Utangulizi


Tabii Tabiina ni wafuasi wa Tabiin au wafuasi wa wajukuu wa maswahaba.


Wanazuoni katika kipindi cha Tabiina, wakiwemo maimamu wanne wa Fiq-h, walijitahidi sana kukusanya Hadith za Mtume (s.a.w) lakini kazi zao hazikuweza kukidhi mahitaji yote ya kuendea kila kipengele cha maisha ya kibinafsi na kijamii. Kwa mfano kitabu cha Imamu Malik, Al-muwatta,kilichokuwa mashuhuri sana katika enzi hizo kiligusia baadhi ya mambo tu yakiwemo yale ya Ibada maalumu za swala,swaumu,Zakat na Hija. Pamoja na mapungufu haya pia iligundulika kuwa katika kipindi cha Tabiina zilizushwa Hadith za uwongo maelfu kwa maelfu.


Katika kupunguza mapungufu haya wanazuoni katika kipindi cha Tabii Tabiin walijishughulisha sana na kukusanya na kuandika Hadith kuhusu nyanja zote za maisha ya muiislamu. Pia ili kuhakikisha usahihi wa Hadith walizozikusanya na kuziandika walichukua tahadhari kubwa sana katika kuzichuja. Katika kipindi hiki walitokea maimamu mashuhuri sita waliojitahidi na kutumia sehemu kubwa ya maisha yao katika kukusanya,kuchuja na kuandika Hadith.


Maimamu hawa ni: Bukhari, Muslim, Abu Daud, Nasai, Ibn Majaha na Tirmidh. Walisafiri masafa marefu kwa ajili ya kazi hii ya ukusanyaji Hadith na ilibidi wajifunze tabia ya wapokezi kadhaa wa Hadith kabla hawajaiandika. Sio kila Hadith waliyoambiwa waliiandika bali kulikuwa na utaratibu wa kuchambua Hadith iliyo sahihi na isiyo sahihi kwa kuzingatia tabia za wasimulizi na vigezo vya matini ya Hadith. Kutokana na jitihada zao za uchujaji wa Hadith, vitabu vyao vilijulikana kwa jina la “Sitta Sahihi”. Kila Imamu wa Hadith alivyozidi kuwa muangalifu katika uchujaji wa Hadith zake alizozikusanya ndivyo kitabu chake kilivyopewa daraja ya juu ya usahihi. Vitabu sita mashuhuri vya Hadith sahihi vilivyoandikwa na maimamu hao ni: