Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Zakaria(a.s) na Yahya(a.s)

Kutokana na Historia ya Nabii Zakaria (a.s) na Yahya (a.s)
tunajifunza yafuatayo:

(i) Tuwe makini katika kulea watoto wetu hasa mabinti – Binti akileleka vizuri atakuwa ni chimbuko la malezi bora katika jamii.(ii) Tusichoke kumuomba Allah(s.w) jambo lolote la msingi tunalohitajia kwa ajili ya kusimamisha Uislamu na kuendeleza wema katika jamii – Hapana linaloshindikana kwa Allah(s.w).(iii) Waumini wanaharakati wa kusimamisha Uislamu katika jamii, waombe watoto wema watakaorithi harakati za Kiislamu na kuziendeleza kwa ari na hima zaidi.(iv) Ili watoto wetu waweze kuwa wanaharakati wazuri, hatunabudi sisi wenyewe kuwa mfano mwema wa kuigwa kama alivyokuwa mzee Zakaria(a.s) na kisha tuwafunz kwa kina elimu sahini ya Uislamu inayotokana na Qur-an na Sunnah na tuwape kwa upana elimu ya mazingira.(v) toto anayependeka mbele ya Allah(s.w) ni yule anayewafanyia wema wazazi wake kisha kuifanyia wema jamii. Mtu hawezi kuwa mwema kwa jamii yake endapo ameshindwa kuwatendea wema wazazi wake waliomzaa na kumlea kwa taabu.(vi) Kila mtoto anazaliwa katika amani, (katika Uislamu). Atabakia kuwa katika amani mpaka kufa kwake
na kufufuliwa kwake endapo tutamlea Kiislamu naye akaendelea kubakia kuwa Muislamu mtendaji mwenye kufanya jitihada za makusudi za kusimamisha Uislamu katika jamii baada ya baleghe yake mpaka kufa kwake.