image

Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)

Katika Suratul Yassin Allah(s.

Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w)

Watu wa Mji Waliomuua Muislamu kwa Kuwa Amewasadikisha Wajumbe wa Allah(s.w).


Katika Suratul Yassin Allah(s.w) anatufahamisha habari za wale watu wa mji mmoja ambao walikataa kwa takaburi yao kumuamini Allah(s.w) baada ya kufikiwa na Wajumbe wake waliowajia kwa dalili wazi wazi. Wajumbe hao wa Allah(s.w) waliwaambia watu wa mji huo:

“............ Kwa yakini sisi tumetumwa kwenu” (36:16).

Watu wa mji huo walikadhibisha na kusema kama kawaida ya wakorofi wa enzi zote walivyosema:“..........Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi, wala (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa Rehema hakuteremsha chochote, nyinyi mnasema uwongo tu” (36:15).

Wajumbe wa Allah(s.w) bila ya kukata tamaa waliendelea kuwalingania na kuzidi kuwathibitishia kwa dalili wazi wazi kuwa wao ni wajumbe wa Allah(s.w). Waliwaambia:

“.........Mola wetu anajua bila shaka kuwa sisi tumetumwa kwenu. Wala hapana juu yetu ila kufikisha (ujumbe wetu) waziwazi” (36:16-17).Pamoja na jitihada za Wajumbe hawa kuwalingania watu wa mji huo kwa dalili waziwazi, watu wa mji huo walizidi kutakabari na kuazimia kuwadhuru Wajumbe wa Allah. Walitoa onyo kali kwao na kusema:


“...........Hakika sisi tumekorofika kwa ajili yenu. Kama hamtaacha (kusema haya mnayosema) tutakupigeni mawe na itakufikieni kutoka kwetu adhabu iumizayo” (36:18).Hii ndio tabia ya makafiri wa zama zote. Mara zote huwaona watu wema wanaolingania kheri ili ipatikane furaha na amani katika jamii kuwa ndio wakorofi na wavuruga amani. Huwapachikamajina mbali mbali ili waonekane mbele za watu kuwa wao ni wakorofi kweli ili wapate kisingizio cha kuwasukumiza gerezani au kuwaondoa kabisa katika ardhi. Bali makafiri ndio wakorofi, waharibifu katika ardhi na wavurugaji wakubwa wa amani na furaha katika jamii. Tabia yao hii Allah(s.w) anaidhihirisha katika Qur’an:
“Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi (katika jamii)”, Husema, “hakika sisi ni watengenezaji”. Hakika wao ndio waharibifu lakini hawatambui” (2:11-12).

Katika kisa hiki tunafahamishwa kuwa wale watu wakorofi wa mji ule waliokadhibisha ujumbe wa Allah(s.w) hawakuishia kutoa onyo kali tu bali walitekeleza kwa vitendo kwa mujibu wa habari ifuatayo:“Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mji, akasema (kwaambia watu wa mji ule), “Enyi watu wangu! Wafuateni wajumbe (hawa). Wafuateni hawa wanaokufundisheni bila ya kutaka ujira; na hali ya kuwa wenyewe wameongoka” (36:20-21). Wakamuuliza, “Kwani wewe umewafuata?” Akawajibu:“Kwanini nisimuabudu yule aliyeniumba (na kukuumbeni nyinyi pia) na kwake mtarejeshwa? Je! Nishike miungu wengine badala yake? Na kama Mwenyezi Mungu akipenda kunidhuru, uombezi wao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa! Nikifanya hivyo nitakuwamo katika upotofu ulio dhahiri. Bila shaka mimi nimemuamini Mola wenu, basi nisikilizeni” (36:22-25).Badala ya kuuzingatia ushauri wake mzuri na kuufuata, waliamua kumuua Muislamu yule. Mfano huu wa kudhulumiwa Waislamu kwa ajili tu ya kulingania waziwazi ujumbe wa Allah(s.w) na Mitume wake, haukuishia kwa watu wa mji ule tu, bali hiki ni kitendo kinachoendelea mpaka hivi leo. Katika mwaka 1993, tumeshuhudia mauaji ya dhuluma ya aina hii huko Misri, Algeria na Tunisia, kwa kisingizio cha “Waislamu wenye siasa kali”/Waislamu wenye imani kali”.Kwa upande mmoja, Mola wetu anatupa moyo na motisha kwa ahadi yake ya neema zisizo na kifani za huko peponi, ili tusimame imara na kuwa wagumu dhidi ya makafiri mpaka Dola ya Allah (Dini ya Allah) isimame katika jamii na iwe juu ya Dola ya makafiri japo watachukia mwisho wa kuchukia. Kama mfano kwetu, mara tu ya kuuliwa yule Mujahidina, alikaribishwa Peponi na Mola wake:“Akaambiwa: “Ingia Peponi. Akasema, laiti watu wangu wangelijua haya, wangelijua jinsi Mola wangu alivyonisamehe na kunijaalia miongoni mwa waliohishimiwa” (36:26-27).

Kamwe Muislamu wa kweli hapaswi kuwaogopa makafiri na wapinzani wote wa usimamishaji wa Uislamu katika jamii, kwani hakuna kifo cha heshima na taadhima mbele ya Allah(s.w) kuliko kifo cha Shahidi kiasi kwamba Allah(s.w) anatukataza kumuita mfu aliyekufa shahidi.
“Wala msiwaite wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu wafu, bali wa hai, lakini nyinyi hamtambui” (2:154).

