Maumivu makali ya tumbo la chango wakati wa hedhi na sababu zake

Maumivu makali ya tumbo la chango wakati wa hedhi na sababu zake

Kwa nini unapata maumivu makali wakati wa kuingia hedhi, je unajuwa sababu za maumivu makali ya tumbo la chago.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Maumivu makali ya tumbo la chango wakati wa hedhi na sababu zake


MAUMIVU YA HEDHI MAKALI SANA



Maumivu ya tumbo la hedhi kikawaida yanatambulika kama tumbo la chango kwa wakinamama. Katika hali ya kawaida maumivu haya sio makali kiasi cha kuharibu ratiba za mwanamke. Lakini hutokea wakati mwingine yakawa makali sana kiasi cha kupelekwa hospitali, ama mwanamke kushindwa kufanya shughuli zake. Sasa nini sababu ya maumivu haya kupitiliza? Makala hii itakwenda kuangalia sababu za maumivu makali ya tumbo la chango au maumivu makali ya tumbo la hedhi.


Sababu za maumivu makali ya tumbo la hedhi
Kama mwanamke anaingia hedhi kwa na maumivu makali anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu kama ibuprofen. Lakini kama kuna sababu nyingine zinazopelekea maumivu kuwa makali hata akimeza dawa hii maumivu yatakuwa ni yenye kuendelea.


Dalili za maumivu makali ya hedhi ni
1.maumivu yasiyokata hata baada ya kumeza dawa za kupunguza maumivu
2.Kama maumivu makali kiasi cha kuharibu ratiba za shunguli za kawaida
3.Kama maumivu yanafuatana na damu nyingi ama kuganda kwa damu


Nini sababu ya maumivu makali ya hedhi?
1.kuota kwa tishu (nyamnyama)
maeneo mengine tofauti na tumbo la mimba. Kitaalam hali hii inatambulika kama endometriosis. Hali pia inaweza kuwa na dalili zifuatazo:-
A.Kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi
B.Hedhi kuchukuwa siku zaidi ya 7
C.Kutokwa na damu kabla ya siku za hedhi kufika
D.Maumivu ya tumbo
E.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
F.Kupata maumivu wakati wa haja kubwa.
G.Kuchelewa kupata ujauzito


2.Shida kwenye mfumo wa homoni, hali hii kitaalamu inatambulika kama Polycystic Ovary Syndrome (PCOS). hali hii ni ya kawaida sana takribani kwa kila wanawake 10 mmoja wao huwa na hali hii. Miongoni mwa sababu kuu ni kuwa na homoni za kiume nyingi (androgens) na kutokuwa na siku maalumu za kupata hedhi. Hali hii inaweza kuwa na dalili kama:
A.Kutokwa na damu nyingi sana
B.Kupata hedhi kwa muda mrefu
C.Kuota ndevu ama mwele kuwa nyingi maeneo mbali mbali ya mwili kama ilivyo kwa wanaume
D.Kuwa na uzito mwingi na usio rahisi kuupunguza
E.Kuota chunusi
F.Kunyonyoka kwa nywele na kukosa afya
G.Kuwa na madoa madoa meusi kwenye ngozi


3.kuwa na uvimbe kwenye kizazi kitaalamu hali hii hutambulika kama fibroids. Huu I uvimbe usio wa saratani unaoota kwenye tumb la mimba. Unaweza kuwa uvimbe mmoja ama zaidi. Unaweza pia kuwa na uvimbe bila ya kuonyesha dalili zozote hali hii ikichanganyika na maumivu ya chango inaweza kuonyesha dalili kaka:
A.Maumivu ya mgongo kwa chini
B.Maumivu ya miguu
C.Kupata damu nyingi ya hedhi
D.Kupata hedhi zaidi ya wiki
E.Kukosa choo kikubwa
F.Kukojoakojoa mara kwa mara
G.Kushindwa kumaliza mkojo wote.


4.kuwa na maambukizi ama mashambulizi ya bakteria, fangasi ama virusi kwenye kizazi. Kitaalamu hii huitwa Pelvic Inflammatory disease au maarufu kama PID. Miongoni mwa dalili zake ni:-
A.Maumivu wakati wa tendo la ndoa
B.Kutokwa na damu kabla ya hedhi na baada ya hedhi
C.Kutokwa na majimaji yanayotoa harufu kwenye uke
D.Maumivu wakati wa kukojoa
E.Homa
F.Kutokwa na damu kidogo kabla ya kuingia hedhi na baada ya kuingia hedhi


5. Maumbile ya kwenye shingo ya uzazi kitaalamu huitwa cervical stenosis, hii ji hali ambayo mlango wa shingo ya kizazi unakuwa ni mdogo sana. Huenda mwanamke amezaliwa ivyo ama mlango umeziba baadaye.


6.kukaza kwa tishu (nyamnyama) za kwenye tumbo la mimba kitaalamu hai hii inatambulika kama (andenomyosis). hali hii hutokea pale nyamnayma laiki za kwenye tumbo la mimba zinapokuwa ngumu na kubadilika kuwa misuli.


7.matumizi ya baadhi ya njia za kuthibiti uzazi kama Intrauterine Device (IUD). hiki ni kifaa kidogo kinachowekwa kwenye tumbo la mimba. Kijikifaa hiki mwa wanawake wengine kinaweza kuwaletea shida za kiafya kama:
A. Maumivu makali wakati wa hedhi
B. Kutokuwa na siku maalumu za hedhi yaani hedhi inaruka ruka
C. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi


NINI NIFANYE KUKABILIANA NA MAUMIVU HAYA
1.fanya mazoezi mara kwa mara
2.Tumia pad zilizo kavu
3.Hakikisha huna stress yaani misongo ya mawazo kupitiliza
4.Oga maji ya moto
5.Tumia dawa za kupunguza maumivu ya chango kama ibuprofen na acetaminophen
6.Tumia vitamini kama vitamini B1, na B6, madini ya magnesium na omega-3 fatty acid.




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 3815

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Dalilili za tetekwanga
Dalilili za tetekwanga

posti hii inazungumziaTetekuwanga . Tetekwanga(varisela) ni maambukizi ya virusi ambayo husababisha kuwasha, kama vile upele. Tetekuwanga huambukiza sana watu ambao hawajapata ugonjwa huo wala kupewa chanjo dhidi yake. Kabla ya chanjo ya mara kwa mara

Soma Zaidi...
Maradhi ya Pumu yanatokeaje?
Maradhi ya Pumu yanatokeaje?

Nini hasa kinatokea mpaka mtu anakuwa na pumu, ama anashambuliwa na pumu. Makala hii itakwenda kukufundisha jambo hili

Soma Zaidi...
 Ni Nini husababisha kukosa choo? (Constipation)
Ni Nini husababisha kukosa choo? (Constipation)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazopelekea kukosa choo ,yaani kinyesi kuwa kigumu au kukosa kabisa choo.

Soma Zaidi...
Dalili za maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Dalili za maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo

Posti hii inahusu zaidi maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo,ni dalili ambazo ujionesha kwa mtu akiwa na shida kwenye utumbo mdogo na tumbo la kawaida.

Soma Zaidi...
Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces
Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces

Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis.

Soma Zaidi...
Minyoo na athari zao kiafya
Minyoo na athari zao kiafya

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu minyoo na athari zao kiafya

Soma Zaidi...
Dalili za Homa ya uti wa mgongo (meningitis)
Dalili za Homa ya uti wa mgongo (meningitis)

Posti hii inahusu zaidi dalili za Homa ya uti wa mgongo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye maambukizi kwenye uti wa mgongo.

Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa Donda koo
Dalili za ugonjwa wa Donda koo

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa Donda Koo ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea viitwavyo kwa kitaalamu corynebacterium diphtheria, ugonjwa huu ushambulia Koo na unaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa, mate na

Soma Zaidi...
Namna magonjwa ya koo yanavyosambaa
Namna magonjwa ya koo yanavyosambaa

Posti hii inahusu zaidi namna ya magonjwa ya koo yanavyosambaa, magonjwa haya usambaa kutoka sehemu Moja kwenda nyingine kwa njia tofauti kama ifuayavyo

Soma Zaidi...