo tutaendelea kufunga mpaka tukamilishe 30 au tuuone mwezi Shawwal baada ya 29 Ramadhani) Nikauliza; (Fadhili): kuonekana kwa Mwezi wa Muawiya hakukutosha? Akajibu; Hapana hivi ndivyo Mtume wa Allah (s.w) alivyotuamrisha ”. (Muslim).



Kutokana na hadithi hii kama kuna masafa marefu kati ya mji ulipoonekana mwezi na mji watu walipopata taarifa juu ya kuonekana kwake haitajuzu kwao kufuata mwandamo huo, lakini endapo mji huo utakuwa umekaribiana basi watu waliopata taarifa ya kuandama mwezi kutoka mji wa karibu watawajibika kufunga au kufungua, mwanachuoni mashuhuri anayeshikilia rai hii ni Imamu Shafii.



Kutokana na hitilafu hizi, imetokea kuwa waislamu wote ulimwenguni hawaanzi kufunga Ramadhani siku moja na kuswali Iddil-Fitr na Iddil Hajj siku moja. Wale wanaoshikilia raia ya kwanza, wanaona kuwa si vyema umma mmoja wa Kiislamu kutofautiana katika matukio haya muhimu ambayo ni alama ya dini. Isitoshe kutokana na maendeleo ya sayansi, mawasiliano ulimwenguni hivi leo yamerahisika mno. Ulimwengu mzima unaweza kupata habari kwa muda wa dakika chache juu ya mwandamo wa mwezi katika mji mmoja.



Wale wanaoshikilia rai ya pili wanaoona kuwa si vyema kufunga au kufungua Ramadhani kwa kufuata habari ya kuandama kwa mwezi kutoka popote pale bila ya kujali masafa au machweo (matlai) kati ya mji huo na pale habari ya kuandamana mwezi ilipopokelewa. Kwani kijiografia sehemu mbali mbali za ulimwengu zinatofautiana sana. Kutokana na uchunguzi wa anga umepatikana ushahidi kuwa kuna kutofautiana katika kuona mwezi ambako katika mji mmoja kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kuona mwezi endapo hapatakuwa na mawingu, katika mji mwingine ulio masafa ya mbali na matlai mengine, mwezi hauandami kabisa siku hiyo hata kama hapata kuwa na mawingu. Kwa hiyo hawa wenye mtazamo wa pili, pia kutokana na maendeleo hayo hayo ya kisayansi, wanaona kuwa hadithi zilizowaamrisha watu kufunga au kufungua kwa kupata habari ya kuandama mwezi kutoka kwa mtu mmoja au watu wachache, hazionyeshi kuwa wale walioleta habari za kuandama mwezi walitoka masafa marefu na pale alipokuwa Mtume (s.a.w).



Kutokana na rai hizi mbili, ni vema Waislamu wasigombane kwa jambo hili. Kila mtu ana uhuru wa kufuata hoja iliyomtua zaidi. Hata hivyo, lingelikuwa jambo zuri kama wanachuoni wa kila jimbo lenye uhusiano mwema kama vile Afrika ya Mashariki, wangelijadiliana na kukubaliana juu ya msimamo mmoja.




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 3389

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰2 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Zijuwe funga za kafara na jinsi ya kuzigunga
Zijuwe funga za kafara na jinsi ya kuzigunga

Post hii itakufundisha kuhusu funga za kafara, zinavyotokea na na jinsi ya kuzifunga.

Soma Zaidi...
Umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu
Umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu

Nguzo za uislamu,umuhimu na msisitizowa zakat na sadaqat katika uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Dhana ya kumiliki raslimali katika uislamu
Dhana ya kumiliki raslimali katika uislamu

Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu.

Soma Zaidi...
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kujenga uchumi wa kiislamu

Nazingatio muhimu katika uchumi unaofuata sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...
Mifumo ya benki ya kiislamu.
Mifumo ya benki ya kiislamu.

Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha

Soma Zaidi...
Aina mbili za talaka zisizo na rejea katika uislamu
Aina mbili za talaka zisizo na rejea katika uislamu

Huwezi kuruhusiwa kumrejea mke endapo utamuacha kwa talaka hizi mbili.

Soma Zaidi...