Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula ambavyo vinaweza kupunguza presha ya kupanda
VYAKULA AMBAVYO HUSAIDIA KUPUNGUZA PRESHA YA KUPANDA AMA HULINDA MWILI DHIDI YA PRESHA YA KUPANDA.
Presha ya kupanda inaweza kupelekea athari kubwa na mbaya sana kwenye afya ya mtu. Presha ya kupanda isipotibiwa ama mtu asipofuata masharti ya kuishi na ugonjwa huu madhara makubwa yanaweza kutokea. Kifo, kupasuka kwa mishipa ya damu, kupalalaizi, kuharibika kwa figo na moyo kushindwa kufanya kazi na kupata shambulio la moyo yote haya yanaweza kuwa ni matokeo ya presha ya kupanda pindi isipotibiwa ama mtu asipofata masharti.:-
Unaweza kupamana na presha kwa kufuata mashari kama kufanya mazoezi, kula vyakula salama kwa presha, kupunguza misongo ya mawazo, kupunguza kula chumvi, kupunguza uzito, kupunguza ama kuacha sigara na pombe. Miongoni mwa vyakula salama kwa presha ni kama
1.Mboga za majani ambazo zina madini ya potassium kwa wingi. Madini haya ni mujarabu sana katika kulinda na kuimarisha afya ya moyo. Ulaji wa mboga hizi unaweza kuwa ni njia ya kujilinda na presha ya kupanda. Miongoni mwa mboga hizi ni kama spinachi
2.Maziwa: maziwa ni katika vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi na pia yana mafuta kwa uchache. Hali zote mbili hizi ni muhimu kwa afya ya moyo.
3.Ndizi; ndizi ni katika matunda yenye madini ya potassium kwa wingi. Ulaji wa ndizi unaweza kuwa ni msaada mzuri kwa kulinda mwili dhidi ya presha ya kupamda.
4.Mayai
5.Samaki aina ya salmon na wanaofanana nao.
6.Ulaji wa mbegu za mimea kama maboga na alizeti
7.Kitunduu thaumu: unaweza kutumia vitunguu thaumu kwa kula ama kutafuna, ni vyema kufunga mdomo wakati unapotafuna.
8.Makomamanga; unaweza kula atunda hili kama juisi ama kula kawaida.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi faida za matumizi ya vyakula vya asili, kama tunavyojua kwamba mababu na mabibi zetu walitumia vyakula vya asili wakaishi miaka mingi kweli.
Soma Zaidi...Posti hii itakwenda kukupa faida za kula samaki kwenye mwili wako.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za karoti na umuhimu wake kiafya
Soma Zaidi...Hapa tutaona kuhusu virutubisho vya wanga, kazi zake na athari za upungufu wake
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kuwepo kwa vyakula vya kisasa, vyakula vya kisasa ni vyakula vya madukani ambavyo vimetengenezwa na kuwekwa kwenye maduka
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maini
Soma Zaidi...