Dawa ya kiungulia na njia za kuzuia kiungulia
utajifunza njia za kuzuia kiungulia, dalili za kiungulia na dawa ya kutibu kiungulia.
NJIA ZA KUZUIA KIUNGULIA
Kiungulia hutokea pale tindikali zilizopo tumboni zinapanda juu na kufikia koo sehemu ambayo inaunganisha tumbo na koo la chakula. Kiungulia sio shida sana kiafya kwani huwa kiaondoka chenyewe. Hata hivyo kuna watu wapo hatari kupata kiungulia cha mara kwa mara.
Je na wewe ni mmoja katika wanaopata kiungulia mara kwa mara. Je kiungulia ni kikali kiasi cha kuharibu ratiba na uhuru wako? Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakuletea njia ambazo zitakusaidia kuzuia kiungulia cha mara kwa mara.
Njia za kuzuia kiungulia
1.Usile chakula kingi kupitiliza
2.Punguza uzito ulio nao
3.Punguza unywaji wa pombe
4.Usinywe sana chai ya majani ya chai yenye caffein kwa wingi
5.Tafuna bigjii zisizo na sukari nyingi
6.Wacha kutumia kitunguu kisichopikwa kama kwenye kachumbari
7.Epuka vinywaji vyenye carbonate. Soma lebo ya kinywaji chako kama ni soda ama maji kama kuna carbonate
8.Usinywe kwa wingi juisi zilizotokana na vitu vya uchachu kama limao
9.Punguza kula chokoleti kwa wingi
10.Unapolala inuka kichwa chako kwa mfano tumia mto
11.Usilale ndani ya masaa matatu baada ya kula
12.Ukilala lalia upande wa kushoto usilalie upande wa kulia.
Dawa za kutibu kiungulia
Unaweza kutibu kiungulia kwa kutumia antacid kama vile Tums, Rolaids na Maalox. Dawa ambazo zimetengenezwa kwa madini ya calcium carbonate au magnesium ni nzuri pia. Magnesium si nzuri kama ujauzito upo mwishoni.
Madaktari wengi wanakataza kwa wajawazito matumizi ya antacid ambazo zimechanganywa na sodium, ama zila lebo ya aluminium carbonate kwani zinawza kupelekea kukosa choo. Pia dawa hizi za kiungulia zinakatazwa kwa wajawazito Alka-Seltzer.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 ai web app 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Vinywaji vyakula salama kwa mwenye Presha ya kupanda
Je umesha wahi kujiuliza kuwa ni vinywaji vipi mwenye presha ya kupanda anafaha kutumia, Unadhani ni maji, mvinyo wa pombe, chai na kahawa. Bila shaka ungependa kujuwa zaidi kuhusu jambo hili. Makala hii ni kwa ajili yako
Soma Zaidi...Mafidodo (mafindofindo) au tonsils kweye koo je inaweza ikawa Ni moja kati ya dalil za ukimwi
Tezi za lymph huanza kuonyesha dalili za kuwa mwili upo katika mapambano dhidi ya vijidudu vya maradhi. Ishara ni pale utakapoona tezi za lymph zina maumivu. Tezi hizi hupatikana kwenye mapaja, kwapa nashingo.
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kula topetope/ accustard apple
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula topetope/ accustard apple
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kula kungumanga/nutmeg
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kungumanga/nutmeg
Soma Zaidi...