Sahihi al-Bukhari
Sahihi al-Bukhari ni kitabu cha Muhammad bin Isma'il Abu
'Abdallah al'Ju'fi anayejulikana kwa jina la "Imamu al-Bukhari." Alizaliwa 13 Shawwal, 194 A.H./21 Julai, 810 A.D. katika mji wa Bukhara huko Urusi, na alifariki 30 Ramadhan, 256 A.H./31 Agosti 870 .D.
Hamu yake ya kuhifadhi Hadith aliipata bado akiwa mtoto wa umri wa miaka kumi na moja. Alipofikia umri wa miaka kumi na sita alikwenda kuhiji Makka na kubakia humo humo kujifunza Hadith kwa wanazuoni mbali mbali. Baada ya kutoka Makka alikwenda Misr kisha Basra na sehemu nyingine za Asia ambapo alitembea huku na huko katika kujifunza na kukusanya Hadith kwa muda wa miaka kumi na sita.
Kazi yake ya miaka kumi na sita inaonekana katika kitabu chake mashuhuri kijulikanacho kwa jina la "Al-Jami'u al-Sahihi au Sahihi al-Bukhari".Kitabu hiki ndio kitabu cha kwanza cha Hadith kinachotemgemewa na Umma wa Waislamu baada ya Qur-an, kwa sababu ya uangalifu mkubwa uliochukuliwa na Imamu Bukhari katika ukusanyaji na uchambuaji wa Hadith zake. Jumla ya Hadith alizokusanya ni 600,000 na katika hizo alihifadhi Hadith 200,000. Lakini kutokana na uangalifu na tahadhari kubwa aliyoichukua katika kuhakiki usahihi wa Hadith alizozipokea, ni Hadith 7,275 tu zilizotokea katika kitabu cha Sahihi al-Bukhari. Kabla hajaikubali Hadith kuwa ni sahihi, ilibidi kwanza achunguze historia ya maisha ya kila mpokeaji wa Hadith hiyo kutokea kwa Mtume(s.a.w) mpaka kumfikia.
Imamu Bukhari amezipanga Hadith katika kitabu chake kufuatana na mada za fiq-h. Ameigawanya kazi yake katika juzuu tisini na saba na katika milango (sura) 3,450.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kutokana na Historia ya Nabii Ismail(a.
Soma Zaidi...Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B.
Soma Zaidi...KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba.
Soma Zaidi...Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...Tukio la kartasiTukio la βkartasiβ lililonakiliwa katika vitabu vya Muslim na Bukhari kuwa siku tatu kabla ya kutawafu Mtume (s.
Soma Zaidi...