Mtume Lut(a.
Mtume Lut(a.s) ni mpwawe Ibrahiim(a.s) waliohama pamoja yeye kutokea Iraq. Lut(a.s) alitumwa kuulingania Uislamu katika miji miwili ya Sodoma na Gomora katika nchi ya Transjodan.
Tabia ya Watu wa Miji ya Sodoma na Gomora
Jamii aliyoikuta Mtume Lut(a.s) ilikuwa imeanguka sana kimaadili. Walifikia hali ya kuwa waovu zaidi ya wanyama licha ya kuwa maumbile yao yalikuwa ya binaadamu. Walizama kwenye kufanya maovu matatu mazito kama yanavyotajwa katika Qur-an:
Na (wakumbushe Nabii) Lut; alipowaambia watu wake: โBila shaka nyinyi mnafanya uovu (ambao) hakuna yoyote aliyekutangulieni kwa (uovu) huo katika walimwengu.(29:28)
โJe, mnawaendea wanaume, na mnawakatia njia (watu kwa kuwaua na kuwanyangโanya njiani) na mnafanya maovu katika mikusanyiko yenu?โ basi halikuwa jawabu ya watu wake ila kusema: โTuletee adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa umiongoni mwa wasemao kweli!โ (29:29)โ
Katika aya hizi tunafahamishwa kuwa watu wa jamii ya Lut (a.s) walikuwa wakifanya maovu mazito yafuatayo:
1) Walikuwa wakiwaendea wanaume wenzao katika kutosheleza matamanio yao ya ngono.
2) Walikuwa wakifanya uharamia na uporaji wa mali za watu.
3) Walikuwa wakifanya maovu haya hadharani na kwa ufahari.
Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao (wa maovu); wanahangaika ovyo. (15:72)
Je, jamii yetu hivi leo haifanyi haya na zaidi ya haya tena kwa ufahari. Hivi leo kuna mashindano ya U-miss ambayo wasichana vigoli hujitokeza jukwaani mbele ya hadhara ya watazamaji wanaume kwa wanawake wakiwa wamevaa viguo visivyo sitiri mwili. Hali ni hiyo hiyo kwenye kumbi za dansi, disko na hata kwenye sherehe za kiserikali. Na wengine wameenda mbele zaidi hata kufikia wanawake kusoma taarifa za habari katika television wakiwa uchi wa mnyama na kufikia wengine kucheza sinema za wanawake na wanaume wakifanya ngono hadharani.
Leo hii baadhi ya nchi za magharibi zimepitisha sheria yakuruhusu ndoa baina ya wanaume kwa wanaume wakifanya ushenzi ule ule wa mabaradhuli wa miji ya Sodoma na Gomora.
Umeionaje Makala hii.. ?
Yiomyokea khalid Ibn al walid katika vita vya Muta
Soma Zaidi...HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a.
Soma Zaidi...Mayahud Mwanzoni Mayahud walipoona kuwa Waislamu wanafunga siku ya Ashura pamoja nao na wanaelekea Qibla cha Baitul- Muqaddas pamoja nao hawakuonyesha chuki ya dhahiri dhidi ya Mtume(s.
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 8. Hapa utajifunza malezi ya Mtume kutokakwa Halimavkuja kwa mama yake.
Soma Zaidi...