Papai (papaya)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula papai

Papai (papaya)

Papai ni katika matunda yanayoingiza afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia kuna potassium na folate. Pia tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani.

 

Pia papai lina vitamin B, vitamin E na vitamin K. Pia lina madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper. Pia punje za papai ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo. Pia kwenye papai kuna protelytic enzymes hawa husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kum eng’enya chakula).

 

Papai linatambulika kwa kuwa na uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeheka kwa haraka. Ndani ya papai kuna Zeaxanthin hii ni anti oxidant ambayo inakazi ya kuchija miale hatari ya jua. Pa inaaminika kuwa antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.

 

Papai huaminika kusaidia kupunguza hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu. Hupunguza hatari ya kuuguwa pumu. Ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa beta-carotene ndani ya papai husaidia kwa wagonjwa wenye pumu.

 

Ulaji wa antioxidanti zilizopo kwenye papai kama beta-carotene husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya saratan kwa vijana. Ulaji wa tunda hili husaidia katika kudhibiti upatikanaji wa saratani ya kwenye via vya uzazi hasa saratani ya korodani.

 

Papai ni katika matunda yenye vitamini K ambavyo ni muhimu katika afya ya mifupa. Hivyo ulaji wa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa na kudhibiti kupasuka kwa mifupa. Vitamin k pia husaidia katika ufyonzwaji wa madini ya calcium na huzuia upotevu wa madini haya kupitia mkojo. Kupuka madini haya pia ni muhimu katika kuimarisha na kudhibiti afya ya mifupa.

 

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa papai n I tunda zuri kwa wenye kisukari. Papai ni katika vyakula vya kambakamba ambacho kina maji kwa wingi. Tafiti zinaonesha kuwa watu wenye kisukari type 1 diabetes wameweza kupunguza kiwango cha sukari mwilini mwao. Wakati huohuo watu wenye kisukari type 2 diabetes wameweza kuimarisha kiwango cha sukari mwilini pamoja na kiwango cha homoni ya insulin.

 

Ndani ya papai kuna enzyme zinazoitwa papain hizi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Pia kama tulivyo sema papai lina maji nmengi na kambakamba vyote kwa pamoja husaidia katika upatikanaji wa choo na kusaidia katika kudhibiti mmeng’enyo wa chakula.

 

Madini ya potassium (aina ya chumvi) na vitamini vilivyomo kwenye papai husaidia katika kulinda afya ya moyo dhidi ya maradhi hatari yanayoshambulia mfumo wa usukumwaji wa damu. Ulaji wa madini haya wakati huohuo ukiwa unapunguza ulaji wa madini ya sodium (chumvi hii tunayotumia) husaidia katika kuulinda moyo dhidi ya maradhi hatari kama shambulio la moyo, presha na kiharusi (stroke).

 

Ndani ya papai kuna madini ya Choline, haya ni muhimu katika kusaidia miili yetu hasa kulala, kujongea kwa misuli (kukunja na kukunjuka, kutanuka na kusinjaa). pia husaidia katika kulinda mpangiliuo wa utando wa seli, husaidia katika kutunza kumbukumbu pamoja na kujifunza yaani kusoma. Pia husaidia katika ufyonzwaji wa fati (mafuta).

 

Kwa ufupi papai lina matumizi mengi sana kama ukuaji wa nywele na kuzifanya zing’ae, kupona kwa vidonda, ukuaji wa tishu na ukuaji wa mwili kwa ujumla. Na haya yote ni kutokana na kuwepo kwa vitamin c na vitamin A

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 2132

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Habari ndugu naomba kuuliza eti mtu akipaliwa na asali anakufa?

Post hii inakwenda kukujulisha hatari za kupaliwa na asali ama kitu kingine kama muulizaji alivyouliza.

Soma Zaidi...
Faida za kula bamia

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida ambazo anaweza kupata mwanadamu Kama akila bamia Mara kwa mara. Bamia huliwa Kama tunda au Kama mboga pia na husaidia vitu vingi mwilini.

Soma Zaidi...
Dalili za ukosefu wa madini ya iodini (goiter)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za upungufu wa iodini ambapo kitaalamu hujulikana Kama goiter. Goiter Ni Sababu ya kawaida ya goiter duniani kote ni ukosefu wa iodini katika chakula. Nchini Marekani, ambako utumiaji wa chumvi yenye iodini ni j

Soma Zaidi...
Tufaha (apple)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula apple/tufaha

Soma Zaidi...
Faida za kitunguu thaumu mwilini

Makala hii itakuletea faida za kitunguu thaumu katika afyabyako.

Soma Zaidi...
Faida (matunda) ya kusimamisha swala katika jamii

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo baada ya kula

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula

Soma Zaidi...
Asili ya vyakula vya madini ya zinki

Post hii inahusu zaidi asili ya madini ya zinki, hii inaonesha sehemu gani tunaaweza kupata madini ya zinki.

Soma Zaidi...
Faida za kula uyoga

Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya

Soma Zaidi...