ZIJUWE FUNGA ZA KAFARA NA JINSI YA KUZIGUNGA


image


Post hii itakufundisha kuhusu funga za kafara, zinavyotokea na na jinsi ya kuzifunga.


Funga za Kafara

Funga za kafara ni funga anazolazimika Muislamu kuzileta ili ziwe kitubio baada ya kutenda kosa fulani. Yaani funga hizi zimewekwa na sheria ya Kiislamu kama fidia au faini baada ya kutenda kosa na kutaka kutubia kwa Allah (s.w). Zifuatazo ni funga za kafara kama zilivyobanishwa katika Qur-an na Hadith:

 


(i) Kufunga miezi miwili mfululizo kwa Muislamu aliyemuua mtu kwa bahati mbaya na akakosa mali ya kulipia fidiya kama inavyobainishwa katika Qur-an:

 

Na haiwi kwa Mu is lamu kumuua Muislamu (mwenziwe kusudi) ila kwa kukosea.Na mwenye kumuua Muislamu kwa kukosea basi ampe uungwana mtumwa aliye Muislamu, na pia atoe fidiya (Malipo) kuwapa warithi wake. Isipokuwa waache weny ewe kwa kufanya kuwa ni sadaqat (yao). Na aliyeuawa akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Mu is lam, basi ampe uungwana mtumwa aliye Muislamu (basi, hapana wa kupewa fidiya). Na kama (aliyeuawa) ni moja wa watu ambao kuna ahadi baina yenu na baina yao; basi warithi wake wapewe malipo na pia apewe uungwana mtumwa aliye Muislamu. Na asiyepata basi afunge miezi miwili mfululizo. Ndio kitubio kitokacho kwa Mwenyezi Mungu.Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mw eny e Hekim a. (4:92).

 


(ii) Kufunga miezi miwili mfululizo kwa mtu atakayemsusa mkewe kwa kumfananisha na mama yake kwa kutamka: “Wewe kwangu mimi nakuona kama mgongo wa mama yangu.” Maneno haya yalitamkwa na Sahaba wa Mtume (s.a.w) - Aus Ibn Samit (r.a), walipogombana na mkewe. Maneno haya kwa jamii ya Waarabu wakati ule wa Mtume (s.a.w) yalikuwa mabaya sana na yalikuwa ni ya kumdhalilisha mwanamke. Hivyo baada ya kufanyika kitendo hiki, mkewe huyu Sahaba alikwenda kwa Mtume (s.a.w) kushitakia; lakini Mtume (s.a.w) hakuweza kumpatia ufumbuzi wa tatizo lake. Mama huyu alizidi kusononeka sana huku akitarajia nusra ya Allah (s.w).Ni katika hali hii ya kusononeka huyu mama Allah (s.w) alishusha kwa Mtume wake aya zifuatazo:

 


Mwenyezi Mungu amekwisha sikia usemi wa mwanamke yule anayejadiliana nawe sababu ya mumewe, na anashtaki mbele ya

 


Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu; anayasikia majibizano yenu; hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia mwenye kuona. Wale miongoni mwenu wawaitao wake zao mama zao, (kwa hivyo wakajiepusha nao wasiwaingilie wala wasiw ape ruhusa kuolewa na mwanaume wengine), hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa.Wanasema neno baya na la uwongo.Na Mwenyezi Mungu ni mwenye msamaha, mwenye maghfira.(58:1-2).

 


Baada ya kosa la huyu Sahaba kubainishwa katika aya hizi, aya zifuatazo zinatoa kitubio au adhabu ya kosa hili:

 

Na wale wawaitao wake zao mama zao kisha wakarudia katika yale w aliyoyasema (wakataka kuw arejea wake zao w aendelee kuishi kama kawaida), basi wampe mtumwa huru kabla ya kugusana.Mnapewa maonyo kwa haya. Na Mwenyezi Mungu anajua (yote) mnayoyatenda. Na asiye pata (mtumwa) basi afunge saumu ya miezi miwili mfululizo kabla ya kugusana; na asiyeweza basi awalishe maskini sitini.

 

(Mmeambiw a haya ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu,na kwa makafiri iko adhabu iumizayo. (58:3-4).

 


(iii) Kufunga siku tatu mfululizo kama kafara ya kuvunja kiapo kama tunavyoamrishwa katika aya ifuatayo:

 

“Mwenyezi Mungu hatakuteseni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakukamateni kwa viapo mlivyo viapa kwa nia mlioifunga bara bara. Basi kafara yake ni kuw alisha maskini kumi kwa chakula cha katikati mnacho walisha watu wa majumbani mwenu, au kuwavisha, au kumpa uungwana mtumwa. Lakini asiyeweza kupata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na vilindeni viapo vyenu (msiape kisha msitimize). Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainisheni aya zake ili mpate kushukuru ” (5:89).

 


(iv) Kufunga miezi miwili mfululizo kama kitubio cha kufanya tendo la ndoa kati ya mume na mkewe makusudi katika mchana wa mwezi wa Ramadhani.

 


(v)Mtu aliyehirimia Hijja au Umra haruhusiwi kuwinda na endapo atavunja amri hii ya kutowinda kitubio au kafara yake ni kufunga kama inavyobainishwa katika aya ifuatayo

 


“Enyi mliomini! Msiue mawindo na hali (ya kuwa) mumo katika Hija au Umra. Na miongoni mwenu atakayemuua kwa kusudi, basi malipo yake yatakuwa kwa (kuchinja) kilicho sawa na alichokiua,katika wanyama wanaofugwa,kama watakavyohukumu waadilifu wawili miongoni mwenu mnyama huyo apelekwe iliko Ka’aba, au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake hili ... (5:95). Muda wa kufunga utategemeana na thamani ya mnyama ambaye angalimchinja katika hesabu ya vibaba vya chakula.

 


(vi) Kama mwenye kuhiji au kufanya Umra atavunja miiko ya Ihram au iwapo atashindwa kutekeleza baadhi ya matendo ya Hijja, atalazimika kufunga kama inavyobainishwa katika aya ifuatayo:

 

Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na kama mkizuiwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana (nao ni mbuzi). Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjioni mwao. Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana vya kumuudhi kichwani mwake (akafanya yaliyokatazwa kama vile kunyoa), basi atoe fidia kwa kufunga au kutoa sadaqat au kuchinja wanyama (2:196).



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Maktaba ya vitabu    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Tarstibu za kulipa swaumu ya Ramadhani
Hapa utajifunza namna ambayo utatakiwa kulipa funga ya Ramadhani kwa siku ambazo hukufunga Soma Zaidi...

image Mambo yanayoharibu Udhu (yanayobatilisha udhu)
Post hii inakwenda kukufundisha mambo ambayo hubatilisha udhu yaani mam,boa mbayo yanaharibu udhu. Soma Zaidi...

image Sera ya uchumi katika uislamu
Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu. Soma Zaidi...

image Ni ipi hukumu ya muislamu anayekula mwezi wa Ramadhani bila ya sababu ya kisheria
Endapo muislamu hatafunga mwezi wa Ramadhani bila ya ruhusa je atatakiwa afanye nini. Je ataweza kuilipa funga hiyo? Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.
Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla. Soma Zaidi...

image Mgawanyo wa mirathi kutoka kwenye Quran
Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo. Soma Zaidi...

image Historia ya adhana na Iqama na jinsi ya kuadhini.
Hadithi hii inakwenda kukufundisha historia fupi ya adhana pia utakwenda kujifunza jinsi ya kuadhini na kuqimu. Soma Zaidi...

image Mambo yanayobatilisha funga au yanayoharibu swaumu.
Hapa utajifunza mambo ambayo akiyafanya mtu aliyefunga, basi funga yake itaharibika. Soma Zaidi...

image Jinsi ya kuswali swala vitani
Post hii itakufundisha taratibu zinazofanyika ilibkuswalibukiwa vitani. Soma Zaidi...

image Zijuwe nguzo 17 za swala.
Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala. Soma Zaidi...