Mifumo ya benki ya kiislamu.

Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha

Benki za Kiislamu
Benki za Kiislamu ambazo hutoa huduma kama benki nyingine zinaendeshwa katika msingi wa biashara na sio ule wa riba. Benki za Kiislamu badala ya kukopesha kwa riba, hutumia rasilimali zake kwa zenyewe kujihusisha katika uzalishaji kwa kufuata misingi inayokubalika katika Uislamu. Miongoni mwa misingi inayokubalika kwa Muislamu au Benki ya Kiislamu kuingiza fedha zake katika miradi ya biashara au uzalishaji ni hii ifuatayo:

 

(i)Mudharabah
Mudharabah ni makubaliano kati ya watu wawili au zaidi ambapo mmoja au zaidi kati ya hao anatoa mtaji na mwingine hushiriki kwa ukamilifu katika kuendesha na kuongoza mradi wa uchumi. Faida itakayopatikana katika mradi huo itagawanywa kulingana na makubaliano yao. Hasara itakayotokana na mradi huo itakuwa ni ya mwenye kutoa mtaji. Wengine hawatoi chochote kusaidia hasara kwa sababu wameshatoa mchango wao wa hasara hiyo kwa jasho walilolitoa katika shughuli ambayo haikuzaa matunda bali hasara.

 


Benki za Kiislamu zinaingiza fedha zake katika miradi ya uchumi kwa njia hii ya Mudharabah ambapo benki hutoa mtaji kwa ajili ya miradi mbali mbali ya uchumi kwa mapatano ya kupata kiasi (asilimia) fulani cha faida itakayopatikana na kuwa tayari kulipa hasara itakayopatikan a.

 

(ii)Musharikah
Musharikah ni ushiriki kati ya watu wawili ambapo, tofauti na Mudharabah wote wawili wanachangia mtaji na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli ya kiuchumi, lakini si lazima watoe hisa sawa sawa, kwa makubaliano ya kugawana faida na hasara kulingana na kiasi cha hisa alichotoa kila mmoja wao. Kwa mtindo huu wa “Musharikah” Benki ya Kiislamu inaingia katika kuchangia mtaji, kuendesha na kusimamia mradi wa uchumi na watagawana (faida au hasara) kulingana na kiasi cha mtaji kila mmoja alichotoa.

 


(iii)Ijara-Uara wa Iktina
Huu ni utaratibu mwingine unaokubalika kisheria ambapo mtu au benki inatumia fedha zake katika kukodi vitu kama vile magari, majumba, ardhi, na kadhalika, ambavyo vikifanyiwa kazi huzalisha mali na kutoa faida. Benki za Kiislamu hujipatia faida kubwa kutokana na mtindo huu.

 


(iv)Murabah
Huu ni utaratibu unaotumiwa katika kununua bidhaa kwa wingi kwa ajili ya kuwauzia wafanya biashara ambao waliofikiana kuwa bidhaa hizo zinunuliwe kwa ajili yao. Benki kutokana na uwezo wake inapanga na wafanya biashara kuwa inunue bidhaa nyingi kutoka ndani na nje ya nchi kwa jina lake kisha iwauzie wafanyabiashara hao kwa bei itakayoipatia benki faida. Pia benki kwa mtindo huu inaweza kununua mazao ya wakulima na kuyauza kwa walaji kwa faida.

 


(v)Muqaradha
Mtindo huu wa Muqaradha humruhusu mtu au benki kununua “share” au “bonds” katika kampuni ya uzalishaji kwa mapatano ya kugawana faida au hasara kulingana na kiasi cha “share”.

 

Kwa kufuata mitindo hii katika kuingiza fedha zake katika miradi ya uchumi, Benki za Kiislamu hupata faida kubwa hata zaidi ya kipato cha riba kinachopatikana katika benki za riba. Benki za Kiislamu nazo hugawa faida inayopatikana kwa wateja wake walioweka fedha zao kwenye benki.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1409

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Haki za raia katika dola ya kiislamu

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Lengo la kusimamisha swala

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Yaliyoharamishwa kwa mwenye kuwa katika ihram

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango

Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzaziKama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi.

Soma Zaidi...
maana ya Eda na aina zake

Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.

Soma Zaidi...
Watu hawa huruhusiwi kuwaoa katika uislamu

Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa.

Soma Zaidi...
Kuzika-namna ya kuzika hatua kwa hatua

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...