Nabii Yunus(a.
Nabii Yunus(a.s) ni miongoni mwa Mitume wa Allah(s.w) waliotajwa katika Qur-an. Yunus(a.s) ametajwa katika Qur-an kwa majina matatu:
(i) “Yunus” (37:139) Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.
(ii) “Dhun-Nun”
Na (Mtaje) Dhun-Nun (Yunusi) alipoondoka hali amechukiwa, na akadhani ya kwamba hatutamdhikisha. Basi (alipozongwa) aliita katika giza (akasema): Hakuna aabudiwaye isipokuwa Wewe, Mtakatifu “Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu (nafsi zao).” (21:87)
(iii) “Sahibul-Hut” (Mmezwa na Chewa)
Basi subiri kwa hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama mmezwa na Chewa (Yunusi). (Kumbuka) alipolingana, (alipomwita Mwenyezi Mungu), na hali ya kuwa amezongwa (barabara).(68:48)
Majina ya “Dhun-Nun” na “Sahibul-Hut” yana maana ya “Mwenye kumezwa na samaki (chewa).” Nabii Yunus (a.s) ameitwa majina hayo mawili kutokana na historia ya maisha yake ya Da’awah iliyompelekea mpaka akamezwa na samaki mkubwa (chewa) kisha akatapikwa ufukoni akiwa hai kwa uwezo wa Allah(s.w).
Umeionaje Makala hii.. ?
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 8. Hapa utajifunza malezi ya Mtume kutokakwa Halimavkuja kwa mama yake.
Soma Zaidi...Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyewawezesha Mitume na Manabii kufanya miujiza.
Soma Zaidi...Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a.
Soma Zaidi...Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a.
Soma Zaidi...Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 17. Historia ya Bi Khadija na familia yake.
Soma Zaidi...