Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kuchaguliwa na kufuatwa kama muongozo sahihi wa maisha na watu wote kwa sababu zifuatazo;
Uislamu unaeleza lengo la kuumbwa mwanaadamu kuwa ni ibada na kumtumikia Mwenyezi Mungu na kuwa msimamizi wa sheria na hukumu zake hapa ulimwenguni ili kupata radhi zake.
Rejea Qur’an (51:56) na (2:29).
Uislamu ndiyo dini pekee inaenda na kuzingatia kanuni na taratibu zote za kimaumbile za kibailojia kifizikia na kikemia ya viumbe vyote vilivyo na visivyo hai ikiwa ni pamoja na maumbile au mazingira yanayotuzunguka.
Rejea Qur’an (3:83) na (30:30).
Uislamu ni dini inayotoa muongozo namna ya mtu kumiliki hisia zake na kuendea mambo katika hali tofauti tofauti kama vile wakati wa furaha, shida, huzuni, misiba, n.k.
Rejea Qur’an (2:155-157).
Ni Uislamu pekee ndio mfumo kamili wa maisha ya kila siku ya mwanaadamu katika fani na nyanja zote za kibinafsi na kijamii kama vile kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
Uislamu umeweka muongozo katika kumuadilisha mwanaadamu kupitia ibada maalum kama vile swala, funga, hija, kutoa zakat na sadaqat na zinginezo za sunnah.
Uislamu umekuwa ni mwongozo wa maisha tangu binaadamu wa kwanza hadi wa mwisho katika Nyanja zote za maisha bila kujali taifa, ukoo, rangi na hadhi ya watu.
Rejea Qur’an (42:13).
Ni dini ya Uislamu ndiyo inayotoa na kusimamia kwa usawa na uadilifu haki, hukumu na adhabu zote kwa watu wote bila ya upendeleo na ubaguzi wa rangi, taifa, hadhi na ukoo.
Rejea Qur’an (103:1-3), (9:33), (61:9) na (17:105).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Historia na sura ya Mtume Muhammad, sehemu ya 10.
Soma Zaidi...Kama ilivyokuwa katika kaumu zilizotangulia, waliomuamini Shu’ayb(a.
Soma Zaidi...Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.
Soma Zaidi...KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.
Soma Zaidi...HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...