Vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
- Vita vya Badri.
- Vilikuwa ndio vita vya kwanza vya jihad vilivyopiganwa siku ya Ijumaa mwezi 17 Ramadhani, mwaka wa 2 A.H (624 A.D) katika bonde la Badri.
- Chanzo cha vita ni kuwa mtume (s.a.w) alikusudia kuuzuia msafara wa Maquraish wa Makkah uliotokea Syria (Sham) uliosheheni bidhaa zenye thamani ya dinar 50,000 kwa ajili ya maandalizi ya kuupiga vita Uislamu na Waislamu.
- Mtume (s.a.w) alikuwa na askari 313, ngamia 70 na farasi 2 tu na Makafiri wa Kiquraish wakiwa askari 1000 waliojizatiti kivita, ngamia 700 na farasi 300.
- Waislamu walipata ushindi kwa waliuawa Maqurish 70 wengi wao wakiwa vigogo wa Makkah na waislamu 14 tu waliuawa.
Rejea Qur’an (3:123-124), (8:9-11), (54:45), (8:65), (8:17) na (8:48).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...