image

Vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo

Posti hii inahusu zaidi vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo, ni vyakula ambavyo upunguza makali kwenye uti wa Mgongo.

Vyakula anavyopaswa kutumia mwenye matatizo ya uti wa mgongo.

1.Mwenye matatizo ya uti wa mgongo wanapaswa kutumia vyakula vyenye magnesium Ili kufyonza calsiumu ambayo utokea kwenye mifupa, calcium kwenye mifupa ni nzuri Ila ikiwa nyingi usababisha maumivu makali kwenye uti wa mgongo,kwa kutumia vyakula vyenye wingi wa magnesium ambavyo ni mboga za majani, matunda nyama, maziwa hivi vyakula vinapunguza makali ya calcium kwenye mifupa.

 

2. Mgonjwa mwenye matatizo ya uti wa mgongo anapaswa kutumia vyakula vyenye wingi wa  vitamin D ambavyo vinaweza kufyonza calsiumu kwenye mwili na kufanya mifupa iweze kutanuka vizuri bila shida vyakula vyenyewe ni kama vile samaki, mayai, nyama hasa main,maziwa na cheese hivi vyakula vyote vina wingi wa vitamin D ambavyo vina uwezo wa kufyonza calcium kwenye mifupa.

 

3. Mwenye tatizo la uti wa mgongo anapaswa kutumia vyakula vyenye wingi wa vitamin E vyakula hivi vina kazi ya  kulegeza mifupa kama inakuwa imebana na kusababisha maumivu kwenye uti wa mgongo, kwa kutumia vyakula vyenye wingi wa vitamin E kama vile  mboga mboga za majani, maharage,njugu Mawe na kunde usababisha faida kubwa kwenye mwili na kusababisha mifupa kulegea na kuwa kawaida na mifupa ulegea na maumivu kwenye uti wa mgongo upungua.

 

4. Mwenye matatizo ya uti wa mgongo anapaswa kutumia vyakula vyenye wingi wa vitamin C maana vyakula vyenye wingi wa vitamin C upunguza  maambukizi kwenye uti wa mgongo,kama Kuna maambukizi yoyote utoka na na maumivu upungua kwenye uti wa mgongo, vyakula vyenyewe ni kama ifuatavyo kama vile matunda,mboga za majani, ndizi, madini, maziwa, viazi, mahindi ambayo hatyajakomaa, na vyakula vyote vya mbegumbegu usaidia kupunguza maambukizi kwenye mifupa.

 

5. Mwenye matatizo ya uti wa mgongo anapaswa kutumia sana vyakula vyenye protini kwa wingi Ili kuweza kujenga upya mifupa iliyohsribika au iliyokosa nguvu, tunajua kuwa kazi za protini kwenye mwili ni kujenga upya mifupa na vitu vilivyoharibika kwenye mwilini , vyakula vya protein ni kama vile  nyama , mayai na baadhi ya wadudu kama vile senene na kumbikumbi wanakuwa na protini nyingi kwa kutumia vyakula vyenye wingi wa protein  mifupa uweza kuimarika kwa kiwango fulani, kwa hiyo tunapaswa kutumia vyakula vyenye wingi wa protein kwa wingi.

 

6. Mwenye tatizo la uti wa mgongo anapaswa kutumia mafuta ya lotion yanayokutwa ( hot lotion ) mafuta haya yana Tabia ya kuondoa maumivu makali kwenye uti wa mgongo na hasa mwilini  na pia kutumia sana mafuta Aina ya Aloevero nayo pia upunguza mafuta mwilini, kwa kufanya hivyo maumivu yanaweza kuisha kwenye mwili baada ya kutumia mafuta ya Aina hii.

 

7, pamoja na kutumia vyakula mbalimbali mwenye matatizo ya uti wa mgongo anapaswa kuacha mawazo mengi hii usababisha kupunguza madini mwilini kwa hiyo stress uharibu afya ya mtu kwa hiyo amani ni kitu Cha muhimu kwa wenye matatizo ya uti wa mgongo.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2629


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Vyakula vya vitamin C
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin C Soma Zaidi...

Nini maana ya protini
Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa Soma Zaidi...

Faida za kula nanasi
Somo hili linakwenda kukuletea za kula nanasi na umuhimu wake kiafya Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamini na faida zake
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamini na faida zake Soma Zaidi...

Upungufu wa protini na dalili zake
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu upungufu wa protini na dalili zake Soma Zaidi...

Sababu za kuwa na fangasi ukeni
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwa na fangasi ukeni, ni vitu ambavyo usababisha fangasi ukeni kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Faida za kula papai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula papai Soma Zaidi...

Kazi za protini mwilini ni zipi?
Virutubisho vya protini vina kazi nyingi mwilini. Zifuatazo ndio kazi protini mwilini Soma Zaidi...

Faida za kiafya za peaz/ peas
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula peazi Soma Zaidi...

Matunda yenye vitamini C kwa wingi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matunda yenye vitamin C kwa wingi Soma Zaidi...

Faida za limao au ndimu
Post hii itakwenda kukueleza umuhimu wa limao kiafya Soma Zaidi...

Vyakula vya wanga na faida zake
Soma Zaidi...