Sifa za waumini zilizotajwa katika Surat Ar-Raad (13:19-26)

Sifa za waumini zilizotajwa katika Surat Ar-Raad (13:19-26)

2. Sifa za waumini zilizotajwa katika Surat Ar-Raad (13:19-26)Katika suratur-Raad, sifa za waumini zimewasilishwa kama ifuatavyo:


Je, anayejua ya kwamba yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako ni haki (akayafuata, basi) ni kama aliyekipofu? Wenye akili ndio wanaozingatia." (13:19).(Nao ni hawa) ambao wametimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu wala hawavunji ahadi za (wanaadamu wenzao)." (13:20)


"Na ambao huyaunga aliyoamuru Mwenyezi Mungu yaungwe na humuogopa Mola wao, na huiogopa hisabu mbaya (itakayowapata wabaya huko Akhera). (13:21)


"Na ambao husubiri (wakastahimilia wenziwao) kwa kutaka radhi ya Mola wao na wakasimamisha swala na wakatoa katika vile Tulivyowapa wakavitoa kwa siri na dhahiri na wakayaondoa maovu kwa mema. Hao ndio watakaopata malipo (mema) ya nyumba (ya Akhera)." (13:22)


Mabustani ya milele watayaingia wao (pamoja) na waliofanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na kizazi chao. Na malaika watawaingilia katika kila mlango, (wanawaambia): Salaam alaykum (iwe amani juu yenu) kwa sababu mlisubiri. Basi ni mema yaliyoje matokeo ya nyumba (ya Akhera kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu)." (13:23-2 4)"Na wale waliovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu (na za wanaadamu wenzao) baada ya kuzifunga, na wakakata aliyoamuru Mwenyezi Mungu yaungwe, na wamefanya uharibifu katika nchi, hao ndio watakaopata laana, na watapata nyumba mbaya (ya akhera). (13:25)


"Mwenyezi Mungu hukunjua riziki kwa amtakaye na Huidhikisha (kwa Amtakaye). Na wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa mkabala wa akhera si kitu ila ni starehe ndogo tu." (13:26)Mafunzo:
Mwanzo mwa aya hizi, Allah (s.w) anavuta fikra zetu kwa kutuuliza swali kuwa, "Je, yule aliyeyakinisha kuwa Qur-an ni kitabu cha Allah (s.w) alichoshushiwa Mtume Muhammad (s.a.w) na akakifuata kikamuongoza katika maisha ya nuru (furaha na amani) ni sawa na yule aliyekataa kuongozwa na Qur-an na kuishi maisha ya giza (upofu)? Baada ya swali hili Allah (s.w) anahitimisha kuwa wenye akili ndio wanaozingatia. Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa wenye akili ni Waumini wenye sifa zifuatazo:(i)Wanaotimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu
Ahadi kuu ambayo sote binaadamu tumeichukua mbele ya Mola wetu ni ile ya kumuabudu yeye pekee kama anavyotukumbusha:"Na (kumbuka) Mola wako Alipowaleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao (akawaambia): "Je, Mimi siye Mola wenu?" Wakasema: "Ndiye; tunashuhudia (kuwa wewe ndiye Mola wetu)." (Akawaambia Mwenyezi Mungu): Msije mkasema siku ya Kiyama kuwa sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo (hatujui); au mkasema: "Baba zetu ndio walioshirikisha zamani, nasi tulikuwa kizazi nyuma yao, basi utatuangamiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya waovu?" (7:172-173)Wengi wa wafasiri wa Qur-an wanakubaliana kuwa ahadi hii ilichukuliwa na Adamu na mkewe Hawwah na roho zote za kizazi chao kabla hawajafika hapa duniani. Kwa hiyo kila nafsi ya mwanaadamu imechukua ahadi hii.Ahadi hii kuu pia tunaikariri katika shahada mara kwa mara kwamba tutamuabudu Allah (s.w) peke yake kwa kufuata mwongozo aliotuletea kupitia Qur-an na Sunnah ya Mtume wake Muhammad (s.a.w). Kila umma uliikariri shahada hii kupitia kwa Mtume wao. Hivyo binaadamu atakapoacha kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo atakuwa amevunja ahadi hii kuu aliyoitoa mbele ya Mola wake.(ii)Wanaotimiza ahadi wanazozitoa kwa binaadamu wenzao
Katika Qur-an tunahimizwa kutekeleza ahadi zote tunazozitoa kwa binaadamu wenzetu katika mambo ya kheri." Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itaulizwa.' (17:34)
Waumini hawafungiki na ahadi zinazovunja ahadi kuu. Bali tunalazimika kuvunja ahadi yoyote ile inayotupelekea kumuasi Allah (s.w) na Mitume wake. Qur-an inatupa dira juu ya mashirikiano na binaadamu wenzetu katika Qur-an:


"' Saidianeni katika wema na ucha-Mungu wala msisaidiane katika uovu na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu." (5:2)(iii) Wanaounga yale aliyoamuru Mwenyezi Mungu yaungwe.
Kuunga yale aliyoamuru Mwenyezi Mungu ni kuufuata Uislamu vilivyo katika kila kipengele cha maisha ikiwa ni pamoja na kuwafanyia wema wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, jirani na binaadamu wote kwa ujumla. Kuwa na huruma kwa maskini, yatima na wote wenye shida. Kuwa mkarimu kwa ujumla na kuwa mstari wa mbele katika kujenga mahusiano mema na watu kwa kuzingatia kanuni na misingi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.(iv)Wanaomuogopa Mwenyezi Mungu na kuiogopa Hisabu mbaya huko akhera
Kumuogopa Mwenyezi Mungu ni kuogopa kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu. Kwani kila atakayekasirikiwa na Allah (s.w) atastahiki kupata adhabu yake ambayo ni kali isiyo na mfano wake:


"Basi siku hiyo hataadhibu yoyote namna ya kuadhibu kwake (Mwenyezi Mungu). Wala hatafunga yoyote jinsi ya Kufunga kwake (Mwenyezi Mungu)." (89:25-26)
Kumuogopa Mwenyezi Mungu kiutendaji ni kujitahidi kufanya mema au yale yote aliyoamrisha Allah (s.w) kwa kutarajia kupata radhi yake na kujitahidi kuacha yale yote aliyoyakataza kwa kuhofia kughadhibikiwa na yeye.(v)Wanaosubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao Wanaosubiri kwa ajili ya kupata radhi za Allah (s.w) ni wale:
(a)Wanaofanya wema na kudumu mpaka mwisho wa maisha yao.
(b)Wanaojiepusha na maovu na kudumu katika kujiweka mbali na maovu mpaka mwisho wa maisha yao.
(c)Wanaostahimili juu ya misuko suko mbali mbali inayowafika katika maisha ya kila siku na wakawa ni wenye kumtegemeaAllah (s.w).
(d)Wanaostahamili maudhi wanayofanyiwa na bianaadamu wenzao katika mchakato wa maisha ya kila siku.
(e)Wasiotoa maamuzi haraka haraka bila kuyapima vya kutosha katika kuendea mambo yao.
(f)Wasiotarajia kupata haraka haraka matunda ya Harakati za kusimamaisha Uislamu katika jamii. Suala la kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii na kuuhami usiangushwe ni suala la kufanywa kwa uhai wote wa maisha ya muumini. Allah (s.w) anawabashiria malipo makubwa wenye kusubiri kuwa:


"Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema; na ndio wenye kuongoka." (2:15 7)


(vi)Wanaosimamisha Swala
Kusimamisha swala ni kudumu katika kuswali swala zote kama alivyozitekeleza Mtume (s.w) kuanzia kwenye faradhi ya Qiyamullailiy (Tahajjud), swala tano za faradh na swala nyingine zote za Sunnah kwa kufuata barabara masharti yake, nguzo zake na kuwa na khushui wakati wa kutekeleza swala hizi. Kiutendaji swala itakuwa imesimama pale itakapomwezesha mwenye kuswali kuepukana na mambo maovu na machafu na kumwezesha kufanya jitihadi za makusudi za kuondoa maofu na machafu katika jamii.(vii)Wanaotoa katika vile alivyowapa Mwenyezi Mungu
Kila tulichonacho ikiwa ni pamoja na mali na neema mbali mbali zilizotuzunguka pamoja na vipawa mbali mbali tulivyonavyo, ikiwa nguvu, siha nzuri, elimu, fikra, n.k. ameturukuzu Allah (s.w). Muumini anatakiwa avitumie vitu hivi kwa ajili ya kujinufaisha yeye na wale wanaomtegemea kwa mahitaji ya lazima na ziada aitoe kwa ajili ya kusimamisha dini ya Allah (s.w) na kuwasaidia binaadamu wenzake wanaohitajia msaada kwa kutarajia malipo kutoka kwa Allah (s.w).(viii)Wanaoondoa maovu kwa wema
Kuondoa maovu kwa wema kuna maana mbili;
(a)Baada ya mtu kufanya maovu, hurejea haraka haraka kwa Mola wake kwa kuleta toba ya kweli; kisha kuzidisha kufanya wema kwa kuleta dhikri nyingi, kuzidisha kufunga, kutoa sadaqa, n.k.:


"Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kweli kweli kwa Mwenyezi Mungu." (25:71)(b)Baada ya mtu kufanyiwa uovu au kuudhiwa na mtu mwingine, huzuia hasira na kuwa mwepesi wa kumpa aliye mnyima, kumsamehe aliyemkosea, kumchangamkia aliyemnunia, kumrudishia maneno mazuri aliyemtukana, n.k. Hekima ya kujipamba na sifa hii inabainishwa katika aya ifuatayo:


"Mambo mabaya na mazuri hayawi sawa. Ondosha ubaya unaofanyiwa kwa wema, tahamaki yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui atakuwa kama ni jamaa (yako) mwenye kukufia uchungu". (41:34)Mwisho, baada ya kufahamishwa hizi sifa za waumini zilizoorodheshwa, tunafahamishwa malipo watakayostahiki kuyapata katika nyumba ya Akhera ambayo ni kuishi Peponi milele pamoja na wazee wao na watoto wao ambao nao walijipamba na sifa hizi za waumini.
                   
Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 133


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

DUA 32 - 40
32. Soma Zaidi...

MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...

Neema Alizotunukiwa Nabii Daudi(a.s)
Soma Zaidi...

KUAMINI SIKU YA MALIPO
Soma Zaidi...

kuwa muaminifu na kuchunga Amana
Uaminifu ni uchungaji wa amana. Soma Zaidi...

Khalifa na Uendeshaji wa Dola kwa ujumla, kulinda wasio waislamu na haki zao na mali zao.
Soma Zaidi...

NAMNA AMBAZO DUA HUJIBIWA
NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA. Soma Zaidi...

Maryam Apewa Habari ya Kumzaa Isa(a.s)
Baada ya maandalizi hayo ya kimalezi pamoja na hifadhi ya Allah(s. Soma Zaidi...

Ni mambo gani yanaharibu na kutengua udhu?
Soma Zaidi...

Hii ndio namna ya kuswali kama alivyoswali Mtume s.a.w
Mtume (s. Soma Zaidi...

Taratibu za mahari katika uislamu
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII AYUBU
Soma Zaidi...