Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Au
Haja ya kuhitaji mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Mwanaadamu pamoja na ujuzi na utundu alionao, hana uwezo wa kujiundia dini sahihi (mfumo sahihi wa maisha) utakaomfikisha na kumbakisha kwenye lengo la kuumbwa kwake. Na hii ni kutokana na sababu zifuatazo;
Pamoja na ujuzi, utambuzi na vipawa alivyopewa mwanaadamu, bado uamuzi na fikra zake ziaathiriwa na matashi ya nafsi yake katika upendeleo, uonevu na chuki, hivyo hawezi kuunda mfumo utakaosimamia haki na uadilifu.
Mwanaadamu hujielimisha kupitia nyenzo zifuatazo;
Kama vile pua, masikio, ulimi, macho, ngozi, n.k, ambavyo vyote vina udhaifu na mara nyingine hutoa taarifu zisizo na ukweli.
Uamuzi wa mwanaadamu wa akili na fikra peke yake hauwezi kutoa jibu/mwongozo sahihi wa maisha kwani huathiriwa na wakati, matashi, mazingira, uelewa, upeo wa kufikiri na pia una kikomo.
Rejea Qur’an (10:36,66), (25:43,45), (6:116) na (28:60)
Sayansi na majaribio haviwezi kutumika kama nyenzo kuu ya kuunda muongozo sahihi kwani vyote hivyo vinategemea milango ya fahamu ambayo nayo ina madhaifu mengi na kikomo pia.
Kutumia uzoefu wa kihistoria katika kuunda muongozo sahihi wa maisha ni dhaifu kwa sababu mwanaadamu huathiriwa na uzoefu na ujuzi wa awali na hivyo kutokubaliana na mabadiliko yeyote yatakayojitokeza.
Rejea Qur’an (2:170, 257), (5:104) na (6:116).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Tukirejea Qurβan (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.
Soma Zaidi...Nabii Ibrahiim na mkewe Sarah walikaa mpaka wakawa wazee bila ya kupata mtoto.
Soma Zaidi...Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri.
Soma Zaidi...(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s.
Soma Zaidi...Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Katika Suratul Yassin Allah(s.
Soma Zaidi...