Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Rejea Kitabu cha 3, EDK – Shule za Sekondari; Uk. 250 - 352.
- Walivamia mji wa Madinah na kupora mifugo na kuipeleka Makkah.
- Walimwandikia barua kwa kiongozi wa wanafiki Abdullah bin Ubayyi kumtaka wamfukuze Mtume (s.a.w) kutoka mji wa Madinah.
- Kuwatishia vita makabila yaliyokuwa yakiishi kati ya Makkah na Madinah yawe dhidi ya Uislamu na wasijekusilimu.
- Walichoma moto mashamba ya mitende ya waislamu Madinah.
- Walimchoma mkuki Zainabu bint Muhammad (s.a.w) wakati akielekea Madinah.
- Walikuwa wanatoa nyudhuru za uongo kuepuka jukumu la kupigana jihadi.
- Walimzulia uzinifu mke wa Mtume (s.a.w) Aisha (r.a) kuwa amezini na sahaba Safwan (r.a) wakati wa kurudi msafara wa Banu Mustaliq.
- Walijenga msikiti wao kama kichaka cha kupiga vita Uislamu na kutaka kumuua Mtume (s.a.w).
- Walishirikiana na maadui wengine wa Uislamu ili kuupiga vita Uislamu.
- Walijitenga wanafiki 300 katika vita vya Uhudi na kuwaacha waislamu 700 Waliopambana na maadui wa Kiquraish 3,000 waliojizatiti kivita.
- Walichochea ugomvi baina ya Muhajirina na Answar na kutishia kumfukuza Mtume (s.a.w) Madinah wakiongozwa na Abdullah bin Ubayyi katika msafara wa vita vya Banu Mustaliq.
- Walishirikiana na wanafiki katika kuwatia wasi wasi waislamu walipobadilishiwa Qibla kutoka Jerusalemu na kuelekea Al-Kaaba, Makkah.
- Walitangaza kuwa Mtume (s.a.w) ni mtume wa uongo.
- Waliifanyia Qur’an stihizai (mzaha).
Rejea Qur’an (2:245), (3:181).
- Wamjaribu Mtume (s.a.w) kwa kumuuliza maswali ya kubabaisha yasiyo na majibu ya dhahiri, kama vile:
- Kuwavunja moyo na kuwadhalilisha waislamu.
- Walishirikiana na Wanafiki kwa njama za kutaka kumuua Mtume (s.a.w) na kuuhilikisha Uislamu.
- Walivunja na kusaliti mikataba ya amani waliowekeana na Mtume (s.a.w).
- Walichochea fitina baina ya Answar kwa kuwakumbushia ugomvi wao wa zamani baina ya Aus na Khazraj.
Rejea Qur’an (3:100-101).
- Gavana, Shurahbil bin Amr Ghassaany wa Dola ya Kirumi alimuua mjumbe wa Mtume (s.a.w), Haarith Bin Umair Al-Az katika mji wa Muttah.
Rejea Qur’an (48:28).
- Mtume (s.a.w) alilishughulikia na kulitia adabu kila kabila la Kiarabu lililojaribu kuleta choko choko dhidi ya Dola ya Kiislamu.
- Makabila ya Taif ya Bani Thaqif na Bani Hawazin yaliyokuwa na nguvu kijeshi, Mtume (s.a.w) aliyasambaratisha katika vita vya Hunain akiwa na askari 12,000, baada ya Fat-h Makkah mwaka wa 8 A.H.
“Bila shaka Mwenyezi Mungu amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunayni (pia); ambapo wingi wenu ulikupandisheni kichwa, lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa dhiki juu yenu; ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkageuka mkarudi nyuma (mnakimbia). Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume Wake na juu ya walioamini. Na akateremsha majeshi (ya Malaika) ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru; na hayo ndiyo malipo ya makafiri.” (9:25-26).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
KIKAO CHAKALIWA KUJADILI HATMA YA MUHAMMAD KATIKA MJI WA MAKAHiki ni kikao kizito hakijapata kutokea toka muhammad katika ji wa maka.
Soma Zaidi...Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a.
Soma Zaidi...Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a.
Soma Zaidi...(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.
Soma Zaidi...Tukirejea Qurβan (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.
Soma Zaidi...(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s.
Soma Zaidi...