Vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo

Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo

VYAKULA HATARI NA VYAKULA SALAMA KWA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo ni moja kati ya maradhi yanayosumbuwa watu kutokana na kuchelewa kwake kupona hata baada ya kutumia dawa nyingi. Hali hii husababishwa kutokana na kutofata masharti ya vidonda vya tumbo vyema. Mgonjwa anatakiwa kufata masharti, ajuwa ni vyakula vipi atumie na vipi asitumie. Makala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

 

Pia makala hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo hutumuka kama dawa kwa ajili ya kutibu maradhi hususan vidonda vya tumbo. Mwisho wa makala hii utaweza kujifyunza ni kwa nini vidonda vingine haviponi, na vidonda sugu vinatokeaje.

 

Vyakula salama kwa wenye vidonda vya tumbo

1. Kabichi

2. Maepo

3. Karoti

4. Mboga za kijani

5. Asali

6. Kitunguu thaumu

 

Vyakula salama kwa vidonda vya tumbo pia ni dawa

1. Juisi ya kabichi

Kabihi ni katika mboga ambazo zina vitamini C. vitamini hii pia ni katika antioxidant ambayo husaidia katika kupambana na bakteria aina ya H.pylori ambao ndio chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo.

 

2. Asali

Asali nikatika baadhi ya vyakula ambavyo huhusishwa na matibabu mbalimbali. Asali husaidia kuimarisha afya ya moyo, pia hutumika kama dawa kwenye majeraha na majeraha ya moto ili kuzuia bakteria. Asali inaweza pia kupambana na bakteria wa kusababisha vidonda vya tumbo

 

3. Kitunguu thaumu.

ni katika viungo vya mboga kama kinavyotumika.lakini pia ni katika tiba za asili ambazo hutumiwa maeneo mengi duniani. Tafiti zinaonyesha kuwa katika kitunguu thaumu kuna chembechembe ambazo husaidia katika kupambana na bakteria aina ya H.pylori ambao ndio chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo.

 

4. Shubiri

Shubiri si katika vyakula ila hutumika sana katika viwanda vya vyakula, urembo na viwanda vya kutengeneza madawa. Shubiri ni katika tiba asili ambazo hutumiwa maeneo mbalimbali duniani. Tafiti zinaonyesha kuwa shubiri lina uwezo wa kuzuia mashambulizi ya bakteria kwenye ngozi. Pia shubiri limeonekana kuwa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.

 

Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo:

1. Maziwa.

Wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanatambuwa kuwa akinywa maziwa maumivu yanapunguwa. Hii ni faida, lakini tafiti zinaonyesha kuwa maziwa yanaongeza uzalishwaji na utaji wa tindikali za tumboni. Tindikali hizi zina mchango sana katika kusababisha vidonda vya tumbo

2. Pombe

Unywaji wa pombe unaweza kuathiri na kuharibu kuta za tumbo na utumbo. Hali hii inaweza kuongeza hatari ya kuweza kupata vidonda vya tumbo. Ama inaweza kusababisha hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

3. Kahawa;

Kahawa inaweza kusababisha kuongezeka kwa uzalishwaji wa tindikali za tumboni (stomach acid). tindikal hizi zikizalishwa kwa wingi tumboni zinaweza kuchubuwa ukuta wa tumbo na hatimaye kusababisha vidonda vya tumbo

4. Vyakula vyenye mafuta na fati kwa wingi.

5. Pilipili kali vyema kupunguza kuzitumia

6. Vyakula vyenye chumvi nyingi

7. Vyakula vya kuoka

8. Vyakula vyenye uchachu

9. Wacha kuvuta sigara

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 1510

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Kazi za madini ya Shaba mwilini.

Post hii inahusu zaidi madini ya Shaba mwilini,ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini, kama ifuatavyo

Soma Zaidi...
Vyakula vyenye vitamini C kwa wingi

Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya vyakula vyenye vitamini C kwa wingi

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za stafeli/soursop

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za stafeli ama soursop

Soma Zaidi...
Faida za juice ya tende.

Posti hii inahusu zaidi faida ya juice ya tende,ni juice inayotumiwa na watu wengi sana na wengine wanajua kabisa faida zake na kuna wengine hawajui wanaitumia kama mazoea tu, ila kuna ambao hawajui kabisa basi zifuatazo ni faida za juice ya tende kwa wal

Soma Zaidi...
Vinywaji salama kwa mwenye kisukari

Vijuwe vinywaji salama kwa mgonjwa wa kisukari

Soma Zaidi...