Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake.
Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu na akamza kwa taabu. Na kubeba mimba yake hata kumwachisha ziwa; (uchache wake) ni miezi thelathini. Hata anapofikia baleghe yake na akawa mwenye umri wa miaka arubaini, (mtoto mwema) husema: "Ee Mola wangu! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na niwezeshe nifanye vitendo vizuri unavyovipenda, na unitengenezee watoto wangu; kwa yakini ninatubu kwako; na hakika mimi ni miongoni mwa waliosilimu (walionyenyekea)." (46:15).
Hao ndio tunaowakubalia vitendo vyao vyema walivyovifanya, na tunayapita kando makosa yao, (tunayasamehe); (watakuwa) miongoni mwa watu wa Peponi: miadi ya kweli waliyoahidiwa. (4 6:16).
Na ambaye anawaambia wazazi wake: "Kefule nyi! Oh! Mnanitishia kuwa nitafufuliwa; na hali karne nyingi, (watu wengi) zimekwisha pita kabla yangu (wala hazikufufuliwa)?" Na hao (wazee wake) wawili huomba msaada wa Mwenyezi Mungu; (na humwambia mtoto wao:) "Ole wako! Amin (haya unayoambiwa). Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli." Lakini yeye husema: "Hayakuwa haya (mnayoyasema) ila ni visa vya watu wa kale (tu si maneno ya kweli)."
Hao ndio ambao imelazimika hukumu juu yao (ya kutiwa Motoni, pamoja na mataifa yaliyopita kabla yao ya majini na watu, hakika hao ndio waliojitia khasarani. (46:17-18)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa:
(a)Hatunabudi kuwafanyia wema wazazi wawili na hasa mama ambaye anapata dhiki kubwa katika kutuzaa na kutunyonyesha mpaka kufikia umri wa miaka miwili.
(b)Hatunabudi kumshukuru Allah (s.w) kwa kutuneemesha kwa neema mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwapa wazazi wetu moyo wa huruma na mapenzi ya kutulea mpaka kufikia utu uzima.
(c)Pamoja na kumshukuru Allah (s.w), hatubabudi kuwashukuru wazazi wetu kwa kutulea kwa huruma na mapenzi. Shukrani zetu kwao tutazidhihirisha kwa kuwatii, kuwafanyia ihsani na kuwaombea dua na maghfira kwa Allah (s.w).
(d)Hatuna budi kujiepusha mbali na kuwafanyia wazazi wetu ufedhuli na jeuri. Tusisubutu hata kuwagunia.
(e)Hatunabudi kuomba kizazi chema na kumuomba Allah (s.w) atuwezeshe kukilea vyema kizazi chetu.
(f)Hatunabudi kufuatilia kwa makini usia mwema wanaotupa wazazi wetu.
(g)Hatunabudi kuleta toba na kuomba maghfira mara kwa mara (angalau kila siku mara mia moja).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download Now(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.
Soma Zaidi...Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B.
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 9.
Soma Zaidi...Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: “Mwenye Pembe Mbili”.
Soma Zaidi...Dola ya kiislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...