Kwa upande mwingine, tunafahamishwa wazi wazi, kwa mifano mingi kuwa hatima ya makafiri na wapinzani wa Uislamu ni kuangamia hapa duniani na huko akhera. Hapa duniani watadhibitiwa au kufutiliwa mbali kabisa na Allah(s.w) kwa urahisi sana. Hahitajii Allah(s.w) kuandaa jeshi kubwa lenye silaha kali katika kuwadhibiti makafiri. Katika kisa hiki, Allah(s.w) anatufahamisha:
“Na hatukuwateremshia watu wake jeshi kutoka mbinguni (kuwaangamiza) baada yake, wala hatukuwa wateremshao (majeshi kutoka mbinguni). Basi hakukuwa (kuangamizwa kwao) ila kwa ukulele mmoja tu, na mara wakawa waliozimika” (36:28-29).Kutokana na kisa hiki na visa vingine vilivyohadithiwa katika Qur’an tunajifunza kuwa daima katika kipindi chote cha historia wanaadamu wamekuwa wakigawanyika katika makundi mawili makubwa baada ya kufikiwa na Ujumbe wa Allah(s.w). Kundi la wenye kuwaamini Mitume na kufuata ujumbe wao na kundi la makafiri waliowakataa Mitume na kuukanusha ujumbe wao.Kundi la waumini huanza na watu wachache na wanyonge, wenye kukandamizwa na makafiri, lakini kila baada ya siku, kulingana na juhudi zao za kuulingania Uislamu na kujitoa muhanga kwao kwa mali na nafsi zao katika kuusimamisha, waliongezeka na kuwa nguvu dhidi ya maadui zao na hatimaye walishinda na kuusimamisha Uislamu katika jamii.Kundi la makafiri daima huanza na watu wengi wenye mamlaka na hadhi katika jamii, lakini kila baada ya siku, kulingana na ukweli unaodhihirishwa na Uislamu, idadi yao ilizidi kupungua na vitimbwi vyao kubainika na kudhibitiwa na Waislamu hatimaye kuporomoka na kuwa chini ya himaya ya Uislamu na kutoa jizya. Pale ambapo makafiri walipindukia mipaka na kutakabari katika ardhi kiasi cha kutowaruhusu kabisa waumini kuligania Dini ya Allah(s.w) na kuongeza idadi yao, kama walivyokuwa makafiri wa wakati wa Nabii Nuhu, Lut, Salihi, Shuayb(a.s), n.k. Allah(s.w) aliwdhibiti mwenyewe na kuwafuta katika ardhi.Hivyo,mafunzo haya tunayoyapata kutokana na historia ya mwanaadamu kama inavyodhihirishwa Qur’an, Waislamu wa kweli hatunabudi kufuata vilivyo ujumbe wa Mitume na kufuata nyayo zao na za wale watu wema waliokuwa pamoja nao, katika kuilingania na kuipigania Dini ya Allah(s.w)kwa mali zao na nafsi zao. Kamwe hatutapokelewa mbele ya Allah(s.w) kwa kuwaamini tu Mitume bila ya kufuata nyayo zao na wale watu wema walioamini pamoja nao katika kupigania Dini ya Allah(s.w). Mola wetu anatukumbusha hili katika Qur’an:
“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, na hali hamjajiwa na mfano wa (yale yaliyowajia) wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara na wakatetemeshwa sana hata Mitume na walioamini pamoja nao wakasema: “Nusura ya Allah itafika lini?” jueni kuwa nusura ya Allah iko karibu” (2:214).Hatunabudi kufahamu wazi kuwa, tukifuata vilivyo nyayo za Mitume na wale walioamini pamoja nao katika kumtii Allah(s.w) na kupigania kusimama kwa Uislamu katika jamii kwa mali zetu na nafsi zetu ushindi ni wetu na makafiri kamwe hawataweza kuufuta Uislamu katika jamii. Hebu tuirejee Qur’an kwa makini katika aya zifuatazo:
“Yeye ndiye Aliyemtuma (Aliyemleta) Mtume Wake (Nabii Muhammad) kwa uwongofu na kwa Dini ya haki ili kuifanya ishinde Dini zote, ijapokuwa washirikina watachukiwa”.
Enyi Mlioamini! “Je! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo?”. (Basi biashara yenyewe ni hii): Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na piganieni Dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu; ikiwa mnajua (kuwa ni bora, basi fanyeni)”.(Mkifanya haya) Atakusameheni dhambi zenu na atakuingizeni katika Mabustani yapitayo mito mbele yake na (Atakupeni) maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele: huku ndiko kufuzu kukubwa”. Na (Atakupeni) kingine mnachokipenda: nayo ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu na ushindi ulio karibu! Na wapashe habari njema Waislamu” (61:9-13).                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 289


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Uendeshaji na Kupanuka kwa Dola ya Kiislamu Kipindi cha Makhalifa Waongofu
Soma Zaidi...

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...

Kazi alizokuwa akizifanya Mtume Muhammad s.a.w kabla ya utume.
Historia na sifa ya Mtume Muhammad s.a.w , sehemu ya 14. Hapa utajifunza kuhusu kazi alizozifanya Mtume s.a.w Enzo za ujana wake kabla ya utume. Soma Zaidi...

NI IPI FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA NI IPI NASABA YAKE, UKOO WAKE NA KABILA LAKE
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Soma Zaidi...

tarekh 08
KULELEWA NA MAMA YAKE ALIPOFIKA MIAKA MINNEMtume (s. Soma Zaidi...

Kufunguliwa Yusufu(a.s) Kutoka Gerezani
Yusufu(a. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Bani Israil
Soma Zaidi...

CHANZO CHA VITA VYA VITA VYA AL-FIJAR NA ATHARI ZAKE
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU). Soma Zaidi...

tarekh
Soma Zaidi...

Mpango wa kumuuwa Khalifa ally na Gavana Muawiya
Soma Zaidi...