Watu wa Lut(a.
Watu wa Lut(a.s) walipokataa kabisa kuonyeka kwa nasaha na maonyo ya Nabii Lut(a.s) na badala yake wakazidi kushabikia machafu na kupania kuwafanyia ubaya waumini, Allah(s.w) alipitisha hukumu yake ya kuwanusuru waumini na kuwaangamiza makafiri.
(Wale wajumbe) wakasema: “Ewe Lut! Sisi ni wajumbe wa Mola wako (Malaika). Hawatakufikia (kwa baya lolote). Na ondoka pamoja na watu wako katika sehemu ya pingapinga la usiku.Wala yoyote miongoni mwenu asitazame nyuma. Isipokuwa mke wako (mwanamke mbaya huyo hatakufuata). Naye utampata msiba utakaowapata hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Jee, asubuhi si karibu tu? (Basi tuliza moyo wako. Umekwishafika wakatiwao wa kuangamizwa).(11:81)
Basi ilipofika amri yetu, tulifanya (ardhi hiyo iwe juu chini); juu yake kuwa chini yake, na tukawateremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu (wa motoni uliyokamatana). (11:82) (Changarawe) zilizotiwa alama kwa Mola wako (kila moja kuwa ya mtu fulani). Na (adhabu) hii haiko mbali na madhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya). (11:83)
Jeshi la Allah lililotumika kuwaangamiza watu wa Lut(a.s) ni mvua ya changarawe kutokea motoni na kisha ardhi ikapinduliwa juu – chini.
Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. (48:7)
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri?
Soma Zaidi...Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Vita vya Ahzab- Maquraish waliungana na mayahudi, wanafiki na makabila mengine ya waarabu baada ya kuona kuwa wao peke yao hawawezi kuufuta Uislamu.
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 11
Soma Zaidi...