Ni zipi nguzo za swaumu na masharti ya Swaumu

Ni zipi nguzo za swaumu na masharti ya Swaumu

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Ni zipi nguzo za swaumu na masharti ya Swaumu

Nguzo za Funga



Nguzo za funga ni mbili: Kutia Nia na kujizuilia na kila chenye kufunguza tangu mwanzo wa alfajiri mpaka kuingia magharibi.Nia ni dhamira anayokuwa nayo mtu moyoni mwake kuwa atafunga. Nia ya funga ya faradhi inatakiwa iletwe kabla ya Alfajir, kwa mnasaba wa Hadith ifu atayo:



Bibi Hafsah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: ambaye hakunuia kufunga kabla ya alfajir, hana funga. (Tirmidh, Abu Daud, Nis a i).



Ama nia ya funga za sunnah, inaweza kuletwa mchana iwapo mtu hajala chochote tangu alfajir kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:



Aisha, Mama w a Waumini (r.a) ameeleza: Mtume (s.a.w) alikuja kwangu siku moja akaniuliza: Una chochote (cha kula)? Nilijibu: Hakuna. Kisha akasema: β€œBasi nitafunga.” Siku nyingine alikuja tena kwetu tukamuambia: Mtume wa Allah, tumeletewa zawadi ya Hais (aina ya chakula cha mchanganyiko wa Tende na Siagi). Kisha akasema: β€œNionyeshe, nilifunga tangu asubuhi. Kisha alikula chakula kile.” (Muslim).



Katika Hadith hii tunajifunza mambo mawili. Kwanza tunajifunza kuwa mtu anaweza kunuia funga ya sunnah mchana kabla ya adhuhuri, iwapo atakuwa hajala chochote tangu alfajiri.



Pili, tunajifunza vile vile kutokana na Hadith hii kuwa mtu anaruhusiwa kuvunja funga ya sunnah pasi na sababu ya kisharia.




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2887

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰5 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana: