Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.

Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi.

Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.

Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.


Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi. Siku hiyo ilitengwa iwe ya kufanya ibada tu. Hata hivyo

Mayahudi kidogo kidogo walianza kuivunja amri hii kwa ujanja ujanja na hatimaye wakaivunja kwa dhahiri. Basi Mwenyezi Mungu aliwaadhibu kwa kuwageuza kuwa Manyani.




'Na kwa yakini mmekwisha kujua (khabari za) wale walioasi miongoni mwenu katika (amri ya kuihishimu) Jumamosi. Basi tukwaambia: 'Kuweni manyani wadhalilifu'. Kwa hiyo tukaifanya (adhabu hiyo) kuwa onyo kwa wale waliokuwa katika zama zao na waliokuja nyuma yao, na (tukaifanya ni) mawaidha kwa wamchao Mwenyezi Mungu' (2:65:66).



Ni katika utaratibu wa Mwenyezi Mungu kuwapa watu mtihani ili kuwapambanua wale wanaotii kweli na wale wenye kuasi. Kwa hiyo amri ya kutokufanya kazi siku ya Jumamosi iliandamana na mtihani. Ulikuwako mji mmoja wa Kiyahudi ambao wakazi wake kazi yao kubwa ilikuwa uvuvi. Basi Mwenyezi Mungu aliwaletea mtihani. Ikawa ile siku ya Jumamosi waliyokatazwa kufanya kazi samaki walijaa na kuonekana wakichezacheza majini. Hali ikawa hivi siku zote za Jumamosi; lakini siku zingine ikawa taabu kuwapata samaki. Hali hii iliwashinda wengine kustahamili. Wakawa wanakwenda kuvua siku hiyo iliyokatazwa. Wale walioamini kweli kweli kitendo cha wenzao kuvunja amri ya Jumamosi kiliwashtua. Wakawaendea kuwanasihi na kuwakataza. Wapo waliotii amri ya kutokufanya kazi; lakini wasichukue juhudi yoyote kuwaonya wale waliovunja amri.



Basi ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu ya kuahdibiwa; walionusurika ni wale waliotii na wakawaonya wenzao. Wale ambao hawakuasi lakini hawakuwanasihi na kuwakataza wale waliovunja amri, waliadhibiwa pia. Habari hizi zinapatikana kwa urefu kaitka aya zifuatazo:



'Na waulizeni habari za mji ambao ulikuwa kando ya bahari (watu wa mji huo) walipokuwa wakivunja (sheria ya) Jumamosi (ambayo waliambiwa wasifanye kazi katika siku hiyo, wafanye ibada tu. Na kazi yao ilikuwa uvuvi). Samaki wao walipowajia juu juu siku za Jumamosi zao, na siku isiyokuwa Jumamosi hawakuwa wakiwajia (hivyo). Basi namna hivyo tuliwatia mtihani kwa sababu ya kuasi kwao' (7:163).



'Na (wakumbushe wakati) baadhi ya watu katika wao waliposema (kuwaonya waliovunja hishima ya Jumamosi kwa kuvua, na hali ya kuwa wamekataza, waliposema): 'Pana faida gani kuwaonya watu ambao Mwenyezi Mungu atawaua au atawaadhibu kwa adhabu kali (papa hapa)?' Wakasema: 'Tupate kuwa na udhuru mbele ya Mola wenu (kuwa tumeonya lakini hatukusikilizwa) na huenda wakaogopa' (7:164).




'Basi walipoyapuuza waliyokuwa wakikumbushwa, tuliwaokoa wale waliokuwa wakikataza maovu na tukawatesa wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa kuasi kwao' (7:165).



'Na walipotakabari wasiache waliyokatazwa, tuliwaambia: 'Kuweni manyani madhalilifu' (7:166).



Mafunzo yatokanayo na historia ya watu wa jumamosi:

Funzo la kwanza tunalopata kutokana na kisa hiki ni kufahamu falsafa na lengo la maisha ya mwanadamu. Tunafahamishwa katika Qur'an kuwa lengo la kuumbwa mwanadamu ni kumwabudu Allah(s.w).



'Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu' (51:56).

Pamoja na lengo hilo kuu tunafahamishwa kuwa mwanadamu amezungukwa na mitihani ya kila namna. Mitihani hii inadhihiri katika sura ya makatazo na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo kipindi cha uhai wetu wote ni kipindi cha mitihani kwetu:




Ametukuka yule ambaye mkononi mwake umo ufalme (wote). Naye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. Amabye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye Msamaha' (67:1-2).



Kwa kuzingatia lengo hilo mwanadamu anatakiwa ajichunge katika kuchuma kwake na mengineyo ayafanyayo katika kuendeleza maisha yake asitoke katika lengo kuu. Kama ni kuchuma na kutumia mali basi iwe ni kwa ajili ya kufikia lengo la kuumbwa kwake. Mtu asije kufanya kuchuma na kutumia ndio lengo lenyewe la maisha. Kwa hiyo hata kama ataona mahali pana chumo zuri kiasi gani hatalikimbilia endapo kufanya hivyo kutamtoa katika twaa ya Mwenyezi Mungu.



Jambo la msingi la kuzingatia ni kuwa maisha yamejaa vishawishi vingi sana. Watu waliovunja heshima ya siku ya Jumamosi walishindwa kuhimili kishawishi cha upatikanaji wa samaki. Leo sisi tumeamriwa inapaoadhiniwa Sala ya Ijumaa tuache shughuli zote tukimbilie kwenye Swala. Hapa panahitaji uangalifu. Yawezekana kwa mfanya biashara asubuhi yote ya siku ya Ijumaa asipate wateja. Inapokaribia saa sita mchana ndio wakaanza kumiminika. Bila kuwa makini katika hali kama hiyo mtu atafeli mtihani kama ilivyokuwa kwa wale walioshindwa kuhimili kuwaona samaki nje nje wasiwavue.



Funzo la pili na la msingi tunalopata ni kuwa suala la kuamrishana mema na kukatazana mabaya ni muhimu mno. Mtu pekee kuacha mabaya haitoshi. Ni wajibu juu yake pia awaelimishe na kuwahimiza wengine nao wafanye vitendo vizuri. Aidha ni muhimu afanye juhudi kuwaonya na kuwakataza wengine wasifanye maovu.



Katika aya ya 165 ya Sura ya 7 tuliyoinukuu hapo juu imebainishwa wazi kuwa waliookoloewa ni wale waliokuwa wakikataza maovu. Kwa hiyo pamoja na juhudi tunazofanya kuzitakasa nafsi zetu hapana budi juhudi hizo ziende sambamba na harakati za kuelimisha na kuwanasihi wengine. Na kufuzu kwa Muislamu kumeegemea kazi ya kuamrisha mema na kukataza maovu.





'Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri (Uislamu) na wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu. Na hao ndio watakaotengenekewa' (3:104).



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 227


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

zijue Nguzo za uislamu, imani, ihsani pamoja na dalili za qiyama
' ' ' ' ' ' ': " ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ?... Soma Zaidi...

Uchambuzi wa Neema Alizopewa Nabii Sulaiman(a.s)
(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake. Soma Zaidi...

Madai ya Makafiri Dhidi ya Qur'an na Udhaifu Wake
i. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)
Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a. Soma Zaidi...

Hukumu na taratibu za ndoa katika uislamu
Soma Zaidi...

Hadithi Ya 21: Sema Namuamini Allah Kisha Kuwa Mwenye Msimamo
Soma Zaidi...

hukumu na taratibu za biashara ya ushirika na hisa katika uislamu
Soma Zaidi...

Namna ya Kutayamam hatua kwa hatua, suna zake nguzo za kutayamam na masharti ya kutayamam
Soma Zaidi...

DUA ZA WAKATI WA SHIDA
DUA ZA WAKATI WA SHIDA 1. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MAISHA YA MTUME S.A.W KABLA YA UTUME
MAISHA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

(c)Vipawa vya Mwanaadamu
Vipawa vya mwanaadamu ni sababu nyingine inayomfanya mwanaadamu asiweze kuishi bila ya kufuata dini moja au nyingine. Soma Zaidi...

quran na sayansi
2; mbegu ya uhai uliyo changanyikaUmbile la mwanadamu limepitia hatua nyingi sana kama tutakavyoendelea mbele kuonalakini ukiachilia mbali na hatua zote alizopitia mwanadamu wakati wa kuumbwa lakiniumbile la mwanadamu bado limebakia kuwa dhalili kama ALLA Soma Zaidi...