Ibrahiim(a.s) Aomba Kupata Kizazi Chema

Nabii Ibrahiim na mkewe Sarah walikaa mpaka wakawa wazee bila ya kupata mtoto.

Ibrahiim(a.s) Aomba Kupata Kizazi Chema

Ibrahiim(a.s) Aomba Kupata Kizazi Chema


Nabii Ibrahiim na mkewe Sarah walikaa mpaka wakawa wazee bila ya kupata mtoto. Ibrahim(a.s) alinyoosha mikono ya maombi kwa Mola wake, kuomba watoto wema watakao msaidia katika harakati zake za kusimamisha Uislamu katika jamii. Aliomba:




โ€œEe Mola wangu! Nipe (mtoto awe) miongoni mwa watenda mema.โ€ Ndipo tukampa habari njema ya (kuwa atapata) mtoto mpole. (Basi akapata. Naye ndiye Nabii Ismaili). (37:100-101)



Aliamua kuoa mke wa pili, Hajirah, aliyekuwa mjakazi wa mkewe Sarah. Dua yake ilipokelewa na Hajirah akajifungua mtoto Ismail (a.s) akiwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim (a.s). Baadaye pia Allah(s.w) alimruzuku mtoto wa pili, Is-haqa, kutoka kwa Sarah, wote wawili wakiwa wazee vikongwe:

โ€œTena tukambashiria (kumzaa) Is-haqa. Nabii, miongoni mwa watu wema (kabisa)โ€ (37:112)




(Mkewe Ibrahiim akastaajabu) akasema: Ee mimi We! Nitazaa na hali mimi ni mkongwe, na huyu mume wangu ni mzee sana? Hakika hili ni jambo la ajabu.โ€ Wakasema (wale wajumbe- Malaika): Je! Unastaajabu amri ya Allah? Rehema ya Allah na Baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika (Allah) ndiye anayestahiki kusifiwa na kutukuzwa.โ€ (11:72-73).



Nabii Ibrahiim(a.s) aliwalea watoto wake kiharakati na aliwausia kumcha-Allah na kuendeleza harakati mpaka mwisho wa maisha yao.




(Kumbukeni habari hii) Mola wake alipomwambia: โ€œNyenyekea;โ€ akanena โ€œNimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu (wote)โ€. Na Ibrahimu akawausia haya wanawe; na Yaakubu (pia akawausia wanawe): โ€œEnyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuchagulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa wanyenyekevu.โ€ (2:131-132)



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1234

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰5 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana: