Mafunzo kutokana na vita vya badri

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Mafunzo kutokana na Vita vya Badri.

  1. Ushindi wa waislamu katika vita unatoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na sio kutokana na ubora wa silaha na wingi wa askari.

Rejea Qur’an (3:123-124), (8:42-45).

 

  1. Tunajifunza pia namna ya kuwafanyia mateka wa kivita ikiwa ni pamoja na;

-  Kuwapatia haki na huduma zote msingi za kimaisha, kibinaadamu na kiutu.

-  Kuwalea na kuwafanyia wema na uadilifu kama wanafamilia wengine.

-  Kwa mateka wanaoweza kuleta madhara kwa waislamu na Uislamu, ni bora 

    kuuawa badala ya kuachwa huru kwa kujikomboa.

    Rejea Qur’an (8:67-69).

 

  1. Mwenyezi Mungu (s.w) aliwaadhibu makafiri na kuwanusuru waislamu katika vita vya Badri na hawakuadhibu walipokuwa Makkah kwa sababu walikuwa pamoja na Mtume (s.a.w) na pia walipewa muda wa kutubia.

Rejea Qur’an (8:32-34) na (8:19).

 

  1. Tunajifunza pia, inafaa nguvu ya kivita kutumika ikibidi katika kuzuia na kuondoa uovu, udhalimu, uonevu na choko choko za maadui.

Rejea Qur’an (8:60) na (60:8-9).

 

  1. Tunajifunza pia, Uislamu bila ya juhudi za kweli kufanyika na kumwagika damu na kujitoa muhanga ipasavyo, hautasimama katika jamii.

 

  1. Choko choko na mbinu za maadui dhidi ya Uislamu na waislamu ni zenye kuendelea na hazitaisha kamwe hadi siku ya Qiyama.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1674

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana: