Swala ya ijumaa, nguzo zake na suna zae, namna ya kuswali swala ya ijumaa

Swala ya ijumaa, nguzo zake na suna zae, namna ya kuswali swala ya ijumaa

Swala ya ijumaa, nguzo zake na suna zae, namna ya kuswali swala ya ijumaa

Swala ya Ijumaa



Swala ya Ijumaa ni faradh inayosimamishwa siku ya Ijumaa badala ya swala ya Adhuhuri. Swala ya Ijumaa imefaradhishwa kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya swala siku ya Ijumaa nendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora
kwenu ikiwa mnajua. Na itakapokwisha swala tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mw enyezi Mungu na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufaulu.(62:9 -1 0)



Pia faradhi ya Ijumaa inasisitizwa katika hadithi ifuatayo:


Ibn Umar, (r.a) na Abu Hurairah (r.a) wamesikiwa wakisema: “Tumemsikia Mtume wa Allah akisema akiwa ulingoni (jukwaani): Watu wajiepushe na kutohudhuria swala ya Ijumaa, la sivyo Allah (s.w) atawapiga muhuri nyoyo zao, na kisha wakawa miongoni mwa wasioonyeka na wasiomkumbuka tena Allah (s.w). (Muslim).



Wanaolazimika Kuswali Swala ya Ijumaa



Wanaolazimika kuswali swala ya Ijumaa ni Waislamu wanaume waliomukalafu kama tunavyojifunza katika Hadithi ifu atayo:
Twaariqi bin Shihaabi (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Ijumaa ni faradhi kwa kila Mu is lamu kwa kuiswali jamaa ila si faradhi kwa watu wanne” Watumwa (wafungwa), wanawake, watoto na wagonjwa ”.(Abu Daud).



Kutokana na Hadithi hii tunajifunza kuwa swala ya Ijumaa ambayo ni lazima iswaliwe kwa jamaa ni faradhi kwa kila Muislamu mwanamume aliye balegh, muungwana na aliye mzima wa afya. Pia tunajifunza kuwa wanaoruhusiwa kuto swali swala ya Ijumaa ni hawa wafuatayo:



1. Wanawake.
2. Watoto wadogo.
3. Vikongwe na vilema.
4. Wagonjwa na wenye kuuguza wagonjwa.
5. Msafiri.
6. Kwa kuzuiliwa na hali ya hewa kama vile mvua, joto kali sana
7. Kuwa na khofu ya kudhuriwa njiani.



Idadi ya Watu katika Jamaa ya Ijumaa
Kuhusu idadi ya watu inayokamilisha au inayotosheleza jamaa ya swala ya Ijumaa haikutajwa kabisa katika Qur-an wala katika Hadithi, ila tunaona katika Hadithi kuwa Mtume (s.a.w) alibakiwa na watu kumi na mbili tu wakati Maswahaba wake walipokimbilia msafara na kumuacha akiendelea kuhutubu. Hivyo, si jambo la busara kwetu kung’ang’ania kuwa ni lazima idadi maalum ya watu ifikiwe ndio swala ya Ijumaa iswihi. Kutokana na Hadithi ya Mtume (s.a.w) jamaa huanza na watu wawili - Imamu na Maamuma.



Abu Mussa al-Ash’ariyyi ameeleza kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema: “Wawili au zaidi ya wawili hufanya jamaa ”. (Ibn Majah).


Maimamu wa ‘Fiqhi’ wametofautiana juu ya idadi ya watu wanaotosheleza jamaa ya swala ya Ijumaa. Imamu Abu Hanifa na Ahmad bin Hambal wametoa rai kuwa jamaa inakamilishwa na watu watatu na Imamu wa nne. Imamu Abuu Yusufu yeye amesema jamaa ya Ijumaa inatoshelezwa na watu wawili na Imamu wa tatu. Ambapo Imamu Shafii anasema kuwa Jamaa ya swala ya Ijumaa inatoshelezwa na watu arubaini (40) wakazi wa mji. Kwa ujumla utaona kuwa maoni ya Maimamu watatu - Abu Hanifa, Ahmad na Abuu Yusuf, yanakaribiana sana, na kiwango cha chini cha jamaa alichokitaja Mtume (s.a.w) katika hadithi iliyotangulia. Imamu Shafii yuko mbali sana na kiwango hicho. Jambo muhimu la kuzingatia ni kwamba, kinachotakiwa tukifuate moja kwa moja ni Qur-an na Sunnah ya Mtume, na mawazo ya yeyote yule mwingine hatulazimiki, kwa namna yoyote ile iwayo, kuyafuata mpaka kwanza tuyaingize kwenye kipimo (kigezo) cha Qur-an na Sunnah.



Namna ya kutekeleza swala ya Ijumaa
Swala ya Ijumaa ina tanguliwa na adhana mbili. Adhana ya kwanza ni wito wa kuwatanabahisha watu wafunge shughuli zote za kawaida kwa ajili ya swala ya Ijumaa. Adhana hii kwa kawaida inakuwa kabla ya wakati wa swala kuingia. Adhana ya pili ya Ijumaa inatolewa wakati inapoingia swala ya adhuhuri. Baada ya adhana ya pili khatibu husimama mimbarini au ulingoni na kuanza kutoa khutuba huku akiwa amewaelekea watu. Wakati wa Mtume (s.a.w) na Ukhalifa wa Abubakr na ‘Umar adhana ya Ijumaa ilikuwa moja tu, ya wakati wa kwanza khutuba. Adhana ya nyongeza ambayo ndiyo adhana ya kwanza ilianzishwa wakati wa ukhalifa wa ‘Uthman bin Affan.
Swala ya Ijumaa inatanguliwa na khutuba mbili zinazotolewa na khatibu wenigne wote wakiwa wasikilizaji. Baada ya khutuba, swala ya ijumaa hukamilika kwa kuswali rakaa mbili kwa jamaa.



Khutuba ya Ijumaa
Khutuba ni jambo lililosisitizwa sana siku ya Ijumaa. Khutuba hii imegawanyika katika sehemu mbili zinazotenganishwa na kikao cha muda mfupi. Hivi ndivyo alivyokuwa akifanya Mtume (s.a.w) kama inavyodhihiri katika hadithi ifuatayo:



Jabir bin Samurat (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akitoa khutuba mbili, na katika khutuba hizo alikuwa akisoma Qur-an na kuwaonya na kuwausia watu. Sw ala yake ilikuwa fupi kiasi na khutuba yake pia ilikuwa fupi kiasi.” (Muslim).


Lengo la khutuba ni kuwausia, kuwatanabahisha na kuwakumbusha, Waislamu juu ya wajibu wao kwa Allah (s.w) na viumbe vyake na juu ya lengo lao la maisha kwa ujumla na namna ya kulifikia. Hivyo ili khutuba ifikie lengo lake, hapana budi itolewe kwa lugha ya wale wanaohutubiwa. Lengo la khutuba na lengo kuu la swala ya Ijumaa kwa ujumla halitapatikana iwapo khutuba itatolewa katika lugha isiyoeleweka kwa wasikilizaji.



Khutuba ya Ijumaa inatimia kwa kutimiza nguzo tano zifuatazo:
1. Kumshukuru au kumhimidi Allah kwa kusema: Al-hamdulillaah…
2. Kumtakia Rehma Mtume (s.a.w).
3. Kuwausia Waislamu kumcha Mungu au kuwapa mawaidha juu ya Uislamu.
4. Kusoma Qur-an angalau aya moja.
5. Kuwaombea Waislamu dua.



Khatibu ni sharti awe na udhu na akhutubu akiwa amesimama na kuwaelekea anao wakhutubia. Pia kulingana na Sunnah ya Mtume (s.a.w) ni vyema khutuba isiwe ndefu sana kama Mtume (s.a.w) alivyoshauri katika kauli yake ifuatayo:



Ammar (a.r) amesimulia kuwa alimsikia Mtume (s.a.w) akisema: Urefu wa swala ya mtu na ufupi wa khutuba yake ni alama ya kuwa na hekima. Kwa hiyo refusha swala na fupisha khutuba kwani kuna dawa katika kukhutubu. (Muslim).



Swala ya Ijumaa
Baada ya khutuba mbili, swala hukimiwa kama kawaida na Imamu kuswalisha rakaa mbili za swala ya Ijumaa kwa sauti. Baada ya kusoma suratul Fatiha, Imamu anaweza kusoma sura yoyote lakini kutokana na hadithi nyingi za Mtume (s.a.w), ni sunnah katika rakaa ya kwanza kusoma Suratul Jumua (sura ya 62) na katika rakaa ya pili kusoma sura ya 63 Al-Munafiquun kama tunavyofahamishwa katika hadithi ifu atayo:



Ibn Abbas (r.a)amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) alikuwa akisoma katika swala ya Al-fajir ya siku ya Ijumaa sura ya 32 - As-sajda na sura ya 76 - Ad-dahr na alikuwa akisoma suratul Jumua na Suratul-Munaafiquuna. (Muslim).



Nuuman bin Bashir (r.a) amehadithia kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akisoma katika swala za Iddi mbili na swala ya Ijumaa suratul A ’ala (87) na suratul Ghashiyah (88). Na kama imesadifu kuwa siku ya Idi ndio siku ya Ijumaa, basi alikuwa akisoma sura mbili hizi katika swala zote, yaani ya Idi naya Ijumaa. (Muslim).



Baada ya swala ya Ijumaa na swala nyingine yoyote ya jamaa Waislamu wanashauriwa wasambae katika ardhi kutafuta fadhila za Allah huku wakimkumbuka kwa kuchunga barabara mipaka aliyoiweka ambayo iko wazi. Rejea Qur’an (62:10)




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 836


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

haki ya kutaliki: kuacha na kuachwa katika ndoa ya kiislamu
Haki ya KutalikiKatika jamii nyingi za kjahili haki ya kutoa talaka iko kwa mwanamume tu na mwanamke hana haki yoyote ya kumtaliki mumee. Soma Zaidi...

Hukumu ya Talaka kabla ya kufanya jimai
Talaka Kabla ya Jimai:Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa. Soma Zaidi...

Namna lengo la zakat linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Adhabu ya mzinifu katika jamii ya kiislamu
(iii) Adhabu ya UzinifuKatika Sheria ya Kiislamu mtu haadhibiwi mpaka atende kwa uwazi matendo yenye kuvuruga utaratibu na amani ya jamii. Soma Zaidi...

Utaratibu wa kuzika maiti ya kiislamu, hatua kwa hatua
Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa. Soma Zaidi...

Zoezi la nne mada ya fiqh.
Maswali mbalimbali kuhusu fiqh. Soma Zaidi...

Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...

Jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ambavyo mgonjwa anatakiwa aswali kulingana na ugonjwa wake. Soma Zaidi...

namna ya kutekeleza Funga za Sunnah pamoja na majukumu mengine
Soma Zaidi...

Kutoa kati kwa kati
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Madhara ya riba kwenye jamii
Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba? Soma Zaidi...

Umuhimu wa uchumi katika uislamu
Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu. Soma Zaidi...