Navigation Menu



image

Mjadala juu ya ndoa ya Mtume Muhammad s.a.w na bi Khadija.

Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 16. Hapa utajifunza maandalizi wa mjadala wa ndoa hizi.

 


 


LAKINI UMRI WANGU MKUBWA
Baada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam). “Kwa nini nisimtake Muhammad aniowe? Inagawaje fikra hii ni mfano wa ndoto, lakini ni jambo linalowezekana. Lakini vipi? Nani atakayekubali kunifikishia ombi langu?” Alipokuwa katika hali ile, mlango ukagongwa.
“Nani anayegonga mlango?”
“Mimi dada yako Halah.”
Bibi Khadija akamkaribisha dada yake.
“Ahlan wa sahlan, karibu ewe Halah”
Halah:
“Ahsante Khadija vipi hali zenu?”
Khadija:
“Hatujambo, ziara hii ya ghafla naona.”
Khadija:
“Bila shaka ewe dada yangu, kwani nimekuja kukujulia hali yako tu”.
Khadija:
“Kuijua hali yangu tu! Mbona unasema maneno ya kiajabu, au kuna jambo unataka kunificha?”
Halah akamtizama dada yake mtizamo wa kuchunguza, kisha akamwambia:
“Abadan, hakuna la kukuficha isipokuwa mchana wa leo ulinichukuwa usingizi nikakuota unatembea mfano wa mtu aliyepotea katika njia ya kiza na nyuma yako sauti inakwambia: “Nenda mbele, nenda mbele”. Nikaona bora nije kukujulia hali yako, ingawaje sijuwi ndoto hiyo tafsiri yake nini”. Bibi Khadija (Radhiya Llahuu anha) akatabasamu kidogo kisha akasema:
“Kusema kweli mimi siku hizi ninaishi ndani ya mawazo mengi sana.”
Halah:
“Unawaza juu ya nini na wewe upo katika neema kubwa kama hii?”
Khadija:
“Muhammad, ewe dada yangu. Nafikiri juu ya sifa zake na utukufu wake ambao hajapata kuufikia hata mmoja katika watu wa kabila la Kikureshi.”
Halah:
“Na nini mwisho wa fikra hizo?”
Khadija:
“Nataka aniowe”.
Halah:
“Basi muombe akuowe”.
Bibi Khadija akamjibu kwa uoga:
“Naogopa asije akanikataa, kwani yeye ni kijana anayeheshimika kupita vijana wote”
Halah:
“Na wewe pia dada yangu ni mtu mtukufu unayeheshimika na watu wote”.
Khadija:
“Lakini umri wangu mkubwa unaokaribia miaka arubaini, na nishaolewa mara mbili, wakati yeye bado ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na mitano na bado hajapata kuowa. Vipi Muhammad atakubali kumuowa mwanamke aliye na umri sawa na mama yake aliyekwisha olewa mara mbili na ana watoto?”
Halah akasema:
“Nani aliyekujulisha na Muhammad mara ya mwanzo hata ukaweza kumpa mali yako aifanyie biashara?”
Khadija:
“Rafiki yangu mmoja anayeitwa Nafisa”.
Halah:
“Basi Nafisa huyo huyo ndiye atakayeweza kukufikishia ombi lako hilo”.
Kisha Halah akamuaga dada yake na kuondoka



ANAOLEWA NA MUHAMMAD
Ziara ya Hala ilikuwa mfano wa ufunguo wa kheri katika nafsi ya bibi Khadija (Radhiya Llahu anha), kwani siku ya pili yake Nafisa alipokuja kumtembelea bibi Khadija, akamhadithia juu ya mazungumzo yaliyopita baina yake na baina ya dada yake Halah, na Nafisa akakubali kuchukuwa jukumu la kulifikisha ombi hilo kwa Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam).



Alipoondoka, Nafisa alielekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Abu Talib alipokuwa akiishi Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam) na alipomuona akamwambia:


“Ewe Muhammad, wewe una umri wa miaka ishirini na tano na mpaka sasa bado hujaowa.”
Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akashangazwa sana na maneno hayo, akamuuliza:
“Kipi kilichokufanya ujishughulishe na jambo hili ewe Nafisa?
Nafisa:
“Bibi anayeheshimika anataka umuowe, nini rai yako?”
Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam):
“Bibi gani huyo?”
Nafisa:
“Bibi huyo ni Khadija binti Khuwaylid, na wewe unamuelewa vizuri juu ya heshima yake na utukufu wake na sifa zake zote njema”.
Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akasema:
“Naam, hakika yeye ni mtu anayeheshimika, lakini mimi sina mali hata niweze kumuowa.”
Nafisa;
“Yeye hana haja ya mahari, kwani unajuwa vizuri kuwa yeye hana shida ya mali na anao utajiri mkubwa”.
Muhammad:
“Mimi utajiri haunishughulishi, kwani mali inakuja na kuondoka, na Khadija pia ni mwanamke mzuri wa umbo na tabia na mwenendo, lakini niache nimshauri ami yangu kwanza juu ya jambo hili”. Ami yake akamwambia:


“Ewe Muhammad, hii ni bahati iliyokujia kutoka mbinguni. Naapa kuwa Khadija ni mwanamke aliyetakasika kupita wote katika Makka na mwenye akili na uwezo wa kupima mambo kupita wote, na mwenye hekima kupita wote na anayetokana na ukoo bora kupita wote. Wangapi wenye mali na jaha walitaka kumuoa akawakataa, na leo anakutaka wewe wakati huna mali yoyote, hii ni bahati kubwa.
Kubali ewe mwana wa ndugu yangu, kwani asingekutaka isipokuwa amekuwekea heshima kubwa sana”.
Muhammad (Swallah Llahu alayhi wa sallam) akakubali, na bibi Khadija akafanya arusi kubwa sana iliyohudhuriwa na watu wengi, na wanyama wengi sana wakachinjwa siku hiyo na kila muhitaji alifaidika.

 






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1978


Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰5 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Darsa za sira (maisha ya mtume jaribio la 01
Soma Zaidi...

Historia ya maimam Wanne wa fiqh
Soma Zaidi...

Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.
Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s. Soma Zaidi...

Maana ya kusimamisha uislamu katika dini
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME ZAKARIA(A.S) NA YAHYA(A.S)
Zakaria(a. Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA MTUME IDRISA (A.S)
Mtume aliyemfuatia Nabii Adam(a. Soma Zaidi...

tarekh
Soma Zaidi...

Historia ya Al-Khidhri
Jina Al-Khidhri halikutajwa mahali popote katika Qur’an. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME YUNUS(A.S)
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

Hatua mbili kuu za kushuka kwa Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuingia Kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Soma Zaidi...

Vipengele vya mkataba wa Hudaibiya na faida zake katika Ukombozi (ufunguzi) wa mji wa Makkah
Soma Zaidi...