22.
22. Kuwa Mpole na Mnyenyekevu
Mtu mpole ni yule aliyetulia, asiyelipuka kwa hamaki. Huzungumza na watu kwa sauti ya chini. Akiudhiwa halipuki kwa hasira na kupaza sauti bali husubiri kwa utulivu. Huwa ni mwepesi wa kuwasamehe waliomkosea. Muumini hana budi kujipamba na sifa hii ya upole kwani ni miongoni mwa sifa za waja wema wa Allah (s.w)
“Na waja wa Rahman ni wale wanokwenda (na kurejea) katika ardhi kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama”. (25:63)
Pamoja na kujipamba na tabia ya upole, Waislamu hawaruhusiwi kuyaachia maovu yakafanyika katika jamii bila ya kuyakemea. Ni juu ya Waumini kuamrisha mema na kukataza maovu na kuwa wagumu kwa maadui wa Uislamu na wenye kuhurumiana wao kwa wao. Hii ndiyo tabia ya Mtume na Maswahaba wake kama tunavyojifunza katika Qur’an:
“Muhammad ni Mtume wa Allah na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti (ngumu) dhidi ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao...” (48:29).
Pindi maadui wakiacha uadui wao dhidi ya Uislamu, waislamu watawaelekea kwa upole:
“Na kama (hao maadui) wakielekea katika amani, wewe pia ielekee (amani) na mtegemee Allah. Hakika yeye ndiye asikiaye na ajuaye.Na kama wakitaka kukuhadaa basi Allah atakutosheleza. Yeye ndiye aliyekusaidia kwa nusura yake na kwa walioamini”. (8:61-62).
Umeionaje Makala hii.. ?
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha hatuwa kwa hatuwa jinsi ya kumuosha maiti wa kiislamu
Soma Zaidi...Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu?
Soma Zaidi...Uchumi wa kiislamu unatofautiana sana na uchumi wa kikafiri. Hapa utajifunza tofauti hizo.
Soma Zaidi...Katika uislamu imekatazwa kutamani kufa hata kama utakuwa ni mtu muovu sana ama mchamungu sana.
Soma Zaidi...