Musa(a.s) Kuwaongoza Bani Israil Hadi Palestina
Baada ya matukio haya ndipo Musa(a.
Musa(a.s) Kuwaongoza Bani Israil Hadi Palestina
Baada ya matukio haya ndipo Musa(a.s) aliamuriwa kuwaongoza Bani Israil hadi Palestina. Aliwaongoza kupitia Taberah na Hazeroth hadi kwenye jangwa la Paran. Hapo Nabii Musa(a.s) alituma watu mashuhuri kufanya upelelezi Palestina. Baada ya siku arobaini ujumbe huu ulirejea na taarifa yao waliitolea sehemu iitwayo Kadesh. Taarifa za wajumbe wote ila wawili (Joshua na Caleb) ziliwakatisha tamaa. Hivyo wakagoma kuingia Palestina. Hawakutaka kabisa kutoa nafsi zao muhanga. Bali walitaka Allah(s.w) awatengenezee kila kitu wao waje tu kuvuna na kufaidi matunda. Kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
β(Musa(a.s) akasema): "Enyi watu wangu! Ingieni katika hiyo ardhi (nchi) iliyotakaswa ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni. Wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika". Wakasema: "Ewe Musa! Huko kuna watu majabari. Nasi hatutaingia huko mpaka watoke humo, wakitoka humo hapo tutaingia". Watu wawili miongoni mwa wale waliomwogopa (Allah) ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha, walisema (kuwaambaia wenzao). "Waingilieni katika hilo lango (la nchi yao); maana mtakapo waingilia hapo, kwa yakini nyinyi mtashinda. Na tegemeeni juu ya Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini". Wakaema: Ewe Musa! Sisi hatutaingia humo kamwe maadamu wao wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako mkapigane, sisi tutakaa hapa (kungojea nini litakalokuwa)" (5:21-24).
Baada ya ukaidi huu Nabii Musa(a.s) hakuwa na la kufanya tena bali kuleta dua ifuatayo:
(Musa) akasema: "Mola wangu! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu; basi tutenge na hawa mafasiki".(5:25)
Allah(s.w) aliwatia adabu kwa ukaidi wao; wakawa wanatangatanga Jangwani kwa muda wa miaka arobaini.
(Mwenyezi Mungu) akasema: "Basi wameharamishiwa (ardhi) hiyo kwa (muda wa) miaka arobaini, watatangatanga (mumu humu) ardhini (jangwani muda wote huo). Basi usihuzunike juu ya watu maasi" (5:26).
Basi Mayahudi hawa wakadumu kuhangaika majangwani bila kupumua. Kizazi kipya kilichochipuka baadaye wakawa na mwendo mzuri na utii. Wakapigana na majabari wa Palestina na wakatawala wao.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 ai web app π2 Simulizi za Hadithi Audio π3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π4 Kitabu cha Afya π5 Bongolite - Game zone - Play free game π6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Mbinu na njia walizotumia maadui wa uislamu dhidi ya waislamu na dola ya kiislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)
Katika Suratul Yassin Allah(s.
Soma Zaidi...Nabii Ibrahiim(a.s) Afanywa Kiongozi wa Harakati za Uislamu Ulimwenguni
βNa (kumbukeni habari hii) Mola wake alipomfanyia mtihani (Nabii) Ibrahiim kwa amri nyingi; naye akazitimiza.
Soma Zaidi...Mateso waliyoyapata waislamu wa mwanzo Maka, na orodha ya waislamu walioteswa vikali
Pili, Maquraish walimuendea Mtume(s.
Soma Zaidi...