JITIBU KWA KITUNGUU THAUMU: faida za kiafya za kitunguu thaumu

JITIBU KWA KITUNGUU THAUMU: faida za kiafya za kitunguu thaumu

Kitunguu thaumu ni katika viungo vya mboga na chakula.

JITIBU KWA KITUNGUU THAUMU: faida za kiafya za kitunguu thaumu

FAIDA ZA KITUNGUU THAUMU

Kitunguu thaumu ni katika viungo vya mboga na chakula. Karibia maeneo yote duniani wanatumia kitungiuu thaumu. Kitunguu thaumu huweza kutumika kikiwa kibichi. Wataalamu wa afya wanaeleza faida nyingi za kiafya. Wataalmu wa afya wametengeneza kidonge kwa kutumia vitunguu thaumu ili kuwezesha upatikanaji wa virutubisho vya mmea huu.

 

Kitunguu thaumu kina chembechembe nyingi ambazo ndizo husaidia katika tiba. Miongoni mwa chembechembe hizo ni chembechembe za salfa ziitwazo allicin. Allicin hupatikana kwenye kitunguu kibichi pindi kinapopondwa ama kutafunwa. Chembechembe nyingine ni kama  diallyl disalfide na s-allyl cysteine.

 

Zifuatazo ni faida za kiafya za kitunguu thaumu

  1. Kunapatikana virutubisho vingi ndani ya kitunguu thaumu kama vitamini B6, B1 na vitamini C.  madini ya calcium, copper, phosphoros, potassiumna selium.
  2. Hushusha presha ya damu (hypertsnsion). kitunguu thaumu sio kizuri kwa wenye presha ya kushuka, kwani itashuka sana.
  3. Hudhibiti cholesterol (kolesto) hivyo husaidia katika kuzuia hatari ya kupata maradhi ya moyo.
  4. Kitunguu thaumu kina antioxidant ambazo husaidia kupunguza hatari ya kupata maradhi ya kusahausahau
  5. Huimarisha mfumo wa kinga mwilini.
  6. Huondoa sumu za vyakula mwilini.
  7. Huimarisha afya ya mifupa.
 


                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views: 3181

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 ai web app     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Yafahamu magonjwa nyemelezi kwa watoto chini ya miaka mitano

Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano,. Ni magonjwa yanayowapata watoto wadogo kwa sababu kinga Yao bado ni ndogo.

Soma Zaidi...
Vyakula vya wanga

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za vyakula vya wanga na umuhimu wake mwilini

Soma Zaidi...
Dalili za ukosefu wa madini ya iodini (goiter)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za upungufu wa iodini ambapo kitaalamu hujulikana Kama goiter. Goiter Ni Sababu ya kawaida ya goiter duniani kote ni ukosefu wa iodini katika chakula. Nchini Marekani, ambako utumiaji wa chumvi yenye iodini ni j

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula samaki

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula samaki

Soma Zaidi...
Vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo

Posti hii inahusu zaidi vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo, ni vyakula ambavyo upunguza makali kwenye uti wa Mgongo.

Soma Zaidi...