Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.


Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.a.w). Makafiri hao walichimba mahandaki na ndani yake wakawasha moto mkubwa kisha wakawa wanawatosa waumini humo mmoja baada ya mwingine. Dhun-Nuwas mmoja



wa waliokuwa wafalme wa Mayahudi; aliingia Najran akiwa na jeshi kubwa ili awalazimishe watu wa Najran wasifuate mafundisho ya Mitume. Watu wa Najran walipokataa kumfuata, alichimba handaki kubwa akawasha moto akawa anamtumbukiza Muumini mmoja baada ya mwingine huku yeye na watu wake wanachekelea. Habari hii inaelezwa katika Suratul-Buruj, kama ifuatavyo:




“(Kuwa) wameangamizwa watu waliowaadhibu Waislamu katika mahandaki. Yenye moto wenye kuni (nyingi). Walipokuwa wamekaa hapo (Waliangamizwa makafiri hao pale wakati walipokuwa) wanatazama yale wanayowafanyia hao Waislamu (walipokuwa wakiwaadhibu). Nao hawajaona baya lolote kwao (Waislamu) ila kumuamini Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda (na) Mwenye kusifiwa. Ambaye ni Mwenye Ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona kila kitu” (85:4-9).



Kisa hiki kimesimuliwa kiwape fundisho na kuwaliwaza waumini wa zama zote; kwamba taabu iwapatayo kutoka kwa makafiri imeanza kuwafikia ndugu zao waliotangulia. Aidha, kutokana na kisa hiki Waislamu wanapata funzo kuwa kubakia na Imani Thabiti na suala la kusimamisha Uislamu katika jamii, kwahitaji juhudi na subira kubwa sana.

Mwenyezi Mungu anawaliwaza Waislamu kuwa makafiri wanaowatesa na kuwaghasi Waislamu hivi leo, atawaadhibu na kuwatesa kweli kweli kama alivyowatesa As-habul- Khudud.




“Hakika wale waliowaadhibu Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, kisha wasitubie basi watapata adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu ya kuungua (barabara)” (85:10). “Hakika kutesa kwa Mola wako ni kukali (sana)” (85:12).



Lakini pamoja na kuliwazwa huko; Waislamu hawatakiwi walale usingizi wasubiri nusura ya Mwenyezi Mungu. Ni wajibu wao wajiandae kwa kila mbinu kupambana na vitimvi vya maadui zao.



“Basi waandalieni (wawekeeni tayari) nguvu mziwezao (silaha), mafarasi yaliyofungwa tayari tayari ili kwazo muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu .................” (8:60).



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views: 2664

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 web hosting     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Ni jitihada gan alizo zifanya sayyidna othman katika kuihifadh qur an ?

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Jitihada alizozifanya Khalifa wa Tatu katika kuilinda Quran

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Adam(a.s)

(i) Utukufu wa mtu katika Uislamu hautokani na nasaba, rangi,kabila,utajiri ila uwajibikaji kwa Allah(s.

Soma Zaidi...
Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume

Uchaguzi wa ‘Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.

Soma Zaidi...
Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.

Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.

Soma Zaidi...