image

Kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu

Kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu

Kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu

a) Wakati wa Ukhalifa wa Uthman bin Affan (r.a)

- Dola ya Kiislamu ilianza kuporomoka nusu ya pili ya uongozi wa Khalifah, Uthman bin Affan (r.a).
- Wanafiki wakiongozwa na Abdullah bin Sabaa, walizua fitna na kumtuhumu kiongozi wa Dola na kuanzisha imani na itikadi potofu.
- Wapinzani wa Dola ya Kiislamu walijiimarisha na kutuma wajumbe watatu kutoka Misri, Basra na Kufa kwa Khalifa kuwasilisha malalamiko yao.
- Wajumbe hao walirejesha fitina kwao kuwa ujumbe wao umepuuzwa na Khalifa, hivyo wakaandaa jeshi la askari 1000 ili kuangusha utawala wa Uthman (r.a).
- Wakazi wa Madina walipambana na waasi hao lakini walizidiwa nguvu na

hatimaye kuingia hadi Msikitini na kumuua Khalifa akiwa anasoma Qur’an.



b) Wakati wa Khalifa Ali bin Abi Taalib (r.a)

- Baada ya kuuliwa Uthman (r.a), wapinzani walishikilia mji wa Madina kwa siku sita na kuongoza wao na siku ya 6 walimtangaza Ali (r.a) kuwa ndiye Khalifa.
- Uchaguzi huu wa Ali (r.a) haukukubalika kwa Waislamu, na kuwagawa waislamu makundi manne.
i. Vita kati ya Bi Aisha (r.a) na Khalifa Ali (r.a), Vita vya Jamal (Ngamia)

- Bi Aisha (r.a) waliungana na Talha na Zubair (r.a) na kuandaa jeshi la kulipiza kisasi cha kuuliwa Uthman (r.a).
- Ali (r.a) walifanya sulhu na Bi Aisha pamoja na Mua’wiya (r.a) kwa kuafikiana kuwa Khalifa Ali (r.a) atawaadhibu wauaji wa Uthman (r.a) Dola ikiwa na amani.
- Mpinzani mkubwa, Abdullah bin Sabaa na jeshi lake walivuruga sulhu hiyo na vita vikapiganwa mji wa Basra na waislamu 10,000 walikufa.

ii.Vita kati ya Khalifa Ali (r.a) na Mua’wiya; Vita vya Sifin

- Wakati Ali anatawazishwa Ukhalifa, Mua’wiya alikuwa Gavana wa Syria, Khalifa Ali alimvua ugavana Mua’wiya lakini Mua’wiya alikataa.
- Khalifa Ali (r.a) aliandaa jeshi na kupigana na jeshi la Mua’wiya huko

Syria sehemu iitwayo Sifin mnamo mwaka 36 A.H.

- Musa Asha’r (r.a) kwa upande wa Khalifa walifanya sulhu na Amr bin Al- As (r.a) kwa upande wa Mua’wiya (r.a) lakini wauaji wa Uthman hawakutaka sulhu na kuamua kujitenga na kupambana na Khalifa Ali na Mua’wiya (r.a).
- Kundi hili lililojitenga na Khalifa Ali (r.a) liliitwa “Khawaarij”

(waliojitenga).



iii.Kuuliwa Khalifa Ali bin Abi Twalib (r.a)

- Khawaarij walipanga njama za kumuua Mua’wiya, Ali na Amr bin Al-As (r.a) aliyekuwa mshauri wa Mua’wiya (r.a) mwaka 40 A.H.ndani ya swala ya Alfajir.
- Muuaji wa Ali (r.a) alimjeruhi Ali vibaya kwa upanga wa sumu na hatimaye akafa siku ya 3 yake.
- Wauaji wa Mua’wiya na Amr (r.a) hawakufanikiwa kwani Mua’wiya na

Amr (r.a) hawakufika msikitini swala ile.

- Baada ya kuuliwa Ali bin Abi Twalib (r.a), mtoto wake Hassan alichaguliwa kushika nafasi ya Ukhalifa.
- Mua’wiya aliandaa jeshi na akapambana na Hassan (r.a) na mwishowe walikubaliana kuwa, Mua’wiya achukue Ukhalifa na baada ya kufa, uongozi utakuwa chini ya Hussein bin Ali (r.a).
- Kinyume na makubaliano, Mua’wiya kabla hajafa alimteua mtoto wake

Yazid kushika uongozi wa Dola baada yake.

- Dola ya Kiislamu iliyoasisiwa na Mtume (s.a.w) ikaporomoka na ufalme

ulioasisiwa na Mua’wiya ukachukua nafasi.



Mafunzo yatokanayo na kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu

i. Ni muhimu na wajibu kwa waislamu kuwa makini katika kuandaa na kuchaguzi viongozi wa Kiislamu kwa mujibu wa malengo yao.


ii. Maadui wa Uislamu hawatarudi nyuma kamwe katika kuupiga vita Uislamu na waislamu.


iii. Mgawanyiko wa kimakundi ndani ya umma wa Kiislamu ndiye ufa pekee unaopelekea kudhoofika Uislamu na waislamu.


iv. Kuwabaini wanafiki na maadui wa Uislamu na mbinu zao ni jambo la msingi mno katika kuendesha harakati za Kiislamu.


v. Waislamu watakapokuwa tayari kikweli kweli kuupigania Uislamu, Uislamu utachukua hatamu yake yak kuongoza maisha ya jamii.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1372


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Historia ya Luqman mtu aliyesifika kuwa na Hikma
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma. Soma Zaidi...

Historia ya Al-Khidhri
Jina Al-Khidhri halikutajwa mahali popote katika Qur’an. Soma Zaidi...

Historia ya Kuzuka Imani ya Kishia waliodai kuwa ni wafuasi wa Ally
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII IBRAHIIM(A.S) NA KUANDALIWA KWAKE:
Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...

Historia ya Vijana wa Pangoni
Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s. Soma Zaidi...

Wapinzani wa Ujumbe wa Nabii Salih(a.s)
Baada ya Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Bara arabu enzi za jahiliyyah, jiografia ya bara arabu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME DHUL-KIFL(A.S)
Mtume Dhul-kifl ananasibishwa na Ezekiel anayetajwa ndani ya Biblia. Soma Zaidi...

Kiapo ya Mtume Ayub na utekelezwaji wake
Mkewe Ayyuub(a. Soma Zaidi...

Juhudi za Waislamu Katika Kuhuisha Harakati za Kiislamu Zama za Nyerere hadi leo
i. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUT(A.S) NA WATU WA SODOMA NA GOMORA
Mtume Lut(a. Soma Zaidi...

Bara la Arabu Zama za Jahiliyyah
Wakati Mtume(s. Soma Zaidi...