image

HISTORIA YA BANI ISRAIL

Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.

HISTORIA YA BANI ISRAIL

HISTORIA YA BANI ISRAIL

Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina. Nchi hii imeitwa takatifu kwa sababu ilikuwa nchi iliyo kaliwa na Mitume watukufu, Ibrahim(a.s),Is-haq(a.s) na Ya‘aquub(a.s). Palestina pamoja na kuwa nchi iliyokaliwa na Mitume maarufu kama hao, watu waliofuatia baadaye waliacha mafunzo yao na kuanzisha mifumo ya maisha ya kishirikina. Hivyo Bani Israil walitakiwa warudi nchini mwao wakautawalishe Uislamu juu ya mfumo ya kishirikina uliokuwemo mle.



Kutoka Misr walienda hadi Mlima Sinai. Hapa walikaa kwa muda wa mwaka mmoja ambapo Nabii Musa(a.s) alishushiwa karibu hukumu zote za Taurat.


Musa(a.s) Kupewa Taurati


Musa(a.s) aliitwa na Allah(s.w) katika Mlima Sinai ili apewe sharia kwa ajili ya wana wa Israili. Siku arubaini ziliteuliwa ili Mtume aweze kujiandaa mwenyewe kwa kufunga na kuswali kwa ajili ya kazi ngumu inayomsubiri ya kuwaongoza Bani Israil wakasimamishe ufalme wa Allah(s.w) katika nchi ya Palestina. Wakati huu Mtume Musa aliwaacha Bani Israil (Mayahudi) katika sehemu ambayo sasa huitwa Wadiy-Shaikh ambayo ipo kati ya Nubi Salih na Mlima Sinai. Mlima Sinai una urefu wa futi 7,359 toka usawa wa bahari na mara nyingi huwa umefunikwa na mawingu. Kileleni mwa mlima huu lipo pango ambapo Nabii Musa (a.s) alikaa siku arobaini. Leo hii karibu na pango hilo pana msikiti na kanisa.



Habari ya kuitwa Musa katika Mlima Sinai inatajwa katika aya zifuatazo:

Na tulimuahidi Musa siku thalathini (afanye ibada, kisha tumpe Taurati) na tukazitimiza kwa kumi ikatimia miadi ya Mola wake siku arubaini. Na Musa akamwambia ndugu yake Haruni: "Shika mahali pangu katika (kuwaangalia) watu wangu na utengeneze wala usifuate njia ya waharibifu" (7:142).

Kama aya inavyobainisha, ilipotimia miadi Musa alikwenda kupokeasheria.



Akasema (Mwenyezi Mungu): "Ewe Musa! Mimi nimekuchagua juu ya watu wote kwa ujumbe wangu na kusema nawe kwangu. Basi pokea haya niliyokupa, na uwe miongoni mwa wanaoshukuru". "Na tulimwandikia katika mbao kila kitu - mawaidha (ya kila namna) na maelezo ya kila jambo. "Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu wako wayashike vema haya. Karibuni nitakuonyesheni miji ya wavunjao amri (zetu namna ilivyoharibika)" (7:144-145).



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 737


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
Soma Zaidi...

Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII IBRAHIIM(A.S) NA KUANDALIWA KWAKE:
Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...

Mikataba ya aqabah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME DAUD(A.S).
Nabii Daudi(a. Soma Zaidi...

UTARATIBU WA KULEA MIMBA
Soma Zaidi...

Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi
Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri. Soma Zaidi...

Mapambano Dhidi ya Maadui wa Dola ya Kiislamu
1. Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Kuulingania Uislamu kwa Jamii Yake
Nabii Ibrahim(a. Soma Zaidi...

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Katika Mji wa Taif
Baada tu ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hadhi na haki za Mwanamke Ulaya Wakati wa mapinduzi ya viwnda
Soma Zaidi...