image

tarekh 01

NASABA YA MTUME (S.

NASABA YA MTUME (S.A.W)
Wanazuoni katika fani ya historia wamegawanya nasaba ya Mtume katiak makundi matatu. Kundi la kwanza ndilo linakubaliwa na kuwa ni usahihi kwa makubaliano ya wanazuoni wote na hili ni kundi linaloiangalia nasaba ya Mtume kutoka tangu kwa baba yake mpaka kufika kwa Mzee ‘Adnan. Kundi la pili lina shaka kwani hakuna makubaliano ya ujumla juu ya baadhi ya watu. Na kundi hili ni lile linaloangalia nasaba ya Mtume kutokea kwa mzee Adnan mpaka kufika kwa Mtume Ibrahimu (a.s). kundi la tatu lina shaka juu ya ukweli wake. Na hili ni lile kundi linaloangalia nasaba ya Mtume kutoka kwa Mtume Ibrahimu mpaka kufika kwa Mtume Adam (a.s).

1. Kundi la kwanza: Muhammad bin ‘Abdullah bin ‘Abdul-Muttalib (ambaye aliitwa Shaiba) bin Hashim, (aliitwa ‘Amr) bin ‘Abd Munaf (aliitwa Al-Mugheera) bin Qusai (pia aliitwa Zaid) bin Kilab bin Murra bin Ka‘b bin Lo’i bin Ghalib bin Fahr (ambaye aliitwa Quraish na kutoka kwa huyo ndipo tunapata kabila la Quraysh) bin Malik bin An-Nadr (pia aliitwa Qais) bin Kinana bin Khuzaiman bin Mudrikah (pia aliitwa ‘Amir) bin Elias bin Mudar bin Nizar bin Ma‘ad bin ‘Adnan.

1. Kundi la pili: ‘Adnan bin Add bin Humaisi‘ bin Salaman bin Aws bin Buz bin Qamwal bin Obai bin ‘Awwam bin Nashid bin Haza bin Bildas bin Yadlaf bin Tabikh bin Jahim bin Nahish bin Makhi bin Aid bin ‘Abqar bin ‘Ubaid bin Ad-Da‘a bin Hamdan bin Sanbir bin Yathrabi bin Yahzin bin Yalhan bin Ar‘awi bin Aid bin Deshan bin Aisar bin Afnad bin Aiham bin Muksar bin Nahith bin Zarih bin Sami bin Mazzi bin ‘Awda bin Aram bin Qaidar bin Ishmael mtoto wa Abraham (amani iwe juu yao).

1. Kundi la tatu: kuanzia kwa Nabii Ibrahim (amani iwe juu yake) , Ibn Tarih (Azar) bin Nahur bin Saru‘ bin Ra‘u bin Falikh bin Abir bin Shalikh bin Arfakhshad bin Sam bin Noah (amani iwe juu yake) , bin Lamik bin Mutwashlack bin Akhnukh [who was said to be Prophet Idris (Enoch) (amani iwe juu yake) bin Yarid bin Mahla’il bin Qabin Anusha bin Shith bin Adam (amani iwe juu yake)


                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 222


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Maana ya kusimamisha uislamu katika dini
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

MTUME MUHAMMAD (S.A.W)ANAKUTANA NA BAHIRA (MTAWA WA KIYAHUDI)
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Soma Zaidi...

Mjadala juu ya ndoa ya Mtume Muhammad s.a.w na bi Khadija.
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 16. Hapa utajifunza maandalizi wa mjadala wa ndoa hizi. Soma Zaidi...

Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.
Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi. Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Kuulingania Uislamu kwa Jamii Yake
Nabii Ibrahim(a. Soma Zaidi...

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija
Baada ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Kuibuka kwa kundi la khawarij baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)
Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a. Soma Zaidi...

Chokochoko na Upinzani wakati wa khalifa uthman khalifa wa Tatu
KUPOROMOKA KWA DOLA YA KIISLAMU ALIYOICHA MTUME(S. Soma Zaidi...

Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah
Baada ya mikataba miwili ya ‘Aqabah na baada ya Waislamu 75 kufika Yathrib salama, Mtume(s. Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 05
Soma Zaidi...

Kulingania watu wake na Miujiza Aliyoonyesha Nabii Isa(a.s)
Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyewawezesha Mitume na Manabii kufanya miujiza. Soma Zaidi...