Vita vya Al Fijar na sababu zake

Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar.

MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU).
Vita hivi ni vita vilivyotokea kati ya kabila la kiquraysh wakisaidiwa na Kinana kutokea makkah na kabila la Qays ‘Aylan kutokea taif. Na vita hivi vilitokea ndani ya miezi mitukufu na vilidumi kwa muda wa miaka mktano. Na mapigano halisi yalidumu kwa muda wa siku tano tu.

 

Vita hivi vimeitwa vita vya uovu kwani vilifanyika ndani ya miezi mitukufu. Vilitokea vita hivi wakati Mtume alipokuwa na miaka kumi na tano. Na alishiriki katika vita hivi. Ijapokuwa Mtume hakupenda kushiriki vita hivi alifanikiwa kutokushiriki ndani ya siku 2 za kwanza lakini siku tatu zilizofata ilibidi ashiriki. Hakuwahi kunyanyua upanga kwa ajili ya kupigana ila alishiriki katika kuokota misahare na kuwapatia wapiganaji.



Inasemekana katika mwezi wa dhul-qada (mfunguo ilikuwa ni ada ya waarabu enzi hizo kufanya sherehe katika sehemu iitwayo Ukaz. Katika sehemu hii ndani ya masiku haya michezo mbalimbali ilifanyika kama kamari, mashindano ya kuchezea panga, kushindana kuimba mashairi, wanawake kucheza na mengineyo mengi. Pia biashara zilikuwa zikifanyika katika eneo hili.

 

Sasa vita hivi vilitokea kwasababu ya sintofahamu iliyotokea kati ya watu wawili wafanyabiashara. Mmoja kutoka kwenye kabila la Quraysh (Makkah) na mwengine kutokea kabila la Qays ‘Aylan kutoke taif.



Sababu ni kuwa mtu mmoja kutoka katika kabila la Quraysh alikuwa na mteja, na ikatokea kuwa mfanyabiashara mwingine kutoka kabila la Qays “Aylan akawa anamfatilia mteja yuleyule. Basi ahapa ndipo pakazuka mgogoro na hatimaye Mtu kutoka kabira la quraysh akamuua yule wa kabila la Qays ‘Aylan.

 

Watu kutoka Taif wakaandaa jeshi kuja kulipa kisasi cha ndugu yao alouliwa bila ya sababu. Watu kutoka kabila la Quraysh wakaandaa jeshi nao kwa kulinda heshima ya kabila lao. Bila ya kujali mwezi mtukufu ambao ni haramu kumwaga damu au kupigana, na bila ya kujali sheria zao juu ya mtu aliuliwa kwa makusudi sheria inasemaje. Wakaamuwa kupigana vita kali sana.

 


Vita vilianza mwanzoni mwa siku na toka vinaanza ushindi ulikuwa ni kwa kabila la Qaysh ‘Aylan lakini ilipofika mida ya jioni meza ikabadilika na ushindi ukawa ni wa Quraysh. Harb bin Umayyah (Baba yake mdogo Mtume (s.a.w)) ndiye alokuwa kiongozi wa vita kwa upande wa Mqauraysh na wasaidizi wake. Mwishoni mwa siku ya tano viongozi wa pande zote walikubali kuacha kupigana na wakaamuwa kufanya majadiliano ya amani kumaliza vita na hapa wakawekeana mkabata (maakubaliano) ulofahamika kwa jina la Al-Fudhul.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 2359

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    πŸ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰4 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰5 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Nasaba ya mtume

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Makubaliano ya Mkataba wa Al Fudhul

Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake.

Soma Zaidi...
tarekh 10

KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake.

Soma Zaidi...
Historia ya Dhulqarnain

Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: β€œMwenye Pembe Mbili”.

Soma Zaidi...
Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam

Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam.

Soma Zaidi...
Mbinu za Da’wah Alizotumia Nuhu(a.s)

Katika kufikisha ujumbe huu kwa watu wake Nuhu(a.

Soma Zaidi